Chadema kushindwa kusimamia agenda zao

Chadema kushindwa kusimamia agenda zao

point taken, kujundu cha watu wachache kinalazimisha mawazo yao yafuatwe, chama cha demokrasia
 
Wana jf kwanza niwaombe wale wote ambao labda walijiunga na mtandao huu kwa bahati mbaya basi wausome tu huu uzi wasichangie. wawaachie wale wenye uono mpana wajaribu kutoa maoni yao pamoja kudadavua zaidi ili labda kama nitakuwa nimekosea nipate sababu yakujirekebisha.
Ni kiri kwa uwazi kabisa kwamba wakati wa Uchaguzi mkuu uliopita, nilipiga kura zangu zote tatu kwa CHADEMA. Yaani kura ya Uraisi kwa SLAA, Ubunge pamoja na Udiwani zote niliwapigia CHADEMA. Niliwapa kura zangu nikiamini kabisa nilikuwa napigia kura mabadiliko. Nakumbuka Makala ya Gazeti la Raia Mwema la Alhamisi ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu iliyokuwa na kichwa cha Habari "HERI WATAKAO CHAGUA MABADILIKO" iliyoandikwa na mwandishi Jonson Mbwambo, ilivyonivutia na kunihamisisha kupigia kura mabadiliko.
Nilijitahidi kuhamasisha wengine kuanzia kwenye familia, marafiki, majirani na kila kijiwe nilichoweza kuwepo ili nao wapigie kura mabadiliko, na mabadiliko hayo yalionekana ndani ya CHADEMA. Hatukuishia kupiga kura tu, bali tulihakikisha tunazifuatilia kura zetu. Nakumbuka jioni ile wakati kura zinahesabiwa ndani huku nje vijana tulikuwa na mihemko ya ajabu na kila mara tukiwasiliana na makamanda waliokuwa ndani kama mawakala huku wakitujibu tusiwe na wasiwasi kwani mambo ni mazuri. Kama ni experience ya UKAMANDA basi wakati ule ukamanda wangu ulikuwa wa kiwango cha juu sana.
Lakini CHADEMA kushindwa kuzisimamia AGENDA wanazo zianzisha ndiko kunakonifanya nifikirie upya kuhusu kuwapa tena kura zangu hapo mwakani Mungu akitupa uhai katika uchaguzi Mkuu. Agenda nyingi wanazo zianzisha huwa zinaishia hewani. Mfano wa agenda hizo ni hizi zifuatazo.

1. KUTOKUMTAMBUA RAIS KIKWETE.
Ikumbukwe kwamba, mara baada ya matokeo yote ya Urais kujumlishwa pamoja na kumpa ushindi JK, CHADEMA walitangaza rasmi kutoyatambua matokeo hayo na kutomtambua Raisi JK. Nakumbuka CHADEMA haikushiriki katika hafla ya kutangaza matokeo rasmi ya uraisi, haikushiriki katika sherehe za kuapishwa kwa raisi Kikwete. Na tukio kubwa ni lile la Wabunge wote wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge mara tu Raisi Kikwete aliposimama ili kulihutubia bunge hilo kwa mara ya kwanza. Lakini mimi sikumbuki ni lini CHADEMA walibadilisha msimamo, na kama kweli waliutangazia umma wa watanzania kwamba wamebadili msimamo na kuanza kumtambua Raisi Kikwete kama Raisi wao pia. Kilichotushangaza ni wao CHADEMA kuukubali mualiko wa kwenda Ikulu kuonana na Raisi JK ili kujadili hatima ya muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba. Kwa wao kukubali kwenda Ikulu kuonana na kujadiliana na kukubaliana mambo kadhaa na Raisi Kikwete, haihitaji akili ya darasani kufahamu kwamba WALISHAAMUA KUBADILISHA MAAMUZI NA KUMTAMBUA RASMI KIKWETE kama Raisi halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nini kilitokea hadi wakaamua kubadili msimamo hakijulikani na wala wanachadema na makamanda watiifu hatujawahi kuelezwa. Agenda hiyo ikaishia hewani.

2. KATIBA MPYA.
Ikumbukwe kwamba suala la katiba mpya lilikuwa ni moja ya agenda za CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu uliopita. Mgombea uraisi wa CHADEMA akaahidi waziwazi kwamba ndani ya siku mia moja za kuwa ofisini, angewapatia wananchi katiba mpya(labda alikuwa anatania). Moja ya sababu kuu za kudai katiba mpya ilikuwa ni kuhakikisha rasilimali za taifa zinalindwa kwa manufaa ya wananchi wote wa taifa hili. Lengo kuu lingine lilikuwa ni kuhakikisha kwamba katiba inaweka miiko imara ya uongozi ili kuminya mianya ya ufisadi. kwakweli hayo mpaka leo bado ndiyo mahitaji makubwa ya wananchi wanyonge wa taifa hili. Na CHADEMA walitegemewa wayatetee iwe kwenye serikali moja, mbili au hata hizo tatu. suala la idadi ya serikali kama ziwe tatu au mbili au moja halikuwepo kabisa wakati ule. Ukweli ni kwamba idadi ngapi za serikali tuwe nazo, ni kwasababu tu ya interest za viongozi(vyeo) na si wananchi. Kwa kuususia mchakato wa katiba kwasababu ya idadi ya serikali, ni sawa na kutupilia mbali interest za wanyonge ambazo mlizibeba wakati ule na kugeukia interest za madaraka ya uongozi. Tunaamini kwamba Rasilimali za wananchi zinaweza kulindwa katika serikali moja, mbili na hata tatu. Maadili ya uongozi yanaweza kupewa makali katika serikali moja, mbili na hata tatu. Usawa wa 50% kwa 50% unaweza kuwepo katika serikali moja, mbili na hata tatu. Maendeleo makubwa ya kiuchumi yana weza kupatikana katika serkali moja, mbili na hata tatu. Sasa iweje mshindwe kusimamia mahitaji muhimu ya wanyonge kwasababu moja tu ya idadi za serikali??? hapo agenda kuu mlioianzisha ya katiba mpya mmeiacha hewani na kuwaacha wanyonge tumeduwaa.

3. MAANDAMANO.
Ikumbukwe pia kwamba Mwenyekiti taifa wa CHADEMA Mh. Mbowe alitangaza maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima ili kupinga kuendelea kwa bunge la katiba. Na akaenda mbele zaidi kwa kusema maandamano hayo ni lazima yafanyike hata kama yatakosa kibali toka kwa jeshi la polisi. Siku ya kuanza maandamano, tunaambiwa Mbowe amesafiri kwenda Afrika ya kusini, Vijana kadhaa wakajikuta peke yao ndio waratibu wa maandamano hayo huku kukiwa na ukimya wa Mwenyekiti na Viongozi wake wa kitaifa. Hadi naandika bandiko hili sijamsikia Mbowe au kiongozi yeyote akisema kama yaliahirishwa au kumetokea nini hadi kushindwa kwa AGENDA hii nayo inayoishia hewani kama nyingine.

Wakuu hiyo ni mifano ninayoikumbuka ambayo ni AGENDA za kitaifa ambazo CHADEMA walizianzisha lakini zikaishia hewani huku wananchi wakiachwa kwenye mataa. Hebu tujadili kuna sababu zipi zinazo wakwamisha?? je, wanaweza kuaminiwa na wananchi wawabebee agenda zao. Jadili!
NB. kwa wale ambao kwao wao kila bandiko lenye changamoto kwa CHADEMA basi limefadhiriwa na Lumumba basi hatuwalaumu, wao ni akili ndogo tutawapuuza)!

thegame

Mkuu CHADEMA ni chama cha siasa za matukio.
Matukio yameisha na chama kimeisha umaarufu, na sasa wameamuka kujibanza nyuma ya Ukawa
 
Matukio yameisha na chama kimeisha umaarufu, na sasa wameamuka kujibanza nyuma ya Ukawa ku-boost popularity!
 
CHADEMA inaonekana ndicho chama pekee ambacho kimeamua kuwapigania watanzania kwa moyo wadhati kabisa.Ndiyo maana kinabuni mbinu mbalimbali zenye lengo la kuwakomboa watanzania ili waondokane na utawala wa kifisadi wa CCM.Japo kuwa wapo wanaobeza kazi zinazofanywa na CHADEMA wengine ni wanachama wenyewe wa CHADEMA kwa vile palipo na wengi tofauti za kimtazamo lazima zitokee.Kazi ya kuwapigania wananchi na juhudi zinazofanywa na CHADEMA wananchi wengi wameziona na ndio watakaochagua mbichi na mbivu.
 
Mimi napenda mageuzi, lakini kwa type ya CHADEMA hapana.
Tatizo la hawa watu, wengi wanaendeshwa na bhangi. Si kwa viongozi, tena wa nafasi za juu kabisa wala kwa washahabiki wao.
Wanadhania politics ni kupiga makerere na kufanya unscientific violations.
Tujirekebishe, nafasi tunayo bado.
 
WEwe unayejiita ASSADSYRIA3 form 4 umemaliza lini? kama ni wakati huu wa division 5 sikushangai maana hujui hata MAANA YA neno STATIC . sasa hapo unawatukana hao uliowalenga au unawasifia? inawezekana nyie ndio mnaoenda kusaign mikataba nje na mkirudi mnajisifia kumbe mmeuza nchi na rasilimali zake

Tena inawezekana wewe ni THINK TANK ya chama fulani na akina nyie ndio washauri wa viongozi wa nchi hii. hebu nenda kasome angalau tuitsheni ya wiki moja angalau ujue kutofautisha kati ya neno STATIC na STAGNANT
 
Mod mmeamisha topic yangu kwenye hii wakati maudhui nitofauti kabisa je huwa mnatumia vigezo gani nasio maramoja naomba kujuwa vigezo
 
Thegame,

..naomba kutofautiana na maelezo yako. nadhani kwa kiasi kikubwa umeshindwa kuelewa ni nini malengo ya CDM na njia gani inapaswa kutumika kufikia malengo hayo.

..kutokana na udogo wa CDM, pamoja na uchache wa wabunge walionao, basi lazima CDM watumie mbinu za kiunaharakati kuliko mbinu za kibunge.

1.KUTOMTAMBUA RAISI:

..ile ilikuwa hatua nzuri tu ambayo ili-draw attention kwa watawala kuanza kuwasikiliza CDM. moja ya malalamiko ya CDM yalikuwa ni jinsi ambavyo uchaguzi ule uliendeshwa, na utendaji mbovu wa tume ya uchaguzi.

..Raisi alilazimika kuwasilikiza CDM na ndiyo maana kukawa na mkutano wa Ikulu. Raisi angeweza kusema hawezi kukutana na chama ambacho hakimtambui, lakini akaamua kukutana nao bila masharti.

..Kwa hiyo utaona kwamba mkutano wa "kunywa juice" Ikulu umewezesha kujenga mazingira na imani kwamba CDM wanamtambua Raisi, that is a positive kwa JK.

..Kwa upande wa CDM mkutano wa "kunywa juice" umewawezesha kupenyeza ajenda zao kwa watawala na kumlazimisha JK kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CDM kwa kuanzisha mchakato wa katiba mpya, which is a positive kwa CDM.

2.KATIBA MPYA:

..marekebisho ya katiba ya Tanzania ni tofauti kwa kiasi kikubwa na marekebisho ya katiba ya mataifa mengine kama Kenya, Uganda, Zimbabwe, etc. Tofauti yetu na mataifa hayo ni kwamba Tanzania ni Jamhuri ya MUUNGANO.

..kwa msingi huo unapotaka kurekebisha katiba yetu ni lazima kwanza ushughulike na suala la MUUNGANO, muundo wake ambao unahusisha idadi ya serikali, idadi ya mabunge, pamoja na muundo wa mahakama.

..baada ya hatua hiyo niliyoieleza hapo juu ndipo unapoweza kushughulika na masuala kama maadili ya viongozi, ulinzi wa rasilimali, haki za wakulima, wafugaji, wavuvi, na makundi mengine mbalimbali katika jamii.

..siyo kweli kwamba suala la maadili ya viongozi, ulinzi wa rasilimali, na haki za makundi kama uwakilishi wa 50/50, etc etc yanaweza kushughulikiwa bila kujali idadi ya serikali. Katiba yetu ni lazima ielekeze masuala hayo yanashughulikiwa ktk level ya serikali ya muungano, au katika level ya serikali za washirika wa muungano.

3.MAANDAMANO:

..Maandamano yalitangazwa na chama kupitia mwenyekiti. kama mwenyekiti alisafiri haimaanishi kwamba chama nacho kinakwenda safari na shughuli zote zinakwama. mandela alihukumiwa kwenda jela maisha lakini harakati za ANC hazikukoma.

..Kama maandamano yameshindwa kufanyika kutokana na shinikizo la POLISI basi chama kinapaswa kuja na mbinu mbadala. Labda badala ya maandamano wafanye mikutano mingi zaidi ya hadhara, na kutoa elimu ya uraia nyumba kwa nyumba.

cc Ritz, Nguruvi3
 
Historia inaonyesha kuwa wakati ambapo tawala zote katika nchi husika ikiwa ipo katika hali ya kiburi na ubabe mkubwa ndipo mabadiliko hutokea na mara zote mabadiliko hayo huanzishwa na mtu mmoja katika mazingira yasiyotegemewa,yamkini inawezekana mabadiliko hayo yakaanzishwa na mkaanga samaki mmoja pale soko la feri hapo dar es salaam,ni swala la muda tu..
 
Wana jf kwanza niwaombe wale wote ambao labda walijiunga na mtandao huu kwa bahati mbaya basi wausome tu huu uzi wasichangie. wawaachie wale wenye uono mpana wajaribu kutoa maoni yao pamoja kudadavua zaidi ili labda kama nitakuwa nimekosea nipate sababu yakujirekebisha.
Ni kiri kwa uwazi kabisa kwamba wakati wa Uchaguzi mkuu uliopita, nilipiga kura zangu zote tatu kwa CHADEMA. Yaani kura ya Uraisi kwa SLAA, Ubunge pamoja na Udiwani zote niliwapigia CHADEMA. Niliwapa kura zangu nikiamini kabisa nilikuwa napigia kura mabadiliko. Nakumbuka Makala ya Gazeti la Raia Mwema la Alhamisi ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu iliyokuwa na kichwa cha Habari "HERI WATAKAO CHAGUA MABADILIKO" iliyoandikwa na mwandishi Jonson Mbwambo, ilivyonivutia na kunihamisisha kupigia kura mabadiliko.
Nilijitahidi kuhamasisha wengine kuanzia kwenye familia, marafiki, majirani na kila kijiwe nilichoweza kuwepo ili nao wapigie kura mabadiliko, na mabadiliko hayo yalionekana ndani ya CHADEMA. Hatukuishia kupiga kura tu, bali tulihakikisha tunazifuatilia kura zetu. Nakumbuka jioni ile wakati kura zinahesabiwa ndani huku nje vijana tulikuwa na mihemko ya ajabu na kila mara tukiwasiliana na makamanda waliokuwa ndani kama mawakala huku wakitujibu tusiwe na wasiwasi kwani mambo ni mazuri. Kama ni experience ya UKAMANDA basi wakati ule ukamanda wangu ulikuwa wa kiwango cha juu sana.
Lakini CHADEMA kushindwa kuzisimamia AGENDA wanazo zianzisha ndiko kunakonifanya nifikirie upya kuhusu kuwapa tena kura zangu hapo mwakani Mungu akitupa uhai katika uchaguzi Mkuu. Agenda nyingi wanazo zianzisha huwa zinaishia hewani. Mfano wa agenda hizo ni hizi zifuatazo.

1. KUTOKUMTAMBUA RAIS KIKWETE.
Ikumbukwe kwamba, mara baada ya matokeo yote ya Urais kujumlishwa pamoja na kumpa ushindi JK, CHADEMA walitangaza rasmi kutoyatambua matokeo hayo na kutomtambua Raisi JK. Nakumbuka CHADEMA haikushiriki katika hafla ya kutangaza matokeo rasmi ya uraisi, haikushiriki katika sherehe za kuapishwa kwa raisi Kikwete. Na tukio kubwa ni lile la Wabunge wote wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge mara tu Raisi Kikwete aliposimama ili kulihutubia bunge hilo kwa mara ya kwanza. Lakini mimi sikumbuki ni lini CHADEMA walibadilisha msimamo, na kama kweli waliutangazia umma wa watanzania kwamba wamebadili msimamo na kuanza kumtambua Raisi Kikwete kama Raisi wao pia. Kilichotushangaza ni wao CHADEMA kuukubali mualiko wa kwenda Ikulu kuonana na Raisi JK ili kujadili hatima ya muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba. Kwa wao kukubali kwenda Ikulu kuonana na kujadiliana na kukubaliana mambo kadhaa na Raisi Kikwete, haihitaji akili ya darasani kufahamu kwamba WALISHAAMUA KUBADILISHA MAAMUZI NA KUMTAMBUA RASMI KIKWETE kama Raisi halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nini kilitokea hadi wakaamua kubadili msimamo hakijulikani na wala wanachadema na makamanda watiifu hatujawahi kuelezwa. Agenda hiyo ikaishia hewani.

2. KATIBA MPYA.
Ikumbukwe kwamba suala la katiba mpya lilikuwa ni moja ya agenda za CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu uliopita. Mgombea uraisi wa CHADEMA akaahidi waziwazi kwamba ndani ya siku mia moja za kuwa ofisini, angewapatia wananchi katiba mpya(labda alikuwa anatania). Moja ya sababu kuu za kudai katiba mpya ilikuwa ni kuhakikisha rasilimali za taifa zinalindwa kwa manufaa ya wananchi wote wa taifa hili. Lengo kuu lingine lilikuwa ni kuhakikisha kwamba katiba inaweka miiko imara ya uongozi ili kuminya mianya ya ufisadi. kwakweli hayo mpaka leo bado ndiyo mahitaji makubwa ya wananchi wanyonge wa taifa hili. Na CHADEMA walitegemewa wayatetee iwe kwenye serikali moja, mbili au hata hizo tatu. suala la idadi ya serikali kama ziwe tatu au mbili au moja halikuwepo kabisa wakati ule. Ukweli ni kwamba idadi ngapi za serikali tuwe nazo, ni kwasababu tu ya interest za viongozi(vyeo) na si wananchi. Kwa kuususia mchakato wa katiba kwasababu ya idadi ya serikali, ni sawa na kutupilia mbali interest za wanyonge ambazo mlizibeba wakati ule na kugeukia interest za madaraka ya uongozi. Tunaamini kwamba Rasilimali za wananchi zinaweza kulindwa katika serikali moja, mbili na hata tatu. Maadili ya uongozi yanaweza kupewa makali katika serikali moja, mbili na hata tatu. Usawa wa 50% kwa 50% unaweza kuwepo katika serikali moja, mbili na hata tatu. Maendeleo makubwa ya kiuchumi yana weza kupatikana katika serkali moja, mbili na hata tatu. Sasa iweje mshindwe kusimamia mahitaji muhimu ya wanyonge kwasababu moja tu ya idadi za serikali??? hapo agenda kuu mlioianzisha ya katiba mpya mmeiacha hewani na kuwaacha wanyonge tumeduwaa.

3. MAANDAMANO.
Ikumbukwe pia kwamba Mwenyekiti taifa wa CHADEMA Mh. Mbowe alitangaza maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima ili kupinga kuendelea kwa bunge la katiba. Na akaenda mbele zaidi kwa kusema maandamano hayo ni lazima yafanyike hata kama yatakosa kibali toka kwa jeshi la polisi. Siku ya kuanza maandamano, tunaambiwa Mbowe amesafiri kwenda Afrika ya kusini, Vijana kadhaa wakajikuta peke yao ndio waratibu wa maandamano hayo huku kukiwa na ukimya wa Mwenyekiti na Viongozi wake wa kitaifa. Hadi naandika bandiko hili sijamsikia Mbowe au kiongozi yeyote akisema kama yaliahirishwa au kumetokea nini hadi kushindwa kwa AGENDA hii nayo inayoishia hewani kama nyingine.

Wakuu hiyo ni mifano ninayoikumbuka ambayo ni AGENDA za kitaifa ambazo CHADEMA walizianzisha lakini zikaishia hewani huku wananchi wakiachwa kwenye mataa. Hebu tujadili kuna sababu zipi zinazo wakwamisha?? je, wanaweza kuaminiwa na wananchi wawabebee agenda zao. Jadili!
NB. kwa wale ambao kwao wao kila bandiko lenye changamoto kwa CHADEMA basi limefadhiriwa na Lumumba basi hatuwalaumu, wao ni akili ndogo tutawapuuza)!

thegame

1, Chadema waliamua kutoka Bungeni kwa lengo la kumuonyesha Kikwete mfumo uliotumika kumuweka madarakani sio haukubaliki na tunaka katiba ibdilishwe ili haki ionekane, - Jambo la muhimu hapa ujumbe ulifka na Rais Kikwete alianzisha mchakato wa Katiba

2, Mchakato wa Katiba ulianza vizri, wote tumeshuhudia jinsi Warioba alivyokusanya maoni Tanzania nzima na akawasilisha kwa Rais Kikwete, Rasimu ya kwanza, Rais akapongeza, Rasimu ya Pili akaipongeza.... kuja Bungeni kikatokea kituko cha Bunge nalo kukusanya maoni! mbaya zaidi wakimtukana Mzee Warioba!.. hii ni kwa kuwa wao CCM hawakujipanga kidhati kuleta katiba ila walilazimika sababu Chadema ilidai katiba, pia wakaona ni mradi wa kupatia posho

kwa hilo wameanikiawa 100% maana posho wamezipata za kutosha!

3, Kuhusu maandamo, maandamano yapo palepale maandamano ni sehemu ya siasa na hatusubiri serikali itupende itupe ulinzi, CCM wanafanya maandamano na mikutano sehemu mbalimbali nchini, wao wanaruhusiwa ila chadema ni dhambi
hoja za kuandamana zipo nyingi, ambazo hakuna jaji atakayemfunga yeyote

hakuna jaji atamfunga mwanachadema kisa ameandamana kudai maoni yake hayakusikilizwa! serikali imetangaza uchaguzi serikali za mitaa na wametoa tarehe za kampeni na uchaguzi, ila hawakutoa kanuni, ni jaji yupi atamfunga mwanachadema kwa kuandamana kudai kanuni?

HAKI HAIOMBWI,
 
Back
Top Bottom