Duh!unatamani Chadema ikubalike mbaka nchi jirani,mimi nafikiri kukubalika kwa chadema huku Tanganyika inatosha sana!.Kwa kuwa Zanzibar ni nchi jirani tuliyoungana nayo,na naamini ipo siku muungano utakufa!!!
Mimi naona Chadema ifungue makanisa mengi ya pentekost zanzibar hiyo tu itasaidia
sio tu kwa chadema bali dunia nzima kila chama kinakuwa na ngome zake hata ukienda marekani utakuta chama fulani kina washabiki wengi katika majimbo fulani, cha msingi ingawa chama kinaweza kutokubalika sehemu fulani lakini sera za chama hicho zinabidi kujali pande zote yani kinapokubalika na kisipokubalika
muungano umeshakufa siku waliposaini muafaka na zanzibar kuwa nchi kamili. kilichobaki ni tanganyika kujitambua na kuunda serikali yake ambayo imeshabaki yatima baada ya wazanzibar kujitoa kimyakimya.sasa unataka chadema waende zanzibar kufanya nini?
na kwa taarifa yako cuf ya zanzibar na ya bara ni vitu tofauti,ya bara ni ya lipumba na ya zanzibar ni ya seif
mtake msitake hakuna tena kitu inayoitwa tanzania labda kwa kujidanganya tu.
natambua umuhimu wa chama kujitanua katika nchi njima lakini vitu kama hivyo vinahitaji fedha nyingi na mikakati ya kudumu, nadhani ni muda huu kabla ya uchaguzi wa 2015 chadema inatakiwa kujijenga nchi nzima kwani itakuwa na wabunge zaidi ya 40, na ruzuku ya kutosha kujifungulia matawi katika wilaya na kata katika taifa letu pia na ccm inatakiwa kujijenga pemba piaDuniani kuna vyama vikubwa na vidogo. Mfano Republican na Democratics kwa USA; hali kadhalika UK. Vyama hivi vikubwa vina ushawishi nchi nzima. Sama kama CHADEMA sasa ni chama kikubwa lazima kienee nchi nzima.
Mh. Tukutuku, DR Slaa alikuwa anagombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na siyo wa Tanganyika. Hatuwezi kuwa na raisi anayekubalika kwenye eneo moja tuu la Muungano
Hata Kibaki hakubaliki kwa Waluo, Obama hakubaliki State nyingi tu na Museven hakubaliki kwa waacholi pia Kumbuka Kikwete hatumkubali hapa Arusha na hata kijijini kwetu kule Kilimanjaro, pia Kikwete hakubaliki Bukoba, maeneo mengi tu ya Mwanza,Shinyanga n.k
after all Zanzibar ni nchi inayofanyiwa ukoloni na Tanganyika very soon watajitenga. Hakuna haja ya Chadema kupoteza resources kwa nchi inayotegemea kujitema muda wowote kuanzia sasa.