Chadema kushindwa kupenya visiwani nini kifanyike kwa maandalizi ya 2015

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,269
4,569
Pamoja na mafanikio ambayo Chadema imeyapata katika uchaguzi wa mwaka huu 2010, bado CHADEMA kama ilivyo CUF kinakubalika sehemu moja ya upande wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kukubalika huku upande mmoja wa Muungano pekee kutawafanya washindwe kuunda serikali inayoshirikisha pande zote za Muungano hata kama watashinda uchaguzi mkuu. Tofauti na ilivyo nchi jirani ya Kenya, hakuna uzoefu wa kuunganisha vyama ili kufikia malengo ya kutwaa dola haraka.

Kwa mwenendo wa kukubalika kwa vyama vya CUF na CHADEMA kimoja visiwani na kingine bara, endapo vyama hivi vingeungana chama ambacho kingezaliwa kingekuwa na ushawishi mkubwa visiwani na bara na hivyo kuwa chama mbadala.

Ni bahati mbaya kwa CHADEMA kwamba CCM visiwani wameshachukua hiyo fursa na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na CUF kule visiwani. Hii inaifanya CHADEMA kukosa chama makini kinachokubalika visiwani ambacho ingeweza kuungana nacho ili kuweza kupenya kwenye siasa za visiwani. Hata hivyo kwa kuwa uchaguzi wa 2010 umekwisha, CHADEMA kama chama inabidi kitafakari sana kura ilizoambulia visiwani na mikoa ya pwani na kuchukua hatua madhubuti kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa 2015.

Mojawapo ya hatua inayoweza kuchukua ni pamoja na kuunganisha nguvu na moja ya vyama vilivyoshiriki uchaguzi chenye ushawishi katika siasa za visiwani hata kama hakikuambulia jimbo lolote.

Chama kama Jahazi Asilia tayari kina mtandao wao visiwani wakiungana na CHADEMA na kupata uzoefu wa huku bara wanaweza kutoa upinzani visiwani na kuifanya CHADEMA kuweza kuingia visiwani na hivyo kuonea Tanzania nzima tofauti na hivi sasa ambapo kipo tu huku bara.
 
Duh!unatamani Chadema ikubalike mbaka nchi jirani,mimi nafikiri kukubalika kwa chadema huku Tanganyika inatosha sana!.Kwa kuwa Zanzibar ni nchi jirani tuliyoungana nayo,na naamini ipo siku muungano utakufa!!!
 
Mimi naona Chadema ifungue makanisa mengi ya pentekost zanzibar hiyo tu itasaidia
 
Mh. Tukutuku, DR Slaa alikuwa anagombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na siyo wa Tanganyika. Hatuwezi kuwa na raisi anayekubalika kwenye eneo moja tuu la Muungano
 
Mimi naona Chadema ifungue makanisa mengi ya pentekost zanzibar hiyo tu itasaidia

Kwani uliambiwa CHADEMA ni dhehebu la dini? Hoja ni kama ilivyo CUF kukubalika visiwani pekee na CHADEMA kukubalika huku bara pekee ni kifanyike ili vyama hivi vikubalike eneo lote la Muungano.
 
Nadhani inatakiwa iwepo katika vikao vya CHADEMA...
 
sio tu kwa chadema bali dunia nzima kila chama kinakuwa na ngome zake hata ukienda marekani utakuta chama fulani kina washabiki wengi katika majimbo fulani, cha msingi ingawa chama kinaweza kutokubalika sehemu fulani lakini sera za chama hicho zinabidi kujali pande zote yani kinapokubalika na kisipokubalika
 
muungano umeshakufa siku waliposaini muafaka na zanzibar kuwa nchi kamili. kilichobaki ni tanganyika kujitambua na kuunda serikali yake ambayo imeshabaki yatima baada ya wazanzibar kujitoa kimyakimya.sasa unataka chadema waende zanzibar kufanya nini?
na kwa taarifa yako cuf ya zanzibar na ya bara ni vitu tofauti,ya bara ni ya lipumba na ya zanzibar ni ya seif
mtake msitake hakuna tena kitu inayoitwa tanzania labda kwa kujidanganya tu.
 
Nadhani inatakiwa iwepo katika vikao vya CHADEMA...

Promise utaipeleka hiyo agenda. Ikibidi sehemu kubwa ya ruzuku watakayopata kuanzia Nov 2010 sehemu kubwa itumike kujitangaza maeneo ambayo hawajaweza kupenya
 
sio tu kwa chadema bali dunia nzima kila chama kinakuwa na ngome zake hata ukienda marekani utakuta chama fulani kina washabiki wengi katika majimbo fulani, cha msingi ingawa chama kinaweza kutokubalika sehemu fulani lakini sera za chama hicho zinabidi kujali pande zote yani kinapokubalika na kisipokubalika

Duniani kuna vyama vikubwa na vidogo. Mfano Republican na Democratics kwa USA; hali kadhalika UK. Vyama hivi vikubwa vina ushawishi nchi nzima. Sama kama CHADEMA sasa ni chama kikubwa lazima kienee nchi nzima.
 
muungano umeshakufa siku waliposaini muafaka na zanzibar kuwa nchi kamili. kilichobaki ni tanganyika kujitambua na kuunda serikali yake ambayo imeshabaki yatima baada ya wazanzibar kujitoa kimyakimya.sasa unataka chadema waende zanzibar kufanya nini?
na kwa taarifa yako cuf ya zanzibar na ya bara ni vitu tofauti,ya bara ni ya lipumba na ya zanzibar ni ya seif
mtake msitake hakuna tena kitu inayoitwa tanzania labda kwa kujidanganya tu.

Ni mtazamo wako lakini uchaguzi uliomalizika hivi karibuni ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si Katiba ya Tanganyika
 
Duniani kuna vyama vikubwa na vidogo. Mfano Republican na Democratics kwa USA; hali kadhalika UK. Vyama hivi vikubwa vina ushawishi nchi nzima. Sama kama CHADEMA sasa ni chama kikubwa lazima kienee nchi nzima.
natambua umuhimu wa chama kujitanua katika nchi njima lakini vitu kama hivyo vinahitaji fedha nyingi na mikakati ya kudumu, nadhani ni muda huu kabla ya uchaguzi wa 2015 chadema inatakiwa kujijenga nchi nzima kwani itakuwa na wabunge zaidi ya 40, na ruzuku ya kutosha kujifungulia matawi katika wilaya na kata katika taifa letu pia na ccm inatakiwa kujijenga pemba pia
 
Mh. Tukutuku, DR Slaa alikuwa anagombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na siyo wa Tanganyika. Hatuwezi kuwa na raisi anayekubalika kwenye eneo moja tuu la Muungano

Hata Kibaki hakubaliki kwa Waluo, Obama hakubaliki State nyingi tu na Museven hakubaliki kwa waacholi pia Kumbuka Kikwete hatumkubali hapa Arusha na hata kijijini kwetu kule Kilimanjaro, pia Kikwete hakubaliki Bukoba, maeneo mengi tu ya Mwanza,Shinyanga n.k
after all Zanzibar ni nchi inayofanyiwa ukoloni na Tanganyika very soon watajitenga. Hakuna haja ya Chadema kupoteza resources kwa nchi inayotegemea kujitema muda wowote kuanzia sasa.
 
Tanzania inaundwa na Visiwa vya Unguja na Pemba + Iliyokuwa Tanganyika. Hoja yangu ili chama kiweze kutwaa dola lazima kikubalike kazi nchi mbili zilizoungana na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vile vile kwa muundo wa Tanzania Serikali =Serikali kuu + serikali za mitaa; haina maana chama kuunda serikali kuu wakati haina ushawishi katika serikali za mitaa kwa utekelezaji wa ilani yake itakuwa ngumu sana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom