CHADEMA kushinda Chalinze

CHADEMA kushinda Chalinze

Msafara wa baba (akiwa na mkewe) na ule wa mtoto imekutana msata na kuzua msongamano wa magari. Mzee kahamishia kambi jimboni kumwokoa mwanae na aibu kubwa.. Shein ametia timu na kuhitimisha kampeni na kurudi Dar akipitia Bagamoyo...
 
Wamemaliza kampeni wakiwa na kambi mbili kubwa, moja Chalinze na ya pili Msata kila moja ikiwa na landcruzer zaidi ya 20 green guard walikuwa wakifanya kazi na TISS (wengine nawafahamu) na polisi.
Msata pia kulikuwa na kambi ya kutraini wapiganaji. Natarajia kuona magari yao yakikamatwa na silaha vituoni.
 
Viongozi wa serikali wilaya ya Bagamoyo na mkoa na taifa, TISS na polisi wameweka kambi chalinze. Nyumba za wageni zimejaa.
 
Mtu mzima unaongea umbea kweli siku hizi taifa limeishiwa watu wenye hoja za maana zamani umbea kama huu ulifanyika kwenye vikao vya akina dada na katika shule za msingi na sekondari lakini siku hizi mpaka watu wazima noma sana.
 
Kesho baada yankupiga kura msiondoke msaidiane kubembelezana naona mtakumbwa na msiba mkubwa sana ambao yawezekana hamjawahi kuuona kabisa lazima muwe na makopo ya kukingia machozi.
 
Kesho baada yankupiga kura msiondoke msaidiane kubembelezana naona mtakumbwa na msiba mkubwa sana ambao yawezekana hamjawahi kuuona kabisa lazima muwe na makopo ya kukingia machozi.

Mkuu Ridhiwani keshashinda tayari ni mtoto wa mkubwa na pesa wanazogawa na tshirts na kofia za bure na polisi kila upande kwa nini asishinde??? Wananchi wengi Njaa kali bora mkono uende kinywaji na trekta kila kijiji wameshaahidiwa wana Chalinze lazima wampe kura
 
hahahah..kushinda nini?
kama kushinda njaa ndio watashinda kwa kishindo tena siku nzima bila kula chochote

Wakuu kuna mtu kanitonya kua mathayo torongey uweza akapata ushindi kwa kishindo kwasababu kuna wamasai asilimia 70% wanamuunga mkono kesho ni kesho wacha tusubili
 
Back
Top Bottom