Chadema kusambaza wabunge nchi nzima kupinga muswada wa Katiba

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Saturday, 09 April 2011 09:10

Midraji Ibrahim, Dodoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema Jumamosi ijayo kitafanya maandamano nchi nzima kupinga muswada wa sheria wa mabadiliko ya Katiba unaoendelea kujadiliwa.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Bunge jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema wabunge wote wa chama hicho watatawanywa nchi nzima kushiriki maandamano hayo.

Mbowe alisema lengo kubwa la maandamano hayo ni kupinga muswada huo kupelekwa haraka haraka na pia kukipa chama hicho fursa ya kupata maoni ya wananchi wengi zaidi.

“Jumamosi wiki ijayo tunaandamana nchi nzima, wabunge wote wa Chadema watatawanyika nchi nzima, lengo ni kupata maoni ya wananchi wengi,” alisema Mbowe.

Alipinga hoja ya Serikali kwamba muswada huo usipopitishwa hivi sasa, hautakuwa na nafasi kwa sababu Bunge la Juni linahusika na Bajeti. Alisema miswada mingi imeshapitishwa kwa hati ya dharura.

“Tunataka maoni ya wananchi wengi yakusanywe ili yazingatiwe, muswada uletwe bungeni Juni. Suala la kwamba Bunge la Juni ni la bajeti ni sawa, lakini mwaka jana uliletwa muswada wa Gharama za Uchaguzi kwa hati ya dharura ukapita,” alisema.

Mbowe alisema Chadema kitaendelea kupinga muswada huo kusukumwa haraka haraka na kuwakosesha wananchi fursa ya kuchangia na kwamba, iwapo makosa yatafanyika na kupitishwa hivi sasa, yatakuwa ni majuto makubwa siku zijazo.

Kuhusu vijana wanaozomea kuhusishwa na Chadema, Mbowe alisema kuzomea ni kuonyesha hisia na kwamba muda wa ubabe kwa CCM umekwisha.“Waacheni wazomee, waacheni washangilie kama unawakataza kuzomea, wakataze na kushangilia. Mbona CCM wakishangiliwa hawakatai, sisi tunazomewa sana lakini tunaamini wanaonyesha hisia zao,” alisema na kuongeza:

“Kuna wanaozomea kama wabunge wa CCM humu ndani? (Bungeni), tunapoonyesha hisia zetu, hisia za wananchi kwa kutoka ndani ya ukumbi mnaona na kusikia jinsi wanavyotuzomea.”

Mbowe alisema kuzomewa kunawafundisha wanasiasa kusoma alama za nyakati na kwamba tuhuma za kila mara kwa chama hicho ni hofu ya watawala.Alisema suala la Katiba halitakiwi kubebwa na kuonekana kama ni mali ya kundi, chama au watu fulani, bali kushirikisha wananchi wote, huku akitahadharisha kuwa iwapo wataacha muswada huo kupita na upungufu huo, yatakuwa majuto makubwa siku zijazo.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alidai muswada wa sheria unaopingwa na wadau takriban asilimia 90, hauwezi kusimamiwa kupita kwa nguvu ya dola.Kuhusu chama hicho kutuhumiwa kuhusika na vurugu, Mbowe alisema hizo ni propaganda kwa chama chochote cha siasa, lakini Chadema itaendelea kuhamasisha wananchi kudai haki zao.

Spika atoa tamko
Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala inasikiliza maoni ya wadau kwa lengo la kuboresha muswada huo na kusisitiza kwamba huo si mdahalo.

“Hivyo busara lazima zitumike. Ibara ya 18 ya Katiba inatoa haki ya uhuru wa mawazo. Kwa kutambua haki ya kikatiba ndiyo maana Bunge limetoa fursa ya kushirikisha wananchi katika masuala muhimu yanayoihusu jamii,” alisema Makinda.

Hata hivyo, alisema hiyo haina budi kuzingatia haki na madaraka ya Bunge na kwamba kuheshimu mawazo ya mtu mwingine hata kama hukubaliani nayo lazima izingatiwe, tabia ya kuzomeana haikubaliki.

Kuhusu wadau waliojitokeza kushiriki na kufyatuliwa mabomu ya machozi na risasi za moto, Makinda alisema inasemekana wapo baadhi ya wanasiasa wanautumia muswada wa mabadiliko ya Katiba kama mtaji wa kisiasa, kuwapotosha wananchi hususan wanafunzi.

“Kama kweli kitendo hicho kinafanyika, hakileti picha nzuri na hakifai. Kinapaswa kukemewa na kuachwa mara moja kwa kuwa inahatarisha amani na usalama wa nchi yetu,” alisema Makinda.

Aliongeza katika mjadala wa Dodoma, dosari zilizojitokeza zimeonekana dhahiri kwa kuwa wadau wengi walioshiriki walitoa michango yao ya kina baada ya kupewa fursa ya kutosha, wakiwamo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Tofauti na mawazo yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya wanafunzi waliokuwa nje ya geti la Bunge kuwa Kamati ya Bunge au Bunge lilikuwa na njama za kuchagua watu maalumu kushiriki kwenye mkutano huo wa kamati.

Alisema wanafunzi hao walikata ushauri waliopewa mwanzo, huku wakiimba na kupiga kelele wakitaka kuingia wote ukumbini bila kukaguliwa, hali ambayo ilitishia usalama wa viongozi na wananchi maeneo ya Bunge.
 
well said mbowe............jana nimeshangaa sana watoto wamejaa karimjee na wote wamesinzia walahi ccm wapuuzi sana......
 
Saturday, 09 April 2011 09:10

Midraji Ibrahim, Dodoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema Jumamosi ijayo kitafanya maandamano nchi nzima kupinga muswada wa sheria wa mabadiliko ya Katiba unaoendelea kujadiliwa.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Bunge jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema wabunge wote wa chama hicho watatawanywa nchi nzima kushiriki maandamano hayo.

Mbowe alisema lengo kubwa la maandamano hayo ni kupinga muswada huo kupelekwa haraka haraka na pia kukipa chama hicho fursa ya kupata maoni ya wananchi wengi zaidi.

"Jumamosi wiki ijayo tunaandamana nchi nzima, wabunge wote wa Chadema watatawanyika nchi nzima, lengo ni kupata maoni ya wananchi wengi," alisema Mbowe.

Alipinga hoja ya Serikali kwamba muswada huo usipopitishwa hivi sasa, hautakuwa na nafasi kwa sababu Bunge la Juni linahusika na Bajeti. Alisema miswada mingi imeshapitishwa kwa hati ya dharura.

"Tunataka maoni ya wananchi wengi yakusanywe ili yazingatiwe, muswada uletwe bungeni Juni. Suala la kwamba Bunge la Juni ni la bajeti ni sawa, lakini mwaka jana uliletwa muswada wa Gharama za Uchaguzi kwa hati ya dharura ukapita," alisema.

Mbowe alisema Chadema kitaendelea kupinga muswada huo kusukumwa haraka haraka na kuwakosesha wananchi fursa ya kuchangia na kwamba, iwapo makosa yatafanyika na kupitishwa hivi sasa, yatakuwa ni majuto makubwa siku zijazo.

Kuhusu vijana wanaozomea kuhusishwa na Chadema, Mbowe alisema kuzomea ni kuonyesha hisia na kwamba muda wa ubabe kwa CCM umekwisha."Waacheni wazomee, waacheni washangilie kama unawakataza kuzomea, wakataze na kushangilia. Mbona CCM wakishangiliwa hawakatai, sisi tunazomewa sana lakini tunaamini wanaonyesha hisia zao," alisema na kuongeza:

"Kuna wanaozomea kama wabunge wa CCM humu ndani? (Bungeni), tunapoonyesha hisia zetu, hisia za wananchi kwa kutoka ndani ya ukumbi mnaona na kusikia jinsi wanavyotuzomea."

Mbowe alisema kuzomewa kunawafundisha wanasiasa kusoma alama za nyakati na kwamba tuhuma za kila mara kwa chama hicho ni hofu ya watawala.Alisema suala la Katiba halitakiwi kubebwa na kuonekana kama ni mali ya kundi, chama au watu fulani, bali kushirikisha wananchi wote, huku akitahadharisha kuwa iwapo wataacha muswada huo kupita na upungufu huo, yatakuwa majuto makubwa siku zijazo.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alidai muswada wa sheria unaopingwa na wadau takriban asilimia 90, hauwezi kusimamiwa kupita kwa nguvu ya dola.Kuhusu chama hicho kutuhumiwa kuhusika na vurugu, Mbowe alisema hizo ni propaganda kwa chama chochote cha siasa, lakini Chadema itaendelea kuhamasisha wananchi kudai haki zao.

Spika atoa tamko
Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala inasikiliza maoni ya wadau kwa lengo la kuboresha muswada huo na kusisitiza kwamba huo si mdahalo.

"Hivyo busara lazima zitumike. Ibara ya 18 ya Katiba inatoa haki ya uhuru wa mawazo. Kwa kutambua haki ya kikatiba ndiyo maana Bunge limetoa fursa ya kushirikisha wananchi katika masuala muhimu yanayoihusu jamii," alisema Makinda.

Hata hivyo, alisema hiyo haina budi kuzingatia haki na madaraka ya Bunge na kwamba kuheshimu mawazo ya mtu mwingine hata kama hukubaliani nayo lazima izingatiwe, tabia ya kuzomeana haikubaliki.

Kuhusu wadau waliojitokeza kushiriki na kufyatuliwa mabomu ya machozi na risasi za moto, Makinda alisema inasemekana wapo baadhi ya wanasiasa wanautumia muswada wa mabadiliko ya Katiba kama mtaji wa kisiasa, kuwapotosha wananchi hususan wanafunzi.

"Kama kweli kitendo hicho kinafanyika, hakileti picha nzuri na hakifai. Kinapaswa kukemewa na kuachwa mara moja kwa kuwa inahatarisha amani na usalama wa nchi yetu," alisema Makinda.

Aliongeza katika mjadala wa Dodoma, dosari zilizojitokeza zimeonekana dhahiri kwa kuwa wadau wengi walioshiriki walitoa michango yao ya kina baada ya kupewa fursa ya kutosha, wakiwamo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Tofauti na mawazo yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya wanafunzi waliokuwa nje ya geti la Bunge kuwa Kamati ya Bunge au Bunge lilikuwa na njama za kuchagua watu maalumu kushiriki kwenye mkutano huo wa kamati.

Alisema wanafunzi hao walikata ushauri waliopewa mwanzo, huku wakiimba na kupiga kelele wakitaka kuingia wote ukumbini bila kukaguliwa, hali ambayo ilitishia usalama wa viongozi na wananchi maeneo ya Bunge.

weka source kwanza kabla sijatumia muda wangu kusoma na kuchangia
 
Saturday, 09 April 2011 09:10

Midraji Ibrahim, Dodoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema Jumamosi ijayo kitafanya maandamano nchi nzima kupinga muswada wa sheria wa mabadiliko ya Katiba unaoendelea kujadiliwa.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Bunge jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema wabunge wote wa chama hicho watatawanywa nchi nzima kushiriki maandamano hayo.

Mbowe alisema lengo kubwa la maandamano hayo ni kupinga muswada huo kupelekwa haraka haraka na pia kukipa chama hicho fursa ya kupata maoni ya wananchi wengi zaidi.

"Jumamosi wiki ijayo tunaandamana nchi nzima, wabunge wote wa Chadema watatawanyika nchi nzima, lengo ni kupata maoni ya wananchi wengi," alisema Mbowe.

Alipinga hoja ya Serikali kwamba muswada huo usipopitishwa hivi sasa, hautakuwa na nafasi kwa sababu Bunge la Juni linahusika na Bajeti. Alisema miswada mingi imeshapitishwa kwa hati ya dharura.

"Tunataka maoni ya wananchi wengi yakusanywe ili yazingatiwe, muswada uletwe bungeni Juni. Suala la kwamba Bunge la Juni ni la bajeti ni sawa, lakini mwaka jana uliletwa muswada wa Gharama za Uchaguzi kwa hati ya dharura ukapita," alisema.

Mbowe alisema Chadema kitaendelea kupinga muswada huo kusukumwa haraka haraka na kuwakosesha wananchi fursa ya kuchangia na kwamba, iwapo makosa yatafanyika na kupitishwa hivi sasa, yatakuwa ni majuto makubwa siku zijazo.

Kuhusu vijana wanaozomea kuhusishwa na Chadema, Mbowe alisema kuzomea ni kuonyesha hisia na kwamba muda wa ubabe kwa CCM umekwisha."Waacheni wazomee, waacheni washangilie kama unawakataza kuzomea, wakataze na kushangilia. Mbona CCM wakishangiliwa hawakatai, sisi tunazomewa sana lakini tunaamini wanaonyesha hisia zao," alisema na kuongeza:

"Kuna wanaozomea kama wabunge wa CCM humu ndani? (Bungeni), tunapoonyesha hisia zetu, hisia za wananchi kwa kutoka ndani ya ukumbi mnaona na kusikia jinsi wanavyotuzomea."

Mbowe alisema kuzomewa kunawafundisha wanasiasa kusoma alama za nyakati na kwamba tuhuma za kila mara kwa chama hicho ni hofu ya watawala.Alisema suala la Katiba halitakiwi kubebwa na kuonekana kama ni mali ya kundi, chama au watu fulani, bali kushirikisha wananchi wote, huku akitahadharisha kuwa iwapo wataacha muswada huo kupita na upungufu huo, yatakuwa majuto makubwa siku zijazo.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alidai muswada wa sheria unaopingwa na wadau takriban asilimia 90, hauwezi kusimamiwa kupita kwa nguvu ya dola.Kuhusu chama hicho kutuhumiwa kuhusika na vurugu, Mbowe alisema hizo ni propaganda kwa chama chochote cha siasa, lakini Chadema itaendelea kuhamasisha wananchi kudai haki zao.
Tunaisubiri kwa hamu siku hiyo mkuu.
 
Hapo umeongea Mbowe, maandamano nchi nzima na kwa wakati mmoja kupinga upuuzi wa CCM.

Mwaka huu hamtoki wezi wakubwa nyie!
 
Mara nyingi Chadema wamekuwa na impact wanapokwenda pamoja kama timu, lakini hii ya kusambaa nchi nzima sioni kama itafanikiwa.

Kwa nini wasiitishe maadamano makubwa kwa mfano katika miji ya Dar es Salaam au Dodoma? kisha watumie media kusambaza propaganda kushadidia uzito wa hoja yao?
 
Mpaka kieleweke,hawawezi kutulazizimisha kufuata wanavyotaka wao,eti mamlaka ya raisi yasihojiwe,hapo ndipo penye matatizo hasa
 
Wengine tunapotoa onyo wao CCM hujikanyagia tu miba kwa kuchukulia kila jambo ni mzaha tu!!!!!!!!!!!
 
Ngoja uone muziki wake mzee!!!!!!!!!!!

Mara nyingi Chadema wamekuwa na impact wanapokwenda pamoja kama timu, lakini hii ya kusambaa nchi nzima sioni kama itafanikiwa.

Kwa nini wasiitishe maadamano makubwa kwa mfano katika miji ya Dar es Salaam au Dodoma? kisha watumie media kusambaza propaganda kushadidia uzito wa hoja yao?
 
Saturday, 09 April 2011 09:10

Midraji Ibrahim, Dodoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema Jumamosi ijayo kitafanya maandamano nchi nzima kupinga muswada wa sheria wa mabadiliko ya Katiba unaoendelea kujadiliwa.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Bunge jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema wabunge wote wa chama hicho watatawanywa nchi nzima kushiriki maandamano hayo.

Mbowe alisema lengo kubwa la maandamano hayo ni kupinga muswada huo kupelekwa haraka haraka na pia kukipa chama hicho fursa ya kupata maoni ya wananchi wengi zaidi.

“Jumamosi wiki ijayo tunaandamana nchi nzima, wabunge wote wa Chadema watatawanyika nchi nzima, lengo ni kupata maoni ya wananchi wengi,” alisema Mbowe.

Alipinga hoja ya Serikali kwamba muswada huo usipopitishwa hivi sasa, hautakuwa na nafasi kwa sababu Bunge la Juni linahusika na Bajeti. Alisema miswada mingi imeshapitishwa kwa hati ya dharura.

“Tunataka maoni ya wananchi wengi yakusanywe ili yazingatiwe, muswada uletwe bungeni Juni. Suala la kwamba Bunge la Juni ni la bajeti ni sawa, lakini mwaka jana uliletwa muswada wa Gharama za Uchaguzi kwa hati ya dharura ukapita,” alisema.

Mbowe alisema Chadema kitaendelea kupinga muswada huo kusukumwa haraka haraka na kuwakosesha wananchi fursa ya kuchangia na kwamba, iwapo makosa yatafanyika na kupitishwa hivi sasa, yatakuwa ni majuto makubwa siku zijazo.

Kuhusu vijana wanaozomea kuhusishwa na Chadema, Mbowe alisema kuzomea ni kuonyesha hisia na kwamba muda wa ubabe kwa CCM umekwisha.“Waacheni wazomee, waacheni washangilie kama unawakataza kuzomea, wakataze na kushangilia. Mbona CCM wakishangiliwa hawakatai, sisi tunazomewa sana lakini tunaamini wanaonyesha hisia zao,” alisema na kuongeza:

“Kuna wanaozomea kama wabunge wa CCM humu ndani? (Bungeni), tunapoonyesha hisia zetu, hisia za wananchi kwa kutoka ndani ya ukumbi mnaona na kusikia jinsi wanavyotuzomea.”

Mbowe alisema kuzomewa kunawafundisha wanasiasa kusoma alama za nyakati na kwamba tuhuma za kila mara kwa chama hicho ni hofu ya watawala.Alisema suala la Katiba halitakiwi kubebwa na kuonekana kama ni mali ya kundi, chama au watu fulani, bali kushirikisha wananchi wote, huku akitahadharisha kuwa iwapo wataacha muswada huo kupita na upungufu huo, yatakuwa majuto makubwa siku zijazo.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alidai muswada wa sheria unaopingwa na wadau takriban asilimia 90, hauwezi kusimamiwa kupita kwa nguvu ya dola.Kuhusu chama hicho kutuhumiwa kuhusika na vurugu, Mbowe alisema hizo ni propaganda kwa chama chochote cha siasa, lakini Chadema itaendelea kuhamasisha wananchi kudai haki zao.

Spika atoa tamko
Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala inasikiliza maoni ya wadau kwa lengo la kuboresha muswada huo na kusisitiza kwamba huo si mdahalo.

“Hivyo busara lazima zitumike. Ibara ya 18 ya Katiba inatoa haki ya uhuru wa mawazo. Kwa kutambua haki ya kikatiba ndiyo maana Bunge limetoa fursa ya kushirikisha wananchi katika masuala muhimu yanayoihusu jamii,” alisema Makinda.

Hata hivyo, alisema hiyo haina budi kuzingatia haki na madaraka ya Bunge na kwamba kuheshimu mawazo ya mtu mwingine hata kama hukubaliani nayo lazima izingatiwe, tabia ya kuzomeana haikubaliki.

Kuhusu wadau waliojitokeza kushiriki na kufyatuliwa mabomu ya machozi na risasi za moto, Makinda alisema inasemekana wapo baadhi ya wanasiasa wanautumia muswada wa mabadiliko ya Katiba kama mtaji wa kisiasa, kuwapotosha wananchi hususan wanafunzi.

“Kama kweli kitendo hicho kinafanyika, hakileti picha nzuri na hakifai. Kinapaswa kukemewa na kuachwa mara moja kwa kuwa inahatarisha amani na usalama wa nchi yetu,” alisema Makinda.

Aliongeza katika mjadala wa Dodoma, dosari zilizojitokeza zimeonekana dhahiri kwa kuwa wadau wengi walioshiriki walitoa michango yao ya kina baada ya kupewa fursa ya kutosha, wakiwamo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Tofauti na mawazo yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya wanafunzi waliokuwa nje ya geti la Bunge kuwa Kamati ya Bunge au Bunge lilikuwa na njama za kuchagua watu maalumu kushiriki kwenye mkutano huo wa kamati.

Alisema wanafunzi hao walikata ushauri waliopewa mwanzo, huku wakiimba na kupiga kelele wakitaka kuingia wote ukumbini bila kukaguliwa, hali ambayo ilitishia usalama wa viongozi na wananchi maeneo ya Bunge.

Ivi hiyo katiba inawahusu dsm dodoma zanzibar wengine hatuhusiki? Au mikowa mingine sii tz nasisi tujiandarie katiba yetu na lais wetu tumetengwa inakuweje huo mswada wasihusishe wa tz wote nikwanini? Uandikwe kwa kimombo rugha ya taifa nikiswahiri tz kirakitu niuchakachuwajii sijuwi kamatutafika mara wanasiasa hawaruhusiwi rakini jk waziri wa katiba wz wa sheriya wawo rukusa kushiriki jee? Wao siwanasiasa? Bira migomo maandamano hakunarorote aundo yareyare yakutikisa kiberiti
 
Back
Top Bottom