Juliana
Hujambo binti,
Nimesoma andishi lako, hakika lina sura mbili kuu
1. Ni andishi la kufikirika kama ulivyoanza mwanzo kwamba umekusudia kuwafikirisha tu makutano, hakika umefikirisha tu na
huna uhakika na usemacho.
2. Umejitoa ufahamu na umang'amuzi wa nera katika kudurusu mambo mtambuka ya husuyo siasa na utawala, kwabahati mbaya kuyapuuza maonyo yangu lakini sitanyamaza kukuonya tena,
Kama akina Chahali na Mwanakijiji unawaamini kuwa ndio kipimo cha uthabiti wa Yericko bora Yericko awe na iq ndogo kwamaana
kwa msaada na uthubutu wake taifa litapona,
Siamini kama wamekutuma uwasemee, lakini kama ndivyo basi nami naliwajua wangali hawajakutuma wewe,
Hao watu nikujuzi tu kuwa hawana msaada kwa taifa hili na ni wakimbizi ambao hata kura hawatapiga.
Chadema ni taasisi peke yakisiasa iliyoyashinda majaribu na hila chini ya Mbowe, hujiulizi kwanini?
Mbowe hana bei, bei yake ni ccm kutoka ikulu tu, Mbowe ni mwanasiasa aliyezaliwa kutoka uanaharakati. Msimamo na
Financial status ya Mbowe ndio mwiba mkali kwa ccm,
hilo Shonza unalitambua,
Jiulize kwanini wewe na akina Zitto mlinunulika na ccm lakini Mbowe hajanunulika na leo anatuongoza kwenda ikulu?
Nikutakie siku njema
my ex honey, mwambie jamaa kuwa "aliyechonga mzinga hula asali mpaka mzinga uanguke"!
Mimi sijambo..nijuze juu ya hali yako..?
Katika andiko langu lililobeba HOJA ya msingi nimesema bayana kuwa IQ ya Yericko Nyerere ni 0.0001, na hauwezi kufananisha uwezo wake na mtu kama Mwanakijiji ama Chahali..sikuwa nimekosea, ulichoandika hapa kimeendelea kuthibitisha maneno hayo na hata kuonyesha ziada ya UMBUMBUMBU wako.
1. Umesema sina uhakika na nilichokisema.,naomba nikuhakikishie kuwa ninauhakika wa asilimia zaidi ya 100 juu ya kile nilichokisema..nitajinukuu;
YERICKO NYERERE, A man with 0.001 IQ, Anaishi katika uongo na uzushi, mpaka kila mmoja amemmpuuza, Mwanakijiji, Chahali na WATABE wengine wa maandishi yenye adili, wameikacha CHADEMA, bado CDM haijiulizi, inajivunia kuwa na YERICKO.
- Nikutakie siku njema
my ex honey, UONGO na UZUSHI ndio maisha yako.
2. Hoja yako nyingine inasema kuwa nimekupima kwa mtazamo wa wanaCCM..
Haiingii akilini mwanaccm unayapima mapungufu ya Yericko kwakutumia kipimo cha mwanaccm,
Niambie ni wapi na lini Mwanakijiji ama Chahali walijiunga na CCM na kuwa wanaccm..?
3.
Chadema ni taasisi peke yakisiasa iliyoyashinda majaribu na hila chini ya Mbowe
Kama unadhani kuwa CHADEMA ya sasa imeshinda majaribu basi ni katika KUTHIBITISHA tu ukweli na uwezo wa IQ yako..,CHADEMA ambayo inaenda kwenye uchaguzi ikiwa na Mgombea asiyejua misingi, dhamira, vision na hata mission ya Chama, Chadema inayoenda kwenye uchaguzi ikiwa haina Katibu Mkuu na kawaida kwenye uchaguzi wowote katibu mkuu ndio mratibu wa shughuli hiyo..CHADEMA inaenda kwenye uchaguzi ikiwa defensive, inaanza kujitetea na kumpiga dodoki mgombea wake kisha ndio iombe kura..,CHADEMA ambayo imepoteza mandate na legitimacy ya KUKEMEA RUSHWA, na badala yake imekumbatia Rushwa na wala rushwa. Uchaguzi ni mwepesi sana kwa CCM kuliko chaguzi zake zote, CCM inasema na kuionyooshea CHADEMA na wapinzani vidole bado kwa UJINGA unasema CHADEMA imeshinda majaribu...wakati kila mmoja anajua kuwa LOWASSA kainunua CHADEMA kwa Bilioni 20...ni aibu.
4.
Financial status ya Mbowe ndio mwiba mkali kwa ccm,
Ndugu yangu kama haujui vitu ni vyema ukanyamaza kimya..financial status ya Mbowe ndio mwiba kwa CCM??? Kumbe kwenye miaka yote CCM wanaogopa financial status ya MBOWE na sio HOJA za wanachadema bungeni na katika majukwaa ya siasa..? Huu ni ujinga uliopevuka, nathubutu kuuita UMBUMBUMBU..Yericko wewe ni MBUMBUMBU.
Hivi kwa akili yako NDESAMBURO na MBOWE nani ana financial status nzuri..? kwanini asiogopwe ndesamburo.? Labda utueleze hapa jamvini, MBOWE anamiliki kiasi gani katika benki,na katika jumla ya vitu vyake (nyumba, mashamba n.k) ili tukubaliane na Hoja yako kuwa Financial status ya MBOWE ni Mwiba kwa CCM..
Bali ninachojua mimi, Mbowe ni mpiga dili, aliwahi kuiuzia CHADEMA magari mabovu kwa bei ya juu, aliwahi kudai fedha iliyotumika kwenye uchaguzi 2010 akidai ilikuwa ni ya kwake hali ya kuwa alipewa na wafadhili kwa ajili ya Chama, Mbowe ameiuza CHADEMA kwa Lowassa kwa bilioni 20 na taarifa nyingine ambayo hauijui ni kuwa KITEGA UCHUMI kikubwa cha mbowe, Club ya BILLICANS imefungwa baada ya watu kuweka mgomo baridi, watu wanakusanyika Maisha BAsement, HIGH SPIRIT. RHAPSOD na Club zingine za wajanga wakila ujana..Huyo mwenyekiti wenu amechacha..
Kimsingi hauna hoja yeyote ya msingi ambayo umekuja nayo zaidi ya kuja kutimiza wajibu wako uliotumwa wa kuitetea CHADEMA na MBOWE mitandaoni..shame on U..