Chadema kumburuza Waitara kamati ya maadili

Chadema kumburuza Waitara kamati ya maadili

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
waitara+pic.jpg

Mwita Waitara
Kwa ufupi
Ni kutokana na madai ya kuhamasisha vurugu kupitia mitandao ya kijamii.

By Hussein Issa, Mwananchi. hissa@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia Maendeleo (Chadema) kimempeleka kwenye kamati ya maadili mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara.
Akizungumza leo Jumatano, Agosti 29, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Dingo Kigaila amesema sababu ya kumpeleka kwenye kamati hiyo ni kutokana na madai ya kuhamasisha vurugu kwa kupitia mtandao wa kijamii.
Amesema kwa kutumia simu yake ya kiganjani Agosti 26 mwaka huu aliandika kwamba watu wa kabila lake yaani Wakurya hususan ukoo wa Wairegi wanoe mapanga yao na kumwaga damu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi jimbo la Ukonga.
Amesema Waitara alitumia lugha ya Kiswahili na Kikurya kuandika ujumbe huo.
Chadema wameitaka kamati ya maadili, kumuita na kumuhoji Mwita Waitara.
 
Farasi yoyote anayeleta mboyoyo apelekwe kizimbani.This guy ,Waitara is "kurrupt" to the earth!He should have gone to hell for quite a long!You,kuryas over there!What are you waiting for?Ghesha that sonovakuku!
 
Nitarudi ngoja wasifiaji waje kwanza kumtetea.
 
Back
Top Bottom