Ikumbukwe ipo tofauti kubwa kati ya Chadema na mashabiki mitandaoni.
Ni muhimu kukawa na focus ya hoja ipi inamhusu nani katika wawili hao.
Kumekuwa na maangalizo mengi ambapo kwa hakika Chadema kama chama kinapaswa kufikiria kuyafanyia kazi:
1.Lwaitama, Heche, Kigaila na wa namna hiyo katika kipindi hiki (ambacho Mbowe yuko gerezani na Lissu yuko nje ya nchi) ni muhimu wasiwe mbali na hatamu za uongozi wa chama.
2. Agenda za chama ni muhimu zikaeleweka, na viongozi wakachukua jukumu la kuhakikisha wanachama na wafuasi wanazielewa.
3. Ni muhimu ikaeleweka kuwa kama chama cha ukombozi kupigania mageuzi makubwa yenye kuhitaji katiba mpya hakuwezi kutenganishwa na uanaharakati.
4. Kama chama cha harakati ni muhimu wasiokuwa tayari kuwa sehemu ya kuchukua hatua wakapisha, wakapiga kimya au hata kufikiria kujiunga ACT, TLP, nk huko kunako bata.
Msingi mzima wa kuyafikia malengo ukiwa uelewa wa wazi kuwa:
a) Minyukano ndani ya CCM haitusaidii kwenye madai yetu ya katiba mpya.
b) Mwendazake hayupo tena, makando kando yake tuhangaike nayo kwenye "haki na maridhiano" baada ya katiba mpya.
c) Agenda zetu ni za kudumu si marafiki.
Ni muhimu kutambua, Lissu na walioko uhamishoni kuja kwao kunategemea sana hali ya mapambano ardhini ilivyo.