Chadema kuiburuza serikali mahakamani

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Akisoma maadhimio kumi na sita mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika amesema chama chake kipo njiani kuishitaki serikali kutokana na makada wake kumi na tano kuuawa na serikali kukaa kimya.

Mnyika aliweka wazi toka chaguzi mbali mbali ndogo zianze chama chake kimekuwa kikipoteza makada wake katika mazingira ya kutatanisha na serikali kukaa kimya kama hanma kitu kilichotokea.

Source ITV.
 
Akisoma maadhimio kumi na sita mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika amesema chama chake kipo njiani kuishataki serikali kutokana na makada wake kumi na tano kuuawa na serikali kukaa kimya.

Source ITV.

hiyo ndiyo dawa.

walikubali mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ili watuuwe?

au walifikiri masihara?

wamelikoroga lazima walinywe.

watake wasitake chama cha mafisadi lazima king'oke.
 
Ninaunga mkono hoja 10000%. Haiwezekani serikali iseme inathamini uhai wa raia wake wakati huo huo ikae kimya wakati mauwaji ya kinyama yanafanywa. Watu 15 ni wengi sana kwa nchi inayodai inathamini uhai wa binadamu.
 
Uchungu huo mnaupata leo?

kwani mara ya kwanza watu kuuwawa na polisi hapa bongo?

Mkapa hakuua wapemba january 21
 
Ni kweli bana watu wanauawa kwa kukatwa na shoka katika mazingira ya kutatanisha lakini serikali ipo kimya tu!!!!

Kila kitu nchi hii mpaka mashinikozo.

Hebu fikiria Igunga tumepoteza kada mmoja Mbwana, Arumeru Mwenyekiti.

Ilemela wabunge wetu wamejeruhiwa hivi hivi halafu inaonekana wazi kabisa Jeshi la Polisi limezembea. Mpaka leo haijulikani kama kuzembea huko ni kwa bahati mbaya au makusudi!!!!
 
Uchungu huo mnaupata leo?

kwani mara ya kwanza watu kuuwawa na polisi hapa bongo?

Mkapa hakuua wapemba january 21

Kwa hiyo mmezoea kuua halafu watu wasihoji? Safari hii imekula kwenu tutakutana mahakani.

Kwanza pelekeni fedha za wanachuo huko maana wamegoma hawajaongiziwa fedha mpaka saizi na nasikia hazina Mkulo kakausha yote.
 
Naona TBC, wameiruka hiyo habari au hawakuwa nayo kabisa!!

Buruza magamba cortini tu!!

TBC1 kwishney yaani wameripoti tukio la kuvuliwa ubunge wa Sumbawanga picha kama imechukuliwa na kasimu ka mchina kutokana na kutokuwa na quality!!

Matukio kama hayo hawawezi kuyarusha.
 
siasa za visasi mpaka lini jama?, serikali kuua raia wake ili itawale hakuna utofauti na serikali ya kidikteta kama ya id amin dada, adolph itler, musolin,etc, shame on them!
 
Naona TBC, wameiruka hiyo habari au hawakuwa nayo kabisa!!

Buruza magamba cortini tu!!

Nimeipenda sana hii,haiwezekani roho za watanzania zika uwawa halafu marpc na maocd wasiwajibishwe,wajifunze kwa mzee ruksa.Mwanadamu si kuku au mbwa,ni lazima alindwe hata kama anakasoro ya aina yoyote.TUNAONA UMUHIMU WA RANGI NYEKUNDU KWENYE BENDERA KWA KUWAKUMBUKA MASHUJAA WETU.
 
siasa za visasi mpaka lini jama?, serikali kuua raia wake ili itawale hakuna utofauti na serikali ya kidikteta kama ya id amin dada, adolph itler, musolin,etc, shame on them!

Mbona enzi za chama kimoja na enzi za CCM kupeta haya hayakuwepo?

Ni kipindi hiki tu ambapo upinzani umeshika hatamu, kunani?
 
Buruza hiyo serikali mahakaman maana hali ya viongozi wetu ni tete,je,tukishinda kesi serikali itawajibikaje? Nna wasiwasi na punishment itakavyotolewa na kutekelezwa.
 
Mahakama ipi ya ICC au zetu za ndani? Kama ICC naunga mkono hoja ila kama ni za ndani sijui kama haki itapatikana.
 
Ni kweli bana watu wanauawa kwa kukatwa na shoka katika mazingira ya kutatanisha lakini serikali ipo kimya tu!!!!

Kila kitu nchi hii mpaka mashinikozo.

Hebu fikiria Igunga tumepoteza kada mmoja Mbwana, Arumeru Mwenyekiti.

Ilemela wabunge wetu wamejeruhiwa hivi hivi halafu inaonekana wazi kabisa Jeshi la Polisi limezembea. Mpaka leo haijulikani kama kuzembea huko ni kwa bahati mbaya au makusudi!!!!

Losambo, nashindwa kuelewa inakuwaje serikali kupitia Jeshi la Polisi wameshindwa hata kumkamata mtu mmoja kutokana na haya matukio ya kutisha? Kama wameshindwa tafsiri yake ni kwamba Tanzania sio salama tena kwa sababu jeshi la polisi halina uwezo wa kupambana na mauwaji! Je, ni kweli polisi hawana uwezo huo? Uvamivi mpaka kwa wabunge?
 
kwenye mazishi ya mkiti wa ccm huko meru leo Andengenye ameahidi mil 10 atakae saidia kukamatwa kwa muaji lakini lema alimpinga hapo hapo na kumwambia wauji walimpigia simu marehemu kwanini wasifanye uchunguzi kwenye mitandano ya simu
 
hiyo ndiyo dawa.

walikubali mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ili watuuwe?

au walifikiri masihara?

wamelikoroga lazima walinywe.

watake wasitake chama cha mafisadi lazima king'oke.

Itakuwa wapi mahakama ya Afrika au kwa Ocampo?
 
Back
Top Bottom