CHADEMA kuanza mchakato wa Katiba Mpya ndani ya siku 90 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kuanza mchakato wa Katiba Mpya ndani ya siku 90

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by MwanaFalsafa1, Aug 9, 2010.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam jana walijitokeza kumlaki mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilibroad Slaa, ambaye wakati akihutubia wananchi pamoja na mambo mengine, ameahidi kuanza mchakato wa utengenezaji wa katiba mpya ndani ya miezi minne kama atapewa dhamana ya kuongoza nchi.
  Dk. Slaa ambaye hadi jana asubuhi alikuwa ameshadhaminiwa na Watanzania 1,397,757 kutoka mikoa 20 Tanzania Bara na Visiwani, alikuwa akitokea Zanzibar alikokwenda kutafuta wadhamini, akiwa ameambatana na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ambapo aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere majira ya saa 6:50 mchana na baadaye kuhutubia umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika viwanja vya Jangwani.
  Wakati akitoa hutuba, Dk. Slaa alisema kero nyingi zinazoikabili nchi kwa sasa zinatokana na Katiba ya nchi kuwa na kasoro nyingi na kwamba iwapo itaandikwa upya kwa kuzingatia matakwa ya wananchi wengi, itasaidia kutatua kero hizo.
  "Siku hizi kila mahali ni foleni, ukienda polisi ni foleni, mahakamani, benki, barabarani kote ni foleni huku chai ya 'wakubwa' kwa mwaka inagharimu zaidi ya bilioni 30, wabunge wanapandishiwa mishahara kila siku na kulipwa posho kubwa wakati mwananchi wa kawaida akiteseka kwenye lindi la umaskini, hizi ni kero zinazohitaji ufumbuzi wa haraka," alisema Dk. Slaa na kushangiliwa.
  Dk. Salaa, ambaye alihutubia kwa takribani dakika 40 kuanzia saa 12:03 jioni, alisema Tanzania inahitaji viongozi watakaoweza kupanga matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo ili zinufaishe umma badala ya kuwanufaisha wachache huku wengi wakiumia.
  Kwa wakati wote ambao Dk. Slaa alikuwa akihutubia wananchi walikuwa wakimshangilia kwa kumwita 'Rais, Rais' jambo lililokuwa likimlazimu kukatisha hotuba yake kila mara.
  Awali, Mbowe alisema Chadema kinamuunga mkono Maalim Seif Hamad Sharif ambaye anawania Urais kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) visiwani Zanzibar.
  Alisema kuwa chama hicho hakitasimamisha mgombea urais kwa upande wa Zanzibar na kwamba wafuasi wake watampa kura za urais Maalim Seif. Hata hivyo, alisema Chadema kitasimamisha wagombea wa ubunge na uwakilishi visiwani humo ili kuweka nguvu ya upinzani ndani ya Baraza la Wawakilishi.
  Hata hivyo, alisema Chadema haiungi mkono uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar kwa maelezo kwamba uundwaji wake hautamaliza siasa za chuki visiwani humo.
  Kwa upande wa Bara, alisema chama hicho kimeshindwa kuungana na vyama vingine kwa kuwa baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikifanya mzaha kwa kushabikia CCM.
  Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, Chadema kitapambana ipasavyo ili kuhakikisha kinapata ushindi na kueleza kwamba wamechoshwa na wizi wa kura aliosema umekuwa ukifanywa na Chama Cha Mapinduzi.
  "Chadema tumeamua kumuunga mkono Maalim Seif kule Zanzibar lakini tutasimamisha wagombea ubunge na uwakilishi wa Baraza. Kwa upande wa Bara, nadhani wote mnafahamu kwamba tunavyama 17 vya siasa, vya kweli na vya mzaha. Hatuwezi kuungana na vyama vinavyocheza ngoma ya CCM," alisema na kuongeza "Haki ya Mungu, ama zao ama zetu...lugha ya kusema tumeibiwa kura mwaka huu tutaiacha. Chadema tunapenda amani lakini mwaka huu ikibidi na sisi tutaiba kura, tumechoka."
  Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Said Arf, alisema afya ya Dk. Slaa ni imara na kwamba anaweza kufanyakazi bila tatizo lolote hivyo kuwaomba wananchi wamchague kuwa rais wakati wa uchaguzi. Alionya kwamba chama hicho hakiwezi kugawanywa na propaganda ya udini ambayo imeanza kunadiwa na wapinzani wao wa kisiasa wanaodai kwamba Dk. Slaa ni chaguo la Kanisa Katoliki.
  Wakili wa maarufu nchini, Mabere Marando, ambaye ni miongoni mwa mawakili wanaowatetea watuhumiwa wa wizi wa EPA, alisema washtakiwa waliofikishwa mahakamani ni matawi na kwamba CCM haitaweza kuwakamata watuhumiwa wakubwa.
  Alisema kuwa watuhumiwa waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa EPA ni watu wadogo, lakini vigogo waliohusika hawajachukuliwa hatua yoyote na kwamba ushahidi anao.
  Hata hivyo, akisoma dua ya kufungua mkutano huo, Sheikh Said Mwaipopo, alisababisha wananchi kushangilia katikati ya swala alipomwomba Mungu awadhalilishe wezi wote wa rasilimali za nchi.
  Aidha, msafara wa Dk. Slaa ambao uliwasili uwanja wa ndege wa zamani majira ya saa 6:50 mchana, ulikuwa ukisimama kila wakati njiani wakati ukielekea Jangwani, kutokana na magari ya wananchi kuingilia jambo lililoibua mgogoro baina ya vijana wa usalama wa Chadema na askari wa usalama barabarani, katika mataa ya Tazara.

  Source: Nipashe Jumapili
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kwa hili la katiba mpya nakubaliana na Mh. Slaa. Natumai kampeni zikianza rasmi ata weka bayana na mabadiliko gani ndani ya katiba ana kusudia kuleta na ita kuaje nafuu kuliko hii tuliyo nayo kwa sasa.
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Miezi minne atoe Katiba Mpya? Au ndio usanii wa kisiasa?

  Amandla....
   
 4. n

  njori Member

  #4
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwakweli ni usanii wa siasa!!!
  ndio yale yale ya "nitawajaza mapesa nikipata urais" hivi kuna anayeridhika na jinsi alivyo hata apewe matrilioni ya fedha atasema hajatosheka.
  labda katiba ya chama chake itawezekana akimua kuwafungia wanachama wake Karatu
   
 5. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Huenda ni namna ya kuripoti, inawezekana amemaanisha mchakato kuanza ndani ya miezi minne, of course kubadilisha katiba ni process ndefu, na inaweza kuchukua muda zaidi, lakini walau kuwepo na mtu mwenye dhamira ya dhati ya kufanya hivyo inatupelekea kuendelea kuamini kuwa ana dhamira ya dhati ya kuwakomboa watanzania. Kama kuna mtu ambaye anaamini kuwa katiba yetu iko sahihi kwa mazingira haya, huenda ana mtazamo tofauti na watanzania wengine. Na ndio maana inakuwa rahisi kutoa kejeli kama za "njori"
   
 6. M

  Masonjo JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 2,725
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kichwa cha habari hakijakaa sawa.
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Asante Mkuu kwa kuweka wazi.

  Amandla......
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Kusema kweli tunahitaji katiba mpya haraka sana badala ya hii iliyojaa viraka hadi vinaulizana "umekuja lini" na vingine vikipingana. Kuchaguliwa kwa Dr Slaa itakuwa na hatua kubwa katika kuanza mkakati wa kuwa na katiba mpya.
   
 9. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Nikinukuu maneneo halisi ni kwamba "ameahidi kuanza mchakato wa utengenezaji wa katiba mpya ndani ya miezi minne ameahidi kuanza mchakato wa utengenezaji wa katiba mpya ndani ya miezi minne". Hii inawezekana kabisa. Hapo kwenye katiba ndo kwenye tatizo la msingi linalosababisha kero nyingi nchini. Songa mbele doc, tuko pamoja. HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Katiba mpya ni lazima wanasiasa wamejigeuza miungu watu
   
 11. d

  dadakuona Member

  #11
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kweli umelonga kweli huo ni usanii wa siasa hivi miezi minne atoe Katiba mimi naona anaota hiyo kauli kaitoa tu kama gear ya kuingilia Ikulu. Hatumchagui ng'oo. Kwani anaonesha ana uchu wa madaraka na sio mkweli. NO FOR SLAA 2010
   
 12. M

  Mnyagundu Senior Member

  #12
  Sep 7, 2010
  Joined: Oct 3, 2008
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mheshimiwa hivi u Dr.wake ni wa kupora wake za watu, du hii ni kali ya mwaka. yeye si Dr. Makombora si angetungua kitu kipyaa????? sasa akina OBAMA wa USA halahala kuja TZ na ma firstlady wenu atakapoingia hekaluni kwani watatunguliwa kwa staili ya B52.
   
 13. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  jamani silaha, nnamuonea huruma, pole padri mstaafu mzinzi
   
 14. FYATU

  FYATU JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2016
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 3,924
  Likes Received: 2,120
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kwenye ile orodha hilo ndio litavuta fund haraka?
   
Loading...