Moja ya sababu zilizomfanya Rostam Azizi ajiuzuru ni pamoja na swali gumu alilokuwa akiulizwa na wananchi kupitia vyombo vya habari kwamba, Je, kwa kuwa yeye alikuwa mwakilishi wa wananchi, ilikuwaje akawasaliti na kuweza kusimama upande wa DOWANS kuwanyonya walipa kodi? Aidha, swali gumu zaidi lingine ni kwa nini sasa kwa vile yeye ni mwakilishi wa walipakodi na kama kweli ana uzalendo na kutokana na kauli zake kwamba, tozo lililotamkwa kwenye tuzo hiyo yeye ni pato la siku moja tu; basi kwa nini asijilipe mwenyewe? Ama kwa nini asifute madai hayo?
Hivyo basi, leo tunaposoma ama kusikia habari za hukumu kutoka makao makuu, ni matokeo ya Rostam Aziz kukosa uzalendo na kuamua kutotusikiliza wananchi ombi letu la yeye kujilipa mwenyewe kwa vile ni yeye huyo huyo aliyetusaliti na kuwa upande wa watapeli ambao, mwisho wa siku wanataka kuchota mali za umma kupitia uongozi dhaifu wa nchi. Hapa tusikubali kabisa na moja kati ya hatua tunazoweza kufanya ni pamoja na maandamano na hata kukusanya sahihi za watu nchi nzima kupiga kutekelezwa kwa hukumu hiyo. Labda wajilipe kupitia mishahara yao (Kikwete, Ngeleja na wengine wote walioshiriki kuruhusu mkataba feki kati ya Serikali na Dowans, mojawapo ni baraza la mawaziri wa kipindi hicho; wote wawajibike na siyo sisi walipa kodi).
Ni hukumu ya ukichaa na sisi wananchi hebu tuwe vichaa tuone nani mwenye nguvu kuliko mwenzake. Haiwezekana hawa jamaa wa huko uarabuni wakaanza kulipwa tuzo za bure bure tu hivi hivi, eti kwa sababu walimsaidia ****** kushinda chaguzi zake kwa kummiminia fedha ili sisi walipa kodi tuje tuzilipe kupitia mlango wa nyuma namna hii. Kama tunawalipa kwanza, kwa nini hawatuambii mmiliki wa DOWANS? Eti Rais naye ambaye kupitia Baraza la Mawaziri aliwajadili hawa jamaa wakati huo ili kuwapa mkataba anatuambia hamjui mmiliki!
HAKUNA KULALA na hatukubali kuwa watumwa kwa mara ya pili tena mchana kweupe namna hii.