Elections 2010 CHADEMA kuandaa maandamano makubwa Igunga Ijumaa kupinga kulipwa DOWANS

Nawashauri watumie helkopta kufikia wananchi wengi na kuwaelezea kuhusu iyo ukumu ya mahakama kuliko kuandamana kwani hawataruhusiwa na wakirazimisha yanaweza tokea ya Arusha.Ujumbe kupitia mikutano ya kawaida unatosha.
 
Magamba wanajifanya wajanja wameona wachomekee hii chapchap wakati huu kwa sababu wapinzani wako biz na Igunga. Hapo CDM wamewakamata na najua polisi watakataa kwa sababu za kiinteligesia. CDM fanyeni hayo maandamano siku ya kufunga kampeni .
 
Moja ya sababu zilizomfanya Rostam Azizi ajiuzuru ni pamoja na swali gumu alilokuwa akiulizwa na wananchi kupitia vyombo vya habari kwamba, Je, kwa kuwa yeye alikuwa mwakilishi wa wananchi, ilikuwaje akawasaliti na kuweza kusimama upande wa DOWANS kuwanyonya walipa kodi? Aidha, swali gumu zaidi lingine ni kwa nini sasa kwa vile yeye ni mwakilishi wa walipakodi na kama kweli ana uzalendo na kutokana na kauli zake kwamba, tozo lililotamkwa kwenye tuzo hiyo yeye ni pato la siku moja tu; basi kwa nini asijilipe mwenyewe? Ama kwa nini asifute madai hayo?

Hivyo basi, leo tunaposoma ama kusikia habari za hukumu kutoka makao makuu, ni matokeo ya Rostam Aziz kukosa uzalendo na kuamua kutotusikiliza wananchi ombi letu la yeye kujilipa mwenyewe kwa vile ni yeye huyo huyo aliyetusaliti na kuwa upande wa watapeli ambao, mwisho wa siku wanataka kuchota mali za umma kupitia uongozi dhaifu wa nchi. Hapa tusikubali kabisa na moja kati ya hatua tunazoweza kufanya ni pamoja na maandamano na hata kukusanya sahihi za watu nchi nzima kupiga kutekelezwa kwa hukumu hiyo. Labda wajilipe kupitia mishahara yao (Kikwete, Ngeleja na wengine wote walioshiriki kuruhusu mkataba feki kati ya Serikali na Dowans, mojawapo ni baraza la mawaziri wa kipindi hicho; wote wawajibike na siyo sisi walipa kodi).

Ni hukumu ya ukichaa na sisi wananchi hebu tuwe vichaa tuone nani mwenye nguvu kuliko mwenzake. Haiwezekana hawa jamaa wa huko uarabuni wakaanza kulipwa tuzo za bure bure tu hivi hivi, eti kwa sababu walimsaidia ****** kushinda chaguzi zake kwa kummiminia fedha ili sisi walipa kodi tuje tuzilipe kupitia mlango wa nyuma namna hii. Kama tunawalipa kwanza, kwa nini hawatuambii mmiliki wa DOWANS? Eti Rais naye ambaye kupitia Baraza la Mawaziri aliwajadili hawa jamaa wakati huo ili kuwapa mkataba anatuambia hamjui mmiliki!

HAKUNA KULALA na hatukubali kuwa watumwa kwa mara ya pili tena mchana kweupe namna hii.
 
Shame to Goverment to accept the payment.
hapo watu wanatafuta ulaji uzalendo haupo tena kila moja ana wahisha kabla ya 2015.

Laana zitawatufana kwa kutumia vibaya wale wote wenye mamlaka
 
Wakowapi wanaotetea mafisadi Igunga ili waendelee kutuvuna hivi,je wao wanaona watanzania wanahaki kunyanyaswa hivi,mbona hawatoi matamko ya kulaani tozo hiyo.Huu ni mwanzo tuu bado maovu mengi yatafanywa ndani ya miaka minne iliyobakia kwa kuwa watetezi watasema watawala wanasakamwa kwa sababu maalum
 
Hii ni aibu kubwa kweli..nchi ishauzwa na si ajabu hata igunga wamepania kulibeba kwa njia yoyote..we are Tanzanians, let's join handsh,...'together we can'. Safari ndo inaanza.. Hongera CDM kwa kuonesha.
 
Kama kuna mtu anafuatilia timeline ya matukio hapa Tz atagundua mpangilio wa matukio ambayo kwa namna hali ilivyo yatakuwa designed na Grand Architect- "The Mastermind himself"

Kwa sasa macho na masikio ya watanzania wengi yapo igunga, halafu hukumu ndio inatolewa! Tena ya malipo! WHY NOW?

Hakika wajinga ndio waliwao. But kwa kuwa sasa ujinga umetutoka hatuwezi kukubaliana na hii dhuluma iliyosababishwa na siasa chafu, na za makundi ndani ya CCM.

Hongera CDM kama mtakuwa mmeliona hili na kuwasha moto huko huko kwenye uwanja wa mapambano. Bahati nzuri ni kwamba, dhuluma hizi na hila za namna hii zinaweza kugeuzwa kuwa opportunity zenu kisiasa na kuwaongezea karata zenu za mwisho. They didn't see you coming
 
hii hukumu imekuja wakati muafaka sasa naamini wataacha kuhubiri udini wa DC wajaribu kuhubiri malipo ya dowans especially magamba ili wananchi waelewe kwa nini magamba wanataka kuifirisi nchi hii
 
Nimepata habari sasa hivi kutoka Igunga kuwa CDM inaandaa maandamano makubwa Igunga baada ya hukumu ya Mahakama Kuu ya kuitaka Tanesco iilipe kampuni fake Dowans, iliyozaliwa kutoka kampuni nyingine fake ya Richmond.

CDM wanaangalia uwezekano wa wafuasi wake wa mikoa na wilaya jirani kuhamasisha katika maandamano hayo ambayo yataenda sambamba na kampeni za kulichukuwa hilo jimbo lililotelekezwa na fisadi aliyesababisha tozo hiyo.
Waacheni waandamane, ni moja kati ya ilani ya uchaguzi 2010 sasa lazima watekeleze kwa vitendo. Laikini na wao watambue iko siku watajibu hizo pesa za kuchezea zinatoka wapi? wasituambie kuwa ni za wafadhili kwa vile wafadhili hawajazitoa kwa ajili ya maandamano. Hivi mara baada ya maandamano, wafuasi hujulishwa kiasi cha fedha walichotumia? wanabaki kujua MBOWE NA SLAA
 
Nawashauri watumie helkopta kufikia wananchi wengi na kuwaelezea kuhusu iyo ukumu ya mahakama kuliko kuandamana kwani hawataruhusiwa na wakirazimisha yanaweza tokea ya Arusha.Ujumbe kupitia mikutano ya kawaida unatosha.
Wakilazimisha siyo "WAKIRAZIMISHA" na kishwahili chako hicho usitegemee hata ubalozi wa nyumba 10 ndani ya CDM
 
Nimepata habari sasa hivi kutoka Igunga kuwa CDM inaandaa maandamano makubwa Igunga baada ya hukumu ya Mahakama Kuu ya kuitaka Tanesco iilipe kampuni fake Dowans, iliyozaliwa kutoka kampuni nyingine fake ya Richmond.

CDM wanaangalia uwezekano wa wafuasi wake wa mikoa na wilaya jirani kuhamasisha katika maandamano hayo ambayo yataenda sambamba na kampeni za kulichukuwa hilo jimbo lililotelekezwa na fisadi aliyesababisha tozo hiyo.

Siyo rahisi kupata kibali cha polisi hasa ukizingatia ni kipindi cha kampeni za uchaguzi na polisi wengi watakuwa kwenye mikutano ya kampeni.
Nivema upinzani hasa CDM wakawaeleza wananchi ccm na mbunge wao aliyepita alivyoifikisha hii nchi hapa kuja kulipa tuzo hiyo ambayo itakuwa mzigo wa wananchi.
 
Nimepata habari sasa hivi kutoka Igunga kuwa CDM inaandaa maandamano makubwa Igunga baada ya hukumu ya Mahakama Kuu ya kuitaka Tanesco iilipe kampuni fake Dowans, iliyozaliwa kutoka kampuni nyingine fake ya Richmond.

CDM wanaangalia uwezekano wa wafuasi wake wa mikoa na wilaya jirani kuhamasisha katika maandamano hayo ambayo yataenda sambamba na kampeni za kulichukuwa hilo jimbo lililotelekezwa na fisadi aliyesababisha tozo hiyo.

kwenye red bolded umeharibu.
Una uhakika limetelekezwa?

Kalirudisha kwa wananchi, waamue juu ya hatma ya maisha yao
 
Magamba wanajifanya wajanja wameona wachomekee hii chapchap wakati huu kwa sababu wapinzani wako biz na Igunga. Hapo CDM wamewakamata na najua polisi watakataa kwa sababu za kiinteligesia. CDM fanyeni hayo maandamano siku ya kufunga kampeni .
Mkuu! Naunga hoja mkono.
 
Tunaunga mkono maandamano hayo kwa asilimia 100%, kwani HUKUMU hiyo HAITEKELEZEKI. kisha tumchunguze huyo Jaji aliyetoa hiyo hukumu kama ni Mtanzania au ni Mwekezaji. Pia kama CV yake inaonyesha alishawahi kufanya kazi IMMA.
 
Fedha hizi ni nyingi sana, Chadema kuzipigania kwa njia ya maandamano ya amani ni vema na haki. Suala hili pia litakuwa limewakalia vibaya ccm huko igunga. Kazi kwao.
 
mkiandamana tu wakati mnajikusanya Cuf tunawaambia kuwa tunapitisha helkopta na kukomba watu wote na maandamano yanafia hapo hapo.
Kipofu kaona mwezi,tangu helikopta ya CUF ije naona hata hamlali,ufisadi,wizi wa mali za waTZ hauwezi kufunikwa kwa helikopta, naamini kabisa baada ya uchaguzi igunga viongozi wa CUF watawekwa rehani kufidia gharama za matumizi ya hiyo helikopta kwa sababu mmekurupuka kuiga bila kujua wenzenu wamewezaje, we shabikia tu.
 
bravo!
Kama ni kweli yatakuwepo ntaona kweli CDM wanahubiri siasa zao kwa vitendo, japo najua Polisi hawatayaruhusu
Ngoja tuone
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom