CHADEMA kitafilisika kwa mtaji wa fahari ya macho

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
nyerere-kikwete.jpg

Rais Jakaya Kikwete na Mwl Julius Nyerere


WASWAHILI wana usemi wao mashuhuri usemao fahari ya macho huwa haifilisi duka na kuona aghalab si kuchukua bali ni kutia macho nuru.

Semi hii ni rahisi sana kuinena mdomoni na nyepesi kunasa masikioni ila ina ni vema kuanza kuichambua katika kina cha kimaarifa na kiakili ili hatimaye kuipatia tafsiri au maana iliyo kamilifu.

Mwaka 1992 kilipoanzishwa na kusajiliwa kisheria chama cha Chadema na kina Mzee Edwin Mtei, Brown Ngululuipwi, Jacob Nkomola, Costa Shinganya, Victor Kimesera, Paul Kyara, Bob Makani na wengine walisikika wakisema kuwa wanadhamiria ya kujenga chama kitakachobeba matumaini ya jamii.


Wakadai wanaunda chama chenye shibe ya ustaarabu na uadilifu, kilicho na sera endelevu na chenye viongozi makini wenye dira na upeo.

Chadema ya wakati huo katika kila mikutano yake kilihimiza azma kuu ya kupita katika njia ya kuimarisha na kushamirisha dhana ya misingi ya amani, umoja na kuendeleza utulivu uliopo nchini mwetu.

Mikutano mingi ya Chadema iliyoanza kufanyika jijini Dar es Salaam ambayo mgeni mkuu akiwa Mzee Mtei kama mwenyekiti wake wa taifa, yeye na timu yake walionekana kuegemea zaidi katika kunadi sera, kujenga nguvu ya hoja na kuzikosoa sera za Serikali ya CCM iliyokuwa ikiongozwa na Rais Ali Hassan Mwinyi wakati huo.


Mtei alidiriki kusema hadharani kwamba anachokifanya Rais Mwinyi na Serikali yake ni ghiliba na kunakili au kuyafanyia kazi maoni yake aliyoyatoa katika Serikali iliyoongozwa na Rais Julius Nyerere juu ya sera za IMF na Benki ya Dunia. Mtei alipingwa na Serikali ya Nyerere kuhusu pendekekezo lake la kuitaka Serikali iafiki matakwa ya taasisi hizo, Rais Nyerere akasema hatageuka nyuma na kuwa jiwe.


Pengine Mtei alikuwa akijua nini maana ya kuheshimu msimamo,kujiamini, kusimamia sera kwa nguvu ya hoja katika kusimamia kisawasawa dhamira na azma aliyonayo.

Hata pale mwanasiasa mashuhuri Oscar Kambona aliyekuwa akiishi uhamishoni nchini Uingereza aliporejea Tanzania Chadema hakikutaka kumpapatikia wala kumshawishi ili ajiunge kwao kilimpuuza na kumuona ni muflisi.

CHANZO: Gazeti la Mtanzania
 
Akitaja Chadema tu anaridhika hata kama hana point; safi sana; CDM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Sijakuelewa hata kdogo!

This is not a critic to CHADEMA it is plus for Chadema; it was written 4 people to think... wakati wa kuanzishwa Chadema hakikuwa na watu wenye tittle what Matters to that new party was kunadi sera, kujenga nguvu ya hoja na kuzikosoa sera za Serikali ... Hata wakati Kambona anarudi hawakumkimbilia kujiunga na Chadema kupata mtaji wa fahari ya Macho...
 
Maudhui ya heading yanapishana na habari yenyewe.
Ila nimependa maelezo yako maana nimepata ufahamu wa ziada. Namna walivyoanza na wanavyoendesha siasa yao sasa ni dhahiri Chadema are destined for Greatness.
 
Badili title basi ueleweke au siyo?
This is not a critic to CHADEMA it is plus for Chadema; it was written 4 people to think... wakati wa kuanzishwa Chadema hakikuwa na watu wenye tittle what Matters to that new party was kunadi sera, kujenga nguvu ya hoja na kuzikosoa sera za Serikali ... Hata wakati Kambona anarudi hawakumkimbilia kujiunga na Chadema kupata mtaji wa fahari ya Macho...
 
Back
Top Bottom