CHADEMA kisisikilizwe tena!

Ndugu ZeMarcoPolo nimesoma kila post katika thread hii, hakuna hata mmoja aliye thubutu kujibu hoja zako! Fact ni kwamba ur article is too strong for these week minds! Thanks bro, Keep it up!

Asante ndugu.
Tuendelee kukumbushana uzalendo kwa nchi yetu.
 
Hii haina u-strong wowote. Heri hata Kamguu katatu ka mtoto wangu wa miezi 6 kana u-strong zaidi kuliko huo upupu hapo juu. Kama wewe unaona ni Strong basi naona wewe Mkuu JUA LIMEKUWAKIA na ndiyo maana walisifia. Kidumu chama cha Mapinduzi ya kumuondoa Nyerere na Matunda yake.

CCM wamekata Umeme na mie ndani umeisha. Ngoja nitoke na Wanangu na madebe yetu tukanunue kwa Waarabu wa hapa Mujini Sikonge. Uzuri si mbali sana na hiki kipikipiki changu cha Mchina.
Ndugu ZeMarcoPolo nimesoma kila post katika thread hii, hakuna hata mmoja aliye thubutu kujibu hoja zako! Fact ni kwamba ur article is too strong for these week minds! Thanks bro, Keep it up!
 
Ndugu ZeMarcoPolo nimesoma kila post katika thread hii, hakuna hata mmoja aliye thubutu kujibu hoja zako! Fact ni kwamba ur article is too strong for these week minds! Thanks bro, Keep it up!

Mazee kwanini usiandike kiswahili tu! Siku nyingine utaandika these year minds!
 
Upuuzi mwingine
 
Nimekugongea Senkyu kabla sijatimka.

Hii ndiyo inaitwa STRONG POINT OF THESE WEEK MINDS. Keep it up bro..... 😛eace:
Mazee kwanini usiandike kiswahili tu! Siku nyingine utaandika these year minds!
 

u r an asshole of u r own
 
Kuwa mkamilifu kazi kwelikweli inahitaji uelewa na ukamilifu wa dahari Arusha na Hai vimeingilianaje hapo au alijaribu kuleta mfano ghafla ikawa ndo hoja?? najiuliza bado, ila hajaeleza kwanini cdm waliandamana Arusha Je walikuwa na haki kuandamana na kwanini walipigwa risasi za moto badala ya kuwalinda na maandamano yao? kama polisi waliona kuna dalili za uvunjifu wa amani katika maandamano yale je walichukua hatua gani kuzuia uvunjifu wa amani? Je walichagua kupiga watu risasi za moto ndo kuzuia uvunjifu wa amani Arusha??? Zaidi wakijibu Hoja za mwanzo ndo tutajua nani alikuwa sahihi na nani mchonganishi wa amani Arusha Nimewakilisha tuu wadau!!:amen:
 
ND WANA JF
Propaganda hazijengi hii nchi yetu sote,na ukWeli unatabia ya kujitenga siku zote,huyu anaye jiitA zemarcopolo
asiwababaishe hana analolijua kuhusiana na arusha na hai,amesikiliza kipindi cha ccm walichonunua air time pale chn 10
na kumtuma tambwe hizza mtu wa propaganda kuupotosha umma wa watanzania,lkn wamefeli kwani miongoni wa umma
tupo tunaoujua ukweli from a to z,JUMLA YA WAJUMBE WA KIKAO HALALI CHA KUMCHAGUA MEYA WA ARSHA NI 31(INCLUDE CHITANDA)
CDM MADIWANI 8,VITI MAALUM 3,MBUNGE ARUSHA LEMA,MBUNGE VITI MAALUM 1
TLP 1,
CCM 10 NA MAALUM 3,WABUNGE VITI MAALUM 3(INCLUDE CHITANDA) TOTAL 31,
KANUNI ZINASEMA LAZIMA WAJUMBE WAFIKIE IDADI YA 2/3 YA WAJUMBE WOTE AMBAO NI 21,SIKU YA TUKIO DIWANI WA TLP ALIKUWA UPANDE WA CHADEMA,HIVYO CCM 16 NA CDM 15,UKATOKEA MVUTANO WA KUTAKA KUJUA UHALALI WA CCM KUWA NA WABUNGE 3 WA VITI MAALUM,JAMBO AMBALO PIA LINAKINZANA NA KANUNI AMBAZO ZINASEAMA WABUNGE WA VITI MAALUM NDANI YA JIMBO WASIZIDI 2,HIVYO KIKAO KILIAIRISHWA MPAKA KESHO YAKE AMBAPO,KULIIKUWA NA SEMINA YA MADIWANI NA OFISI YA MKURUGENZI ILIWATAARIFU
WAENDE ENEO HUSIKA,WALIPOKUWA HUKO MDA ULIKUWA UMEENDA BILA TAARIFA ZOZOTE HUKU WAKIWA WENYEWE WANAJADILIANA KUHUSU UHALALI WA CHITANDA,NDIPO DIWANI WA TLP AKAKUBALIANA NAO ANAENDA OFISI ZA MKOA AMBAPO HUKO HATUJUI NN KILITOKEA NA YEYE AKAUKWAA UNAIBU MEYA,WAKAPATA TAARIFA KUWA WENZAO WANACHAGUA MEYA,KAMA KAWAIDA LEMA AKAONGOZANA NA MADIWANI WAKE MPAKA OFISINI HAPO,NA ALIINGIA NDANI,MKURUGENZI AMBAYE NDIO MWENYEKITI WA KIKAO HICHO NA UCHAGUZI,AKAWAITA POLISI AKASEMA LEMA ANAFANYA FUJO,MTAKUMBUKA SIKU HIYO UCHAGUZI WA MEYA MBUNGE LEMA ALIPIGWA NA POLISI HADI KULAZWA.
SASA UTAONA JINSI HII NCHI INAPOELEKA MBUNGE AMEBURUTWA KUTOKA NDANI YA KIKAO NA KUPOKEA KICHAPO,WAKATI IPO WAZI MKURUGENZI ALIVUNJA KANUNI KWA MAKUSUDI AU KWA KUSHINIKIZWA,AMEFANYA UCHAGUZI BILA QUORUM KUTIMIA,WAJUMBE WALIOKUWEPO NI 17 BADALA YA 21,HIVYO NGUDU ZEMARCOPOLO ACHANA NA PROPAGANDA TUNAUJUA UKWELI,HAKUNA WA KUTUYUMBISHA TUNATAKA MAENDELEO NI PROPAGANDA ZENU NA UTUWAMBIE HICHO CHAMA MBADALA NI KIPI,KISHA UTUAMBIE KIMEFANYA NN KWA WATANZANIA,SS TUNAJIVUNIA CHAMA CHOCHOTE CHENYE NIA YA DHATI KWA WATANZANIA NA SIO HADITHI
ZA KINTEJILISIA NA MCHAKATO USIOISHAAA,NI HAYO TU,PIA KUMBUKA TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO NA SIO WAGANGA NJAA.
 
 
Asante ndugu.
Tuendelee kukumbushana uzalendo kwa nchi yetu.

Ntakubaliana na Article yako kama kuna siku nitasoma makala hapa JF inahozungumzia uozo ama uharo wa CCM ambayo itakuwa imeandikwa na wewe...

Dobi wa kweli utamjuwa siku akipewa nguo nyeupe.

Nakusubiri Mama
 

Mtu akinyimwa haki anaenda mahakamani au anaitisha maandamano?
Ikiwa kila kikundi kinachohisi kimenyimwa haki kikiamua kuitisha maandamano tutaweza kuendelea na shughuli nyingine za maendeleo?
 
Ntakubaliana na Article yako kama kuna siku nitasoma makala hapa JF inahozungumzia uozo ama uharo wa CCM ambayo itakuwa imeandikwa na wewe...

Dobi wa kweli utamjuwa siku akipewa nguo nyeupe.

Nakusubiri Mama

Kama umeisoma vizuri article yangu utaona kuwa nimeeleza kuwa wajumbe wa CCM Halmashauri ya Hai hawakuwa sahihi. Nini zaidi unahitaji?
 
Tukishakosa hoja z kujibia hoja tunapinga huku tukisubiri kina flani waje watujibie!!! Great Thinkers!!!
 
Tukishakosa hoja z kujibia hoja tunapinga huku tukisubiri kina flani waje watujibie!!! Great Thinkers!!!

Unfortunatelly hiyo ndio JF ya siku hizi. JamiiForums sasa imekuwa idara rasmi ya CHADEMA!
 
Unfortunatelly hiyo ndio JF ya siku hizi. JamiiForums sasa imekuwa idara rasmi ya CHADEMA!
Si hamia kwenye idara ya ccm unatafuta nini wewe hapa? ebooooo kama unakuja na crap unaambiwa hata ungekuwa wewe ni Mbowe! Shiiitttty
 
Mtu akinyimwa haki anaenda mahakamani au anaitisha maandamano?
Ikiwa kila kikundi kinachohisi kimenyimwa haki kikiamua kuitisha maandamano tutaweza kuendelea na shughuli nyingine za maendeleo?
Katiba ya nchi inaruhusu mtu au watu kuandamana kupinga kitu chochote ambacho kinawakera. Umezoea ukandamizaji wa ccm ndo maanna unadhani kuandamanai ni kosa la jinai hivyo unastaili kupigwa lisasi. Pole maana wewe ni mtoto au kibaraka wa mafisadi ndo maana unachangia upuuzi tupu. Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtanzania mwenye nia njema na nchi hii ataweza kuitetea ccm kama sio fisadi au kibaraka wa ufisadi. Hakuna kitakachozuia mabbadiliko yaliyoanza, someni alama za nyakati. Hatakama mtatumia njia za kumwaga damu bado hamtazuia bali mtapandisha ujasiri wa watu kusonga mbele kwenye haya mapambano. Kumbuka jambo hili la badiliko haliji kwa sababi ya chadema, bali ni hasira kwa serikali na ccm ambayo wananchi wameirundika mioyoni mwao kwa muda mrefu na sasa they can't take anymore. Hakuna jiwe litakalobaki juu ya lingine ccm na utawala dhalimu unaishia na wala hautaamka tena. Mtailaumu sana chadema lakini ukweli uko wazi kwamba hatakama cdm wangekaa kimya bado wananchi wangeripuka si muda mrefu. tumechoka kuliwa nguvu zetu na kikundi kidogo cha mafisadi wa ccm. Peoples powaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Ninachokifahamu mimi na kukisoma kwenye vyombo vya habari ni kwamba - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai umefanyika baada ya vurugu za Arusha. CHADEMA ilishinda uchaguzi huo baada ya kupigiwa kura mmoja wa madiwani wa CCM. Makamu mwenyekiti ilishindikana kumpata mshindi baada ya kura kulingana, na hivyo kukubaliana kuongoza nusu kipindi kwa kila chama huku wa CCM akianza kushika nafasi hiyo kwa nusu ya kwanza. Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai, aliwakatalia kupiga kura Wabunge wa viti maalum kwa sababu anazozijua yeye, pamoja na kuwepo barua ya Mwanasheria Mkuu wa serikali iliyomtaka awaruhusu.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi na kufanikiwa kuongoza Halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.
Diwani wa Kata ya Machame Kaskazini, Clement Kwayu, ndiye alishinda nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo. Hai ni Halmashauri ya sita kuongozwa na CHADEMA nyingine ni Kigoma Ujiji, Mwanza, Musoma Mjini, Karatu, Moshi Mjini.
Kabla ya jana, uchaguzi huo ulishindikana na kuahirishwa mara mbili, baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Melkizedeck Humbe, kukataa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, aliyeruhusu wabunge wawili wa Viti Maalumu mkoani Kilimanjaro kupitia CHADEMA, Lucy Owenya na Grace Kiwelu, kuwa ni wajumbe halali wa baraza hilo.
Kwayu alipata kura 12 dhidi ya mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ally Mwanga, aliyepata kura 10. Nafasi ya makamu mwenyekiti haikupata mshindi, kwani walifungana kwa kura, hata baada ya kurudiwa.
Baraza la Madiwani wa wilaya hiyo, lilikubaliana na kauli moja kuwa waliokuwa wakigombea nafasi hiyo waongoze kwa kuachiana.
Atakayeanza kuongoza kwenye nafasi ya makamu mwenyekiti katika mwaka wa kwanza ni Diwani wa Kata ya Weruweru, Adris Mandrai (CCM). Baadaye atafuata Diwani wa Kata ya Masama Kati, Deogratius Kimaro (CHADEMA).
Hata hivyo, matokeo hayo yameibua mtafaruku ndani ya CCM baada ya viongozi wa chama hicho kudai kuwa kuna diwani wao mmoja ambaye amewasaliti na wanamjua. Walidai watamfukuza kwenye chama.
Kila chama kilikuwa na wajumbe 11, hali iliyokuwa inaviweka katika wakati mgumu wa kupata mshindi.
Awali, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa kikao hicho, aliwataka watendaji wa serikali kujifunza taratibu za uongozi.
Alisema kuwa kitendo cha watendaji kukaidi maelekezo ya Mwanasheria Mkuu ni ushahidi kwamba watendaji hao hawajui taratibu za uendeshaji wa shughuli za kila siku ndani ya serikali yao.


Source: Tanzania daima
 
cha kujiuliza ni kwamba,je? HUYO MH. CHATANDA NAYE ALISAJILIWA KM MJUMBE HUKO ARUSHA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…