CHADEMA kinahitaji kura kutoka Tanga

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289

Kuna wakati ilikuwa ni vigumu kufikiri kwamba CHADEMA kinaweza kupata kiti cha ubunge kutoka Singida lakini Kamanda Tundu Lissu akadhihirisha kwamba hakuna ngome isiyopitika. Na si ajabu mwaka 2015 vitapatikani viti zaidi vya ubunge kutoka singida tukianza na jimbo la Iramba Magharibi.


Vilevile kuna wakati ilikuwa ni vigumu kufikiri CHADEMA inaweza kupata kata hata moja kutoka Tabora lakini hili likawezekana. Tofauti ya kura za ubunge kule Igunga imedhihirisha hakuna ngome isiyopitika. Lakini vilevile alama ya kukosa kata kule Shinyaga inatupa tafakari nyingine.

Kuna wakati baadhi ya wanachama/wafuasi wa CHADEMA wanaweza kufikiri wanaweza kushinda kwa ngazi ya uraisi kwa kutegemea baadhi ya mikoa (Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya, Shinyanga n.k. ) kwa kisingizio cha chama kukubalika sana na idadi kubwa ya watu bila ya angalau asilimia 40 ya kura kutoka Tanga. Hili ni jambo la kutilia shaka. Naomba nikumbushe:

Kwa mfano: Ukiwa unaamini kwamba Mkoa wa Arusha na Mwanza au Shinyanga ni ngome imara ya CHADEMA na kinashindwa kupata zaidi ya asilimia sitini ya kura na wakati huohuo CCM inapata zaidi ya asilimia 60 ya kura kutoka Tanga (tena mkoa wenye idadi wa watu zaidi ya milioni 1.5) ujue hapa ushindi upo mashakani.

Vilevile unapoona Mbunge wa CHADEMA anashinda jimbo fulani na wakati huohuo mgombea uraisi wa CHADEMA anashindwa na mgombea wa CCM ushindi kwa ngazi ya uraisi ipo mashakani.

Ushindi wa CHADEMA kwa ngazi ya uraisi hauwezi kutokana na wingi wa kura toka kwenye baadhi ya mikoa bali wastani usiopungua chini ya asilimia 40 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.Nguvu ya ziada inahitajika.


Nawakilisha. 

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
314
M4C itazipita hizo sehemu zote ulizosema mkuu nadhani usishange tanga tukapata hata wabunge wawili napiga hesabu muhenza, tanga mjini,korogwe yapo kama wazi vile utashi wetu na ushawishi wetu wenye sera za kuwakomboa wana tanga zitatupatia ushindi kuanzia udiwani ubunge mpaka uraisi.

Wana Tanga wanahitaji machache kwa haraka haraka.
1.Elimu bado ni duni
2.Katani ni kama inakufa tunahitaji sera bora za katani kina zitto walipita kura
3.Bandari ipanuliwe ilete ajira kama itapanuliwa vizuri bandari ya tanga ina maana tuta pambana na bandari ya mombasa ajira zitakua nyingi
4.Wananchi wa tanga hasa lushoto wanahitaji kahawa itawalipaje hapa nalenga bumbuli mpaka sasa kahawa bado haiwalipi
5.Wananchi wa tanga wanahitaji reli itakayotoka tanga kwenda hadi uganda kuongeza ajira kupitia bandari

Fred kavishe
 

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
M4C itazipita hizo sehemu zote ulizosema mkuu nadhani usishange tanga tukapata hata wabunge wawili napiga hesabu muhenza, tanga mjini,korogwe yapo kama wazi vile utashi wetu na ushawishi wetu wenye sera za kuwakomboa wana tanga zitatupatia ushindi kuanzia udiwani ubunge mpaka uraisi.

Wana Tanga wanahitaji machache kwa haraka haraka.
1.Elimu bado ni duni
2.Katani ni kama inakufa tunahitaji sera bora za katani kina zitto walipita kura
3.Bandari ipanuliwe ilete ajira kama itapanuliwa vizuri bandari ya tanga ina maana tuta pambana na bandari ya mombasa ajira zitakua nyingi
4.Wananchi wa tanga hasa lushoto wanahitaji kahawa itawalipaje hapa nalenga bumbuli mpaka sasa kahawa bado haiwalipi
5.Wananchi wa tanga wanahitaji reli itakayotoka tanga kwenda hadi uganda kuongeza ajira kupitia bandari

Fred kavishe

Respect! Umetoa mchango mzuri kwa kuzingatia uhalisia na hali halisi ya mkoa wa Tanga, suala la kupita kwa M4C Tanga lipo wazi, kwa ratiba ya kwanza ya M4C ilipaswa ifanyike mwezi wa 10 but unfortunately hili halikufanyika kutokana na unavoidable circumstances. But kuna jambo moja hapa naomba nisisitize kwa wana-CDM wenzangu kwamba: Tusifikiri tunaweza kushinda nafasi ya uraisi bila kuweka wastani mzuri wa kura kutoka kila mkoa wa Tanzania Bara.

Kutoka makao Makuu ya CDM mpaka Mwanza, Kigoma, Shinyanga au Arusha ni mbali zaidi kuliko kufika Tanga. Tukiwa tunapita mkoa wa Tanga kuelekea Kilimanjaro au Arusha tusipite kwa shingo upande tukidhani watu wa Tanga hawabadilki hasa kwa Makamanda wenzangu wa CDM wanaoamini katika mabadiliko.
 

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
314
Mkuu hata wewe unaweza anza hamasisha usisubiri makao makuu waje anza nyumba hadi nyumba kitaeleweka tu
 

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Mkuu hata wewe unaweza anza hamasisha usisubiri makao makuu waje anza nyumba hadi nyumba kitaeleweka tu

Narrow Minded! Maneno rahisi yasiyo na kanuni za kiutendaji...politics is not a simple task as you think, politics is war without a bloodshed! Copy my words.
 

charityboy

Senior Member
Nov 11, 2010
138
4
Katika tafiti binafsi ambayo nakaribia kuimaliza ndani ya mwezi imeonyesha kuwa hali ya kukubalika kwa cdm katika mikoa ya pwani na pembezoni mwa nchi sio nzuri. Hii inahusisha mikoa ya kagera, kigoma, rukwa, mtwara, lindi, tanga, pwani, na arusha.
Chadema imeonyesha nguvu katika mikoa ya katikati kama dodoma na singida.
Kushinda uraisi tanzania ni lazima ukubalike na mikoa ya pwani ambayo nguvu ya cdm ni ndogo sana. Tafiti hii itakapomalizika mwishoni mwa mwezi huu tutatoa mchanganuo mrefu zaidi na kwa uwazi kabisa. Bila shaka cdm wataitumia tafiti hii katika kujiboresha zaidi kuelekea 2015.
Ninafanya summary yake na nitamkabidhi mh. mnyika mbunge wangu ili aifikishe makao makuu ya chama.
Tafiti hii ni ndogo na imehusisha chama kimoja tu cha chadema.
 

KANYIMBI

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
1,857
3,586
Iwapo katiba mpya ya Jaji Warioba itakamilika mapema kabla ya 2015, Mie ninaimani Katiba mpya itatambua uwepo wa nchi za Zanzibar na Tanganyika pamoja na jamhuri ya muungano wa mkataba wa Tanzania. Na Ili CDM iweze kupata kura za Urais kutoka Tanga na maeneo mengine yaliyojaa wana uhamsho kama Zenji, ni vyema wakamsimamisha Zito kabwe ili agombee nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano kisha Dr Slaa agombee urais wa nchi ya Tanganyika. Haya ni mawazo yangu finyu, nimeyafikiria baada ya kushuhudia hali ya udini inavyoshamiri ktk jamhuri ya muungano wa TZ. Hali hii niliiona kwenye uchaguzi uliopita kwani hizi dini zetu kubwa 2 kipindi cha kampeni za uchaguzi zilikuwa zina desturi ya kuwapigia chapuo wagombea wa dini zao kwenye nyumba za ibada.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom