CHADEMA Kidedea Urais SAUT

CHADEMA Kidedea Urais SAUT

Tatizo saut division for na zero zimejaa sana kile chuo hapo unategemea nini?
 
hahaha!

chama cha magaidi (ccm) vipi video ya rwakatare hawajaileta huko ikasaidia ushindi?

Wengi pro-CCM watakejeli swali lako lakini uchaguzi huu ni kipimo mojawapo cha impact ya issue ya Rwakatare!! Ni wazi sasa utambuzi katika akili za watu wengi umehama kutoka kwenye "kuaminishwa" kwenda "kujiaminisha". Uchaguzi huu umeonesha viongozi wa CCM wameshindwa "kuwaaminisha" angalau hawa wanafunzi wa SAUT.
 
Nakumbuka mahafali ya 2012 pale SAUT, chama tawala (jina la waziri kapuni) walitoa ahadi kwa mkuu wa chuo, Je kwa mabadiliko haya ahadi hizo zitatekelezeka tena?
 
St Augustine hawana mchezo na Elimu, mkichochea migomo mtaishia kupata shahada za kina mulugo! Semister ya kwanza inaisha salama bila ya migomo nadhan hali si mbaya sana vyuon ukilinganisha na msimu ulopita!
Sasa hapa ndio umeongea nini?
 
Baada ya mgombea wa urais SAUT kupitia CHADEMA Bw.Mcheshi Dovakmwene kushinda kwa kishindo dhidi ya mgombea wa CCM Peter Bega aliyekua waziri wa mikopo SAUT ambaye ni kada wa CCM Bi.Sylvester Yalerd anadaiwa kukimbia mji wa Mwanza na simu zake zinaita bila kupokelewa.

Bw.Yalerd ambaye alikua mwenyekiti wa CCM chuoni hapo na waziri wa mikopo mwaka 2011 alipewa jumla ya sh.mil 9 na uongozi wa CCM mkoa wa Mwanza kuhakikisha mgombea wao Bw.Peter Bega anashinda.

Katika kuonesha CCM Mwanza ilijipanga kushinda urais SAUT hata kwa hila, mwenyekiti wa CCM mwanza Bw.Anthony Dialo alinukuliwa akisema "SAUT mwaka huu yetu,maana mwaka jana mlibweteka sana tulipowaachia"

Kwa hiyo katika kutekeleza hilo Bw.Yalerd akaanza kupika majungu na kuichafua Chadema ili kuitafutia uhalali CCM. Akarusha madai kwa serikali inayomaliza muda wake (ambayo ni ya chadema) kuwa hajafanya kitu, madai ambayo si ya kweli.

Serikali hiyo iliyokua inaongozwa na Kamanda Malisa imefanya mengi ambayo hatuwezi kuyataja yote hapa. ndiyo serikali iliyomaliza tatizo la umeme library licha ya kuwa tatizo hilo lilikuwa ni sugu na serikali zilizopita zilishindwa.

Pia ilisimama kidete kuhakikisha bei ya hostel za nje inapungua na wakafanikiwa. Ni serikali hiyo iliyotafuta udhamini kutoka shirika la maendeleo la ujerumani kujenga vimbweta vya kusomea nje ya madarasa. ni makamanda haohao waliosimama kidete kuhakikisha bei ya vyakula inabaki 1200 pale ilipopanda kuwa 2000 mwishoni mwa mwaka jana.

kama haitoshi ni serikali ya Malisa iliyoandaa makongamano na semina mbalimbali kwa nia ya kuwezesha wanafunzi kujifunza na kuhoji. ni serikali ya chadema chini ya Malisa iliyothubutu kumleta Mh.Tundu lisu kufanya mdahalo wa hadhara licha ya kuwa mwaka jana alikuja lakini akaishia kufungiwa nje na serikali ya CCM iliyokuwepo.

Kwa kifupi serikali ya Chadema chini ya Malisa imefanya mengi na watu wakapata moyo kwa mafanikio hayo na kuapa kutoirudisha tena CCM madarakani.

Sasa ili Ccm ijipatie uhalali wa kushinda ikaanza kudiscredit kila kilichofanywa na chadema. na kazi hiyo akapewa Bi.Sylvester Yalerd akishirikiana na mwandishi mmoja wa vigazeti vya udaku Bi.Jelard Lucas. wakajifanya hawajaona lolote lililofanywa na serikali ya Malisa. kazi yao ikawa kuchafua kwenye mitandao ya kijamii ili wananchi wakate tamaa ya kuichagua CHADEMA.

Hiyo ni kazi maalum waliyopewa na sekretarieti ya CCM mkoa, katika kikao chao La Kairo Hotel wiki jana (ushahidi upo).

Lakini kumbe kuikosoa serikali ya Malisa kuwa haijafanya kitu ilikuwa sawa na kupiga upepo rangi maana wanaSAUT walijionea wenyewe na wakafurahia matunda ya chadema na kuahidi kumchagua mgombea yoyote wa chadema atakayejitokeza.

Baada ya kuona propaganda zao hazizai matunda wakaanza kumshambulia mgombea wa chadema mwaka huu Bw.Dova Mcheshi. Wakasambaza uvumi eti ni mdogo wake Malisa wa kuzaliwa na kusambaza picha eti wanafanana. wakadai eti nae ni mchaga kama alivyo Malisa na baba zao ni ndugu (soma wall ya Yalerd kwny ukurasa wake wa fb).

Hawakuishia hapo wakapandikiza hadi mbegu ya udini. eti iweje Dova awe Mlutheri kama Malisa.
Udini, undugu, ukabila ndizo zilikuwa silaha zao kubwa.

Lakini baada ya matokeo kutangazwa kuwa mgombea wa Chedema Bw.Dova Mcheshi amemshinda kada wa CCM Bw.Peter Bega, inadaiwa huko CCM kimenuka.

Pametokea mvurugano mkubwa na kina Yalerd kudaiwa hawakufanya kazi kwa pesa waliyopewa badala yake walipiga cha juu.

Inadaiwa Bw.Yalerd amekimbilia mkoa jirani wa Shinyanga kukwepa aibu, huku namba yake ya simu ikiita bila kupokelewa.

Lakini hali ni mbaya zaidi kwa mwandishi wa vigazeti vya udaku Bi.Jelard Lucas ambaye kila anachoulizwa sasa anajibu matusi. Alipopigiwa simu kwa namba yake 065.... haikupokelewa na badala yake akajibu matusi kwa sms. (sms tunayo). Inadaiwa amechanganyikiwa hadi anaandika matusi kwny wall yake. unaweza kuipitia kwa jina la Jelard Lucas kwenye fb uone alivyochanganyikiwa.

MY TAKE:
CCM futeni kabisa mawazo ya kuiongoza SAUT. Kosa mlilofanya mwaka jana kuruhusu CHADEMA kuingia madarakani chini ya uongozi shupavu wa kamanda Malisa mtalijutia milele. CDM wamefanya kazi na watu wameona. ninyi magamba mlikuwa mnauza maneno, wao wanafanya vitendo. Mwaka jana Nyambari Nyangwine alikuja kumnadi Anthony (kada wa CCM) na kumfanyia harambee bt mkashindwa, mwaka huu Dialo ametoa hela mmeshindwa tena,
mwakani hata aje Rais Kikwete na kuihamishia hazina SAUT bado mtashindwa tu. Jipangeni sana.!!!
 
Chadema pale tatizo wamejaa division 3,4 na zero wee unategemea nini
 
Halafu chuo chenyewe cha kanisa unategemea nini?
 
Back
Top Bottom