Chadema karibuni jimbo la bariadi magharibi kwa chenge(mzee wa simiyu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema karibuni jimbo la bariadi magharibi kwa chenge(mzee wa simiyu)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NGENDA NGOLOMA, Apr 20, 2012.

 1. N

  NGENDA NGOLOMA Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafurahia sana jinsi chama changu kinavyokua hasa katika kipindi hiki cha Mageuzi ya dhati yanayoratibiwa na CDM, wito wangu ni kuwa pamoja na mafanikiwa makubwa ya CDM katika Maeneo mengi, bado chama hiki pendwa na mvuto hakijaweka mizizi imara katika majimbo mawili ya Bariadi ambako ndiko makao makuu ya mkoa mpya wa Simiyu yalipo.

  Hasa ikizingatiwa kuwa katika uchaguzi mkuu 2010, chadema iliambulia patupu katika majimbo haya na kumuacha ''Mzee wa Vijisenti'' na '' Bw. Mapesa'' wakinawili kwa pasipo hata kupiga Kampeini za Maana. Hivyo nawaomba Chama pendwe na makini kuimarisha mikakati na kung'oa mizizi ya Ukoo wa Chenge achilia mbali kwa MOMOSE, Cheyo John anaeonekana kiatu kumpwaya 2015.

  Swali, Mzee wa Vijisenti ana ubavu wa Kutosha kuhimili mikikimikiki ya M4C a.k.a People's pooooooooooower!!!, Lakini pia CDM wana ubavu wa dhati kupambana na mzee huyu wa sheria?
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Chadema ni mimi, wewe na yule. Wewe ume-play role gani huko?
   
 3. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,985
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Wakuu nimeipenda hii, ajidhaniaye amesimama aangalie asianguke!!!!!! Mzee wa vijisenti si ni utajili wake na familia yake?????? Makamanda wa CDM zamia Bariadi na Simiyu ukombozi ni sasa!!!VIVA CDM VIVA UKOMBOZI BARIADI?????
   
 4. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Tatizo la Bariadi ni umaskini wa wanyantuzu, wakichinjiwa ng'ombe na pombe za bure ubunge wanampa kama pipi, kumbuka Joseph Ng'wani alikuwa anapewa ubunge kwa kugawa bia wale wa mjini na kule mashambani wanapewa chumvi tu,
   
 5. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama kuna mistake ambayo chadema wanaifanya ni kutofatilia jimbo la Bariadi na hasa lile la mjini(chenge). Kimsingi hakuna watu wapenda mageuzi kama Bariadi. Tukumbuke jimbo hili na hata halmashauri ilikuwa ikiongozwa na UDP kwa muda mrefu. UDP ni chama ambacho hakina nguvu tena Bariadi na kinadharaulika na kila mtu ispokuwa labda mwasisi wake(Cheyo).Chenge hana uwezo wa kupambana na chadema ni mtu mwepesi sana maana 2010 alipambana na mtu dhaifu amabaye alikuwa mbunge kwa miaka 10 na watu wakamchoka lakini alirudi akagombea tena na watu walimpa kura wengi tu kwa sababu hawaipendi ccm.

  Chenge kinachomweka bariadi ni RUSHWA na ushirikiano na matajiri wa pale bariadi ambao ni wafuasi wa mafisadi. Matajiri wa bariadi ambao wote hawakumaliza hata darasa la saba ndiyo wanaowachagulia wana Bariadi mgombea siku hizi. Kwa kuwa wanafanya biashara kwa kushirikiana na mafisadi wengi wao wako magambani.

  Dawa ya Bariadi ni mikutano ya hadhara maana watu wabariadi wanapenda mtu anayeweza kuongea jukwaaani basi. Rushwa wanaweza kuchukua lakini siku zote wanachagua mtu mwenye mvuto. Cheyo huchaguliwa kwa sababu anaweza kutema vijembe majukwaani wakati wa kampeni.Kijana yule wa ccm 2010 alihonga sana lakini akapigwa chini kwa sababu hakuwa na uwezo jukwaaani.

  Bariadi inahitaji mtu wa aina ya Vincent Nyerere maana wasukuma ni watu wa utani sana. Ukiwa serious kama alivyo chenge hupati kura kwa wasukuma ni lazima uwe mtu wa vijembe na mvuto. Chenge hupata kura kwa sababu ya udhaifu wa wapinzani wake ila yeye hawezi kabisa kuongea jukwaaani ispokuwa mke wake ndiye huwa anamwokoa kwa kuhutubia na kugawa rushwa.

  Chadema lazima wajuwe kuwa Bariadi ni wilaya yenye watu wengi sana katika kanda ya ziwa kuikosa ni kupoteza kura nyingi sana.
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe ila kwenye red ni Edward Ng'wani sio Joseph Ng'wani. Wanyantuzu ni watu wa misifa i mean kutambiana na wanahusudu sana watu wenye pesa waoga wa polisi kama nini. Chenge na Cheyo wanashinda kwa sababu wanafikiri Cheyo ni tajiri anaweza kuwasaidia wakiwa na shida, Chenge wanamuogopa kwa vile wanadhani ni mtu mkubwa sana serikalini. Nakumbuka enzi za Edward Ng'wani wakati wa uchaguzi alikuwa anakwenda kwenye vilabu vya pombe za kienyeji akifika pale ananunua pombe yote na kuwagawia bure unategemea nini. CDM kuingia kule kunahitaji kazi ya ziada inabidi wawekeze haswa, siasa za Bariadi nazijua sana.
   
 7. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180


  Kama ni hivyo basi ntamtuma NYANI NGABU, (Banned)
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  huo mkoa naomba sna tujitahidi maana kweli cdm hatujajipanga kwa kuchukua majimbo hayo tuanze sasa maana watu wakule ni waelewa si kama Morogoro na pwani
   
 9. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Asante kwa kunirekebisha kwa hilo jina, Kidogo nakubaliana na wewe kwa miaka ileeeee ya kwetu lakini sio hivi sasa na ukimsoma vizuri Ngonini hapo juu unaweza pata picha halisi ambayo ni recent na haijachakachuliwa, najua wanyantuzu wa leo hii wakimpata mwenzao anayejua kuupepeta vizuri tu bila pesa basi watamchagua, uchaguzi wa 2010 kuna jamaa yetu wa huko tulimbembeleza sana akasimamishe ndevu na Chenge lakini bahati mbaya akahofia pesa ya Chenge
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ngonini

  Naona kama unaijua vizuri Bariadi, kweli kabisa watu wa Bariadi wanapenda utani utani wewe wapelekee 'mbina' utaona watakavyojazana hiyo strategy ndiyo huwa anaitumia sana Cheyo. Kama unavyosema Chenge hana uwezo wa jukwaani ila anapesa ya kuhonga, nasikia hata uchaguzi uliopita mdogo wake Cheyo Issac alishinda, usiku huo huo Chenge akamtangazia dau la 160+milion cash matokeo yakapinduliwa, kesho yake ndio tukasikia watu wamekatana mapanga kupinga matokeo. Angalia hapo chini kura zilizoharibika ndio utakubaliana na mimi ninachokiongea, hao ni wanyantuzu bana achana na pesa.

  [TABLE="class: arc90_altrows-Blue"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B3D5E6, colspan: 4"]SHINYANGA

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B3D5E6, colspan: 4"]WILAYA YA BARIADI
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B3D5E6, colspan: 4"]BARIADI MAGHARIBI
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%, bgcolor: #B3D5E6"]Candidate
  [/TD]
  [TD="width: 20%, bgcolor: #B3D5E6, align: center"]
  Political Party
  [/TD]
  [TD="width: 20%, bgcolor: #B3D5E6, align: center"]
  Number of Votes
  [/TD]
  [TD="width: 15%, bgcolor: #B3D5E6, align: center"]
  Percentage Votes
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"] CHENGE ANDREW JOHN
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]
  CCM
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]50,107
  [/TD]
  [TD="width: 15%"]30
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"] CHEYO ISAAC MANJOMBA
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]
  UDP
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]34,298
  [/TD]
  [TD="width: 15%"]20.54
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"] MAKONO THOMAS ZACHARIA
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]
  CHADEMA
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]3,372
  [/TD]
  [TD="width: 15%"]2.02
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"] NDULU SHEMU SALUMU
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]
  CUF
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]1,055
  [/TD]
  [TD="width: 15%"]0.63
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"][/TD]
  [TD="width: 20%"][/TD]
  [TD="width: 5%"][/TD]
  [TD="width: 15%"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 10%"]SPOILT VOTES
  [/TD]
  [TD="width: 20%"][/TD]
  [TD="width: 20%"]78,171
  [/TD]
  [TD="width: 15%"] 46.81
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 10%"]TOTALS
  [/TD]
  [TD="width: 20%"][/TD]
  [TD="width: 20%"] 167,003
  [/TD]
  [TD="width: 15%"] 100
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 11. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Ama kweli bariadi: Chenge na mkewe magaidi wanaingiza sumu za kupuliza (spray) na wanapiga watu balaa, siasa kwao ni vita. Cheyo pesa kwishnei na siasa zake sasa pro CCM lakini mchawi, na pia yuko tayari kuua...uliza Lagangabilili walikufa watu wangapi hadi CCM wakachukua kata. Bariadi a.k.a Simiyu inahitaji wana mageuzi wa kweli na waanze campaign leo wakisubiri 2014 wameliwa..wakati wa mavuno hakuna mnyantuzu anasikia siasa ni pesa tu. Matajiri vijana wa CCM pale balaa wana viwanda na malori ya kina riz1 ndiyo wanatumiwa kuhonga pesa
   
 12. N

  NGENDA NGOLOMA Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimezaliwa Bariadi na naifahamu sana Bariadi na nimeshiriki sana katika harakati mbalimbali za kujenga CDM. Chadema walifanya makosa makubwa kumchagua Kijana wa Udom ambaye hakuwa na Mvuto na uzoefu katika siasa. Bw. Makono Ezekia ambaye hata Kampeini hakupiga.
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Umeonyesha upumbavu wa hali ya juu sana hebu nitajie kati ya majibo tiifu kwa upinzania hapa Tanganyika kama siyo pamoja na bariadi nilikuwepo kampeni za mwaka 1995 anajua Edward alivyokuwa anazomewa na wasukuma na bariadi Chadema inanguvu sana pamoja na kwamba kule ndiyo makao makuu ya UDP na hakuna haja ya kuweka nguvu nyingi kwenye jimbo linalo tawaliwa na upinzani tutakuwa hatuna tofauti na James Mbati labda kule kwa Vijisent...
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Yeah huu mkoa ni mpya kama unavyosema na ni rahisi kuwaelewesha watu wa Simiyu kuliko watu wa Morogoro au Pwani. Kinachotakiwa CDM waangalie ni wapi pa ku-invest, wahangaike na mikoa ambayo hawana uhakika wa kupata kura nyingi au waka-invest mkoa mpya wa Simiyu is up to them.

  Navyojua Simiyu ni mkoa wa wapinzani wilaya ya Meatu kule tuna mbunge wa CDM Opulukwa, Maswa imeletwa Simiyu tuna wabunge wawili wa CDM akiwemo Shibuda, Bariadi Mash. tuna mbunge wa UDP Cheyo Momose. Kumbuka vile vile Halmashauri ya Bariadi ni ya kwanza kuongozwa na upinzani mwaka 1995 ikiwa chini ya UDP. Kwenye miaka ya 2000, CUF walitaka kuingia huko (kanda ya Ziwa) kwa gia ya bei ya pamba lakini wakashindwa, sasa watu mategemeo yao ni kwa CDM. So, CDM is your choice twende Simiyu kwa nguvu au twende Lindi kwa nguvu, najua tunataka kotekote lakini lazima tuangalie profit in terms of outcomes.
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hapana Crashwise, Ngasibara kasema kweli wanyantuzu ni wepesi sana kwa kuhongwa ila si masikini kama alivyosema, hata Cheyo si kwamba anashinda kwa uwezo wake anahonga sana hasa wananzengo na viongozi wa vikundi hasa vya 'mbina'. Ila ninachowapendea watu wa huko wakiamua wameamua ndiyo maana CCM huwa inatumia nguvu sana kuibadilisha Bariadi. Nafikiri CDM ikiwekeza vya kutosha kule Simiyu inaweza kuwa ngome yake kama ilivyo Arusha maana watu wa Arusha na Bariadi (Simiyu) hawapishani sana katika kuhangaikia ridhiki hasa eneo la biashara.
   
 16. N

  NGENDA NGOLOMA Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kupotosha Kuwa Bariadi ni Maskini ni Dhambi kubwa, Ina utajiri wa Kupindukia na wala haitegemei vyanzo vya muda kama Madini ambayo yana ukomo. Na wala watu wa Bariadi si rahisi kama mnavyofikifiria, Natambua kuwa Bariadi ni kitovu cha Mageuzi na ni wilaya chache ambazo zilipokea mageuzi katika miaka ya Mwanzo. Ni mikakakti zaidi inahitajika zaidi na wala si nguvu zaidi kumtoa Chenge, naamini M4C inaweza hasa kamanda LEMA akitia mguu.
   
 17. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hapa kweli kulikuwa na kitu mbaya kabisa haiwezekani nusu ya kura ziliharibika!
  Kama nilivyosema mwanzo bariadi ni rahisi sana kuangukia chadema, ila inahitaji mtu mwenye mvuto kama Lema,Vicent Nyerere, Dr. slaaa, Zitto, Mbowe na wengine kupiga kambi pale bariadi mjini tu kwanza japo kwa siku chache. Pia ni lazima chadema waende kipindi cha mavuno ambapo watu wengi wako kwenye mapumuziko ila ukienda wakati wa kilimo hutawapata maana jamaa wale hawanamchezo na kazi. Kipindi hiki kuna wimbi la vijana ambao wanaunga sana mkono upinzani. Nilipata habari wakati wa uchaguzi vijana walifanya kazi kubwa sana kuwapitisha madiwani vijana wenzao. Walikuwa wanafanya maandamano ya kijiji hadi kijiji wakihamsisha kuwapigia kura vijana UDP na walifanikiwa sana.

  Kwa ufupi vijana wa bariadi hawana chama kwa sasa maana UDP ndo inakufa na CCM ndo hawitaki kabisa. Chadema ikienda bariadi ninaimani Vjisenti hatakubali hata kujaribu kugombea tena 2015 maana mziki wake hatauweza.
  Chadema has a good chance to takeover bila shaka yoyote. Sumu mbaya ni wale mafisadi wafanyabiashara wanaofadhiriwa na akina riz1 japo ni watu mbumbu hata hawakumaliza darasa la saba.
   
Loading...