Uchaguzi 2020 CHADEMA karata wamezichanga vizuri

Golobeja

Member
Aug 20, 2017
93
98
Kwa jinsi nilivyomsikiliza mh Nyalandu Leo ni dhahiri kuwa ndiyo mgombea rasmi Kwa tiketi ya CHADEMA.

Hawa jamaa wametumia mbinu hatari za kijasusi sijui kama hapa hakuna mkono wa Yerico Nyerere na kama yupo basi hii strategy ni hatari sana!Achana na mbwembwe za Mh Lissu kuchangisha fedha hii bado ni mbinu kisha nisikize Mimi.

CHADEMA walishajua mbinu za CCM za kutumia propaganda kumchafua mgombea wa upinzani basi wakajidhatiti kwa kuficha dume Mh Nyalandu Kwa kipindi chote amekua kimya kama vile hayupo!

Upande wa pili ukijua Lissu ndiye na wao wakimpamba kwa Kwa sifa kedekede kama mbeba maono hafi! Mungu bado anakazi naye! Vijana wa Lumumba wakakomaa kuleta propaganda za anatumiwa na mabeberu;ana support ushoga na anapinga kila kitu sasa tutarajie kusikia huyu aliuza Twiga wetu!

Swali litakua ni je mahakama ya mafisadi ilishindwa kumfunga muda wote huo? Alishirikiana na Nani?

Kama zilivyo propaganda za faru John zilivyozimwa na kumfananisha mtu na Yesu tutalajie nini?
 
Hakuna wa kusimama na magufuli akamtingisha kati hao wote, watagaragazwa vibaya sana.kifupi chadema hakuna mshindani wa magufuli Ni wasindikizaji tu
 
Back
Top Bottom