CHADEMA, kama Pinda analipwa per diem ni wizi mkubwa zaidi

Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ana nyumba ya serikali Dodoma, askari, wafanyakazi wawili wa ndani, dereva na VX la serikali na GX la ubunge, na hapa napo tuulize.

Zito ameleta matatizo makubwa sana, naona sasa watu mnatoka usingizini.

Nadhani hizi kelele zingeanzia wao kujivua gamba kwa kuyakataa hayo matunizi ya mavx na kuwekewa walinzi ili hizo pesa ziokolewe na kuelekezwa kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo sio wanapiga kelele shs 70,000 za posho na kujakumbatia mavx v8 ya mil 200
 
Mbona hata shamba analo Dodoma,si tulionyeshwa kwenye gazeti akikagua shamba lake,wizi mtupu,hapaswi kupata posho akiwa nyumbani kwake ,kwani ofisi yake si iko Dodoma au huwa analipwa siku zote akiwa Dr es Salaam kwa vile ofisi yake iko Dodoma,kweli Tanzania shamba la bibi

labda analipwa na life/living allowance! Jaman ata home? Hawana jema hawa!
 
Lakini si lazima kuwe na mahali pa kuanzia. Tunaanzia kwa Wabunge. Huo wizi kwa njia ya posho ukomeshwe mara moja ili wawe na ujasiri wa kufuatilia ufisadi kwa ujasiri. Watoe boriti kwenye macho kabla ya kuwaambia wengine kuwa wana boriti.
 
Wizi ni dhambi, na hakuna dhambi iliyo ndogo. Wote ni wezi na hawafai kuwa Viongozi. Tuwaondoe mara moja
 
Ndio maana mkahimizwa msome ili na nyie muwe na maisha mazuri, anyway hivi unataka waziri mfano sitta asafiri kwenda jimboni kwake kwa gari halafu kazi nyingine kwa mujibu wa diary yake zisimame mpaka arudi kutoka jimboni? anafanya hivyo kwa kuokoa muda anapoenda jimboni anafanya mambo yake anamaliza anarudi ofisini kuwajibika. Jaribu kufikiria kabla ya kupost mkuu.
Huko jimboni hakuna magari ya kutumia? Yaani anatoka Dar kwa ndege, gari imfuate jimboni ikiwa na dereva tu. Akimaliza kazi jimboni anapanda ndege kurudi Dar na gari inarudi na dereva. Huu ni ubadhirifu!!
 
Ndio maana mkahimizwa msome ili na nyie muwe na maisha mazuri, anyway hivi unataka waziri mfano sitta asafiri kwenda jimboni kwake kwa gari halafu kazi nyingine kwa mujibu wa diary yake zisimame mpaka arudi kutoka jimboni? anafanya hivyo kwa kuokoa muda anapoenda jimboni anafanya mambo yake anamaliza anarudi ofisini kuwajibika. Jaribu kufikiria kabla ya kupost mkuu.

Mkuu ni hivi kama Six alichaguliwa kuwa mbunge si inamaana anakopeshwa gari la ubunge?, si litakuwa jimboni kwake? sasa kwa nini atoke na gari lauwaziri dar mpaka urambo? kwa nini asipande hiyo ndege na apokelewe na dereva wa halmashauri na kutumia gari yake ya ubunge then akirudi dar ana kuta gari yake ya uwaziri inampokea air port, why kuunguza mafuta go and return?

huu mjadala wa posho ni mzuri sana na umetuonyesha ni kwa nini matumizi ya kawaida yanakuwa ya juu kuliko matumizi ya miradi ya maendeleo nina uhakika tukilitazama vizuri hili jambo we will save more than 35% of normal expenses, matumizi yaliyo mengi hayana justification ni ulaji tu usiokuwa wa maana, na hapa ndipo utagundua watu wakipoteza ukubwa tu wanachizi kabisa nenda kawaone walioukosa kwa sasa hata sura zimeanza kufubaa.

Chadema kaza buti kwa hili.

Kuhusu Mbowe, kama na yeye anapokea posho mara mbili fagio hili halichagui ila naamini hatafanya hayo madudu na ndio maana chama chake kimeibua uozo mkubwa sana unafantwa na serikali.

nilikuwa nashangaa kwa nini mtu awe tayari kutumia mamilioni ya shilingi ili kupata ubunge sasa naelewa mantiki yake ni nini.

Kwa matumizi haya ya serikali ya ccm, naamini Dr Phd Wilbrod Slaa yupo sahihi na tutaendelea kuprove kwamba alitwambia ukweli, Elimu Bure inawezekana, Tiba Bure inawezekana na kuimarisha uchumi wa Taifa tunaweza.

Mungu ibariki Tanzania, Tubariki Watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii.
 
Ndio maana mkahimizwa msome ili na nyie muwe na maisha mazuri, anyway hivi unataka waziri mfano sitta asafiri kwenda jimboni kwake kwa gari halafu kazi nyingine kwa mujibu wa diary yake zisimame mpaka arudi kutoka jimboni? anafanya hivyo kwa kuokoa muda anapoenda jimboni anafanya mambo yake anamaliza anarudi ofisini kuwajibika. Jaribu kufikiria kabla ya kupost mkuu.
. Hata kama kuna haraka, je kuna umhimu wa kutumia gari ya serikali katika mazingira hayo? Kwa nini dereva wake wa Serikali asimpeleke airport then huko anakoenda akapokelewa na gari lake la ubunge na baada ya shughuli za jimboni awasiliane na ofisi yake ili akapokelewe?
 
Acheni unoko wa kijinga! Kila mbuzi ale kutokana na urefu wa kamba yake
 
Ndio maana mkahimizwa msome ili na nyie muwe na maisha mazuri, anyway hivi unataka waziri mfano sitta asafiri kwenda jimboni kwake kwa gari halafu kazi nyingine kwa mujibu wa diary yake zisimame mpaka arudi kutoka jimboni? anafanya hivyo kwa kuokoa muda anapoenda jimboni anafanya mambo yake anamaliza anarudi ofisini kuwajibika. Jaribu kufikiria kabla ya kupost mkuu.
daaa samahani ila wewe kweli shosti hata kama si shosti unaakili kama zao!
 
Hata makinda anakaa nyumba ya speaker Dodoma hastahili kupewa per diem.
 
Back
Top Bottom