The Fixer,
..chama cha siasa kinapaswa kuendeshwa kwa MICHANGO ya wanachama na mashabiki, pamoja na RUZUKU toka serikalini.
..kwa mtizamo wangu BUNGE linapaswa kupitisha sheria itakayopiga marufuku vyama vya siasa kufungua makampuni ya kibiashara.
..mazingira unayopendekeza yanaweza kuleta migogoro haswa pale serikali itakapoanza kuyasumbua makampuni ya biashara ya vyama vya upinzani, au itakapokuwa inapendelea makampuni ya biashara ya chama tawala.
cc:
Mchambuzi,
Nguruvi3,
Jasusi,
EMT,
chama,
NasDaz,
Mdondoaji
JokaKuu,
Uliyosema wewe na aliyosema Braza
chama yote ni kweli kabisa.....hivyo ndivyo siasa inapaswa kuendeshwa! Hata hivyo, mimi lazima nikiri UDHAIFU wangu mmoja! Udhaifu huu, nikiri wazi ninao....nazani siku nikiwa Rais, nitalazima kupata washauri wa dizani yenu!! I don't know why, lakini mara nyingi najikuta nikiwa more commercial/economic oriented kuliko haya mambo mengine....nafahamu ni udhaifu, but that is how i am! Kile kijiji cha makumbusho, mie najionea ni upotezaji wa resources tu; for strategic site kama ile sioni chochote kinachofaa pale zaidi ya commercial center provided hakuna ufisadi utakaofanyika....that's how I am!! Suala la kutaka kufanyika investment eneo la Oyster bay police naliunga mkono kwa 101% coz' sioni rationale ya eneo kama lile kuwa na vibanda vya paa mbili visivyo na kichwa wala miguu ambavyo vimebatizwa na kuitwa eti nyumba za polisi!! TRUST me, yale maofsi ya serikali yaliyojazana kati kati ya jiji naona yanaziba nafasi ya watu kufanya biashara....leo hii nikiambiwa ni wizara gani ya awali ambayo ningependa ihame, basi wala sitasita kuitaja mambo ya ndani....ile ni commercial area bana, waende charambe huko kuna maeneo kibao! Kuna majengo ya ajabu ajabu pale mtaa wa samora, wenyewe wanadai yanaachwa kwa ajili ya historia, kwangu najionea upuuzi mtupu! Ni wazungu wangapi wanatoka Ulaya/America kuja kuangalia majengo ya kale mtaa wa samora? Nafahamu kwamba ni udhaifu, lakini ndivyo nilivyo!!!
So, nikirudi kwenye mada, naungana na
The Fixer! Ingawaje ni kweli kwamba uhai wa chama unategemea michango ya wanachama, lakini bado naamini ni muhimu sana kwa chama kuwa na uwezo wake chenyewe kiuchumi! Watanzania wengi ni maskini hivyo badala ya vyama kutegemea wanachama kwa maana ya wanachama, kinyume chake wanategemea watu wanaojiita wanachama kuliko wanachama wenyewe! Kwa kiasi kikubwa vyama vyetu havitegemei michango ya wanachama bali vinategemea michango ya wafadhili!! Hii ni hatari kwa siasa zetu kuliko hatari inayoweza kutokana na vyama kuwa na vyanzo yake vya mapato!! Wengi wa watu hawa wanaojiita wanachama huwa na malengo yao binafsi lakini hatuna namna ya kuikataa michango yao coz' vyama vyetu havina namna nyingine!! Huwezi kuendesha competitive politics kwa kutegemea michango ya wafadhili(narudia, hakuna michango ya wanachama, kilichopo ni michango ya wafadhili) na viruzuku vya hapa na pale matokeo yake ndo haya unaamua kukaribisha mtu yeyote ambae unafahamu akigombea kwa chama chako anaweza kushinda ubunge na hivyo kuongeza ruzuku ya chama!
Provided ni legal investments, naunga mkono! Tena si ajabu uroho wa wanasiasa wetu tunaweza kuanza kuuona huko huko kabla hawajapata madaraka ya kuongoza taifa! Kama kuna watu walianza kusahau maneno ya Mwalimu Nyerere kuhusu Lowasa. waliweza kukumbuka tena kuhusu Lowasa hasa ni nani wakati CCM wanafanya machakato wa ujenzi pale Umoja wa Vijana!! Kabla ya kupewa wizara ya fedha, tayari Nchembe aame-shaprove kwamba yeye ni masuala ya kiuchumi si yamemzidi kimo ingawaje ana shahada mzuri ya uchumi! Haya yote tusingeyafahamu kama si kupewa cheo cha Mweka Hazina wa CCM ambako alifeli vibaya sana!! SUKITA ya CCM imekufa, lakini ukichunguza unakura wale wale walioiua SUKITA bado hadi leo ni wanasiasa wenye kutia shaka! Ninachotaka kusema ni kwamba, kumbe CCM ingekuwa wanachukua somo kupitia kwenye miradi yake, si ajabu wengi ambao wanaifisidi serikali wasingepata nafasi hiyo kwani tayari wao ni nani hasa walishaanza kujipambanua kwenye miradi ya chama!
Naunga mkono hoja ya
The Fixer ili mradi tu biashara zenyewe zisiwe sawa na moja aliyoipendekeza mtoa mada; kuwa na kampuni ya ulinzi.....NO, hiyo ni hatari kwa chama cha siasa; iwe CCM au CHADEMA! Hata hivyo, hapa tunahitaji uwekezaji na sio uchuuzi! Hapa hatuhitaji biashara za kuagiza pampers kutoka China! BIG UP CCM, endeleeni hivyo ingawaje mlitakiwa muwe thousands of miles kutoka mlipo. CCM kama ingekuwa wameji-establish vizuri commercially, leo hii si ajabu wangekuwa ni moja ya largest money makers! Wangekuwa na uwezo wa kuisaidia hata serikali yake kwa mikopo yenye riba nafuu! Wangekuwa na uwezo wa kutoa ruzuku za maendeleo kwenye majimbo yao!
NAUNGA MKONO HOJA!