CHADEMA jijengeni kiuchumi !

CHADEMA jijengeni kiuchumi !

The Fixer

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
1,365
Reaction score
599
Wana JF,
Habari za jioni !

Kwa bahati mbaya sana mimi sio mfuasi wa chama chochoote cha siasa kwa hiyo haya nnayoyaandika ni mawazo yangu tu binafsi yasiyokuwa na " interest " kokoote katika vyama hivi vikubwa Tanzania

Leo tumeshuhudia ufunguzi wa kiwanda kikubwa cha Cement huko Mtwara kama ambavyo TBC walionyesha mchakato wake na Waziri mkuu Pinda akiwakilisha kutoka pande zile, huu ni mkakati wa siku nyingi wa CCM ingawa ulichelewa sanaa kwani CCM kama chama kongwe kilitakiwa kijijenge kiuchumi miaka mingi sana iliyopita kutokana na fursa nyingi za uwekezaji zilizopo hapa nchini ni bahata mbaya tu CCM wako Wachumi wakubwa lakini ni wachumi wa vyeti na sio / hakuna uhalisia katika kuonyesha juhudi hizo

•CCM;
¤ Wamechelewa sana kujenga vitega uchumi kama " Shopping mall " katika miji mikubwa

¤ Wamechelewa kuwekeza katika bahari na maziwa makubwa

¤ Wamechelewa sana kuwakeza katika machimbo ya madini, mafuta & gesi

¤ Wamechelewa sana kuanzisha hata Mabenki ya kibiashara kwa wakati

¤ Wamechelewa sana kuanzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara

Sasa kwakuwa mahasimu wao kwenye Siasa wanaowanyima usingizi ni CHADEMA na wanatakiwa kuwa na uchumi mzuri wao kama chama ( CHADEMA ) ili wawe na uwezo wa kuwafikia wananchi wanaotaka mabadiliko katika mfumo huu wa CCM wa kuendesha nchi uliogubikwa na UFISADI wa kila aina na kwakuwa ruzuku peke yake haiwezi kutosheleza mahitaji haya ndio maana kwenye mikutano mingi wamekuwa na watu wa kutembeza bakuli ili kupata nguvu ya kuwafikia watanzania wanaotaka mabadiliko na kuuza sera zao huko basi huu sasa ndio wakati na wao WAWEKEZE KATIKA BIASHARA KUBWA !

Mambo ya kuwalalamikia CCM na Bw Dangote wao yamepitwa na wakati, CHADEMA wanatakiwa kuja na mpango kazi wa namna ya kuwa na HQ yenye kukidhi mahitaji na yenye heshima kwa maana halisi ya Makao Makuu ya Chama kikuu cha Upinzani kuwe na jengo la kisasa lenye parking ya kutosha na kumbi kubwa za mikutanao hata minne under one roof.

CHADEMA na wao watafute mwekezaji watakae ingia nae ubia kupitia kampuni yao wao kama Chama . Mwekezaji huyo awe wa mafuta ama hata gesi na waende kufanya survey mikoa ya Tanga na hata Ziwa Victoria waone namna watakavyopata chanzo cha mafuta na gesi kwa maana kazi ya ukombozi ni kubwa na inahitaji uchumi mkubwa sana

• Sifahamu kwasasa kama CHADEMA wanampango wowoote wa kuwa hata na TV/ RADIO stations kwani TBC ama Tv stations zingine sio za kutegemea sanaa kutoa coverage katika mikutano yao mbalimbali na hasa ile ya M4C na ile mikubwa ya kampeni, habari hizi za ukombozi ( kama utakuwa ni ukombozi wa kweli ) basi ziwe rahisi sana kuwafikia watu wengi sana na kwa wakati

• Sifahamu kwasasa kama WABUNGE wa CHADEMA wanajibana kiasi gani kukijenga chama na ruzuku za chama kama chama katika kujenga walao MAKAO MAKUU yenye nafasi na sio ile iliyojificha pale Kinondoni na kupata uwezo wa kuwalipa Makamanda wengine watakao fanya kazi za kawaida za kila siku katika Makao Makuu zao za mikoani na wilayani hizi habari za kuwa wadau / makamanda wafanye kazi kwa kujitolea kwa kuwa chama bado ni kichanga zimepitwa na wakati, mtu hawezi kuacha kazi zake na kuanza kukitumikia chama full time bila ya kuwa na ugali wa watoto nyumbani na hii pia itachangia kuwa na uwezo kifedha kama Taasisi na kuondoa zile njaa za kukubali kuhongwa na CCM ili kubadili matokeo katika chaguzi mbalimbali kwani baadhi ya maeneo CCM wamepita kwasababu ya njaa za wana CHADEMA wengi sanaaa

Haya ni mawazo yangu tu wana JF yanaweza kuwa yakijinga vile vile maana mie sio malaika, CHADEMA inahitaji nguvu kubwa sana kiuchumi kama vile CCM inavyojitahidi kujikuza kiuchumi ili kushinda katika chaguzi zilizombele yao na hii itakuwa ni njia nyingine ya kukuza ajira badala ya kusubiri Serikali kuja kuyatenda haya yoote !

•CHADEMA;

¤ Wana mpango wowoote wa kujikuza / kujijenga kiuchumi hasa katika hizi biashara kubwa kubwa ?

¤ Kwani kuna dhambi kwa chama kama taasisi kujijenga kiuchumi ?

¤ Wana mpango wowoote wa kutafuta wawekezaji kwenda kujenga kiwanda cha kusindika matunda katika ukanda huu wa Tanga ?

Badala ya kuwaona CCM kama watafuna nchi katika miradi yao mbalimbali hadi ya " parking " na wao watafute namna ya kujijenga kiuchumi na kuwa taasisi yenye nguvu kiuchumi maana naamini kuwa SIASA & BIASHARA bado havijawa vitu haramu hapa Tanzania kwenda pamoja hasa kwa taasisi zenye dhamana ya kuendesha vitu hivi.

Fursa zipo tele tatizo ni mtaji.... Tutafute mitaji na tuwekeze badala ya kunyoosheana vidole ! CHADEMA wanaweza pia kuwa na makampuni ya Ulinzi ili makamanda wenye uchungu na nchi walinde rasilimali zetu zinaibwa kwaushirika wa CCM

Nawasilishaa !

The Fixer,

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wana JF,
Fursa zipo tele tatizo ni mtaji.... Tutafute mitaji na tuwekeze badala ya kunyoosheana vidole ! CHADEMA wanaweza pia kuwa na makampuni ya Ulinzi ili makamanda wenye uchungu na nchi walinde rasilimali zetu zinaibwa kwaushirika wa CCM

Nawasilishaa !

The Fixer,

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Ndugu yangu hapo nilipo bold naona ulitakii mema taifa letu kuhusu ujambazi wa kutumia silaha na wizi wa magari.
 
We una mawazo mazuri ila bahati mbaya sana SLAA kakifanya VICOBA badala ya chama cha siasa. Akitaka hela anajikopesha atakavyo.
 
chadema jengeni team yenye watu wenye busara na siyo tu kila mtu anayefikiri anaweza kuwa mbunge kwa umaarufu wake anakimbilia chadema, mbona hawaendi ccm? mtabaki mnalalamika miaka yote kumbe mna wapiga kelele vijana wengi wasiojua hata kupiga kura.
 
Ndugu yangu hapo nilipo bold naona ulitakii mema taifa letu kuhusu ujambazi wa kutumia silaha na wizi wa magari.

ha! ha! ha! ha! Mkuu mkorofi kweli. Nasikia eti siku hizi wezi wa magari wanabaka vidada vya watu.
 
Ndugu yangu hapo nilipo bold naona ulitakii mema taifa letu kuhusu ujambazi wa kutumia silaha na wizi wa magari.

Mkuu Ritz,
Hawa jamaa kama wangekuwa na Ulinzi pale KIA sidhani kama wale Twiga wangepanda ndege hivi hivi....bila hata ya kuulizwa pasi ya kusafiria !

Hata yale malori yaliyosheheni Wanyama wetu yasingevuka vizingati vyoote na kuingia KIA Mkuu...
 
chadema jengeni team yenye watu wenye busara na siyo tu kila mtu anayefikiri anaweza kuwa mbunge kwa umaarufu wake anakimbilia chadema, mbona hawaendi ccm? mtabaki mnalalamika miaka yote kumbe mna wapiga kelele vijana wengi wasiojua hata kupiga kura.

Hilo nalo nenooo !
 
mkuu mieifurahia hii Post yako- very positive, yaani hata unapochukua nchi unakuwa na ''reference on show'' la sivyo itaendelea kuwa theoretical inapendeza lkn kikazi zaidi........utamalizia.
 
Mkuu,
Ningefurahi sana kuona Tanzania yenye ushindani kama huu wa kiuchumi kwani sio dhambi kwa chama / taasisi yoyoote kujiwekeza kwenye kukuza uchumi...sio dhambi na hii ndio itakuwa chanzo cha posho na mambo mengine maana kama mdau analipwa posho ya kujikimu anaweza kuwa mzalendo zaidi kulinda kura za chama lakini njaa...mbaya jamani !
 
Chadema wana uwezo mkubwa sana kiuchumi, ila uchumi huo uko mikononi mwa wachache ambao waliwekeza fedha zao kujenga chama siku za mwanza sasa ni wakati wao wa mavuno ya ruzuku.

Umeshawahi kujiuliza haya:

Nyumba waliyopanga Chadema pale Kinondoni ni ya nanai na wanalipa kiasi gani kwa mwezi?

Tenda ya kununua magari ya M4C alipewa nani na kwa vigezo gani?

Tenda nyingine mbalimbali za chadema zinatolewa kwa nani na kwa vigezo gani?

Kitengo cha fedha kinasimamiwa na nani?
 
Chadema wana uwezo mkubwa sana kiuchumi, ila uchumi huo uko mikononi mwa wachache ambao waliwekeza fedha zao kujenga chama siku za mwanza sasa ni wakati wao wa mavuno ya ruzuku.

Umeshawahi kujiuliza haya:

Nyumba waliyopanga Chadema pale Kinondoni ni ya nanai na wanalipa kiasi gani kwa mwezi?

Tenda ya kununua magari ya M4C alipewa nani na kwa vigezo gani?

Tenda nyingine mbalimbali za chadema zinatolewa kwa nani na kwa vigezo gani?

Kitengo cha fedha kinasimamiwa na nani?

Mkuu,
Wadau wachache hao unaowasema ilikuwa ni lazima kuwekeza katika Chama ili kiwe na uwezo wa kufika hapo kilipo lakini kuendelea na mtindo huo wa ujima wa kutokuwa na uwazi katika masuala ya UCHUMI na katika kazi kubwa ya kukijenga chama hasa kipindi hiki ni hatari zaidi sanaaa....
 
The Fixer,

..chama cha siasa kinapaswa kuendeshwa kwa MICHANGO ya wanachama na mashabiki, pamoja na RUZUKU toka serikalini.

..kwa mtizamo wangu BUNGE linapaswa kupitisha sheria itakayopiga marufuku vyama vya siasa kufungua makampuni ya kibiashara.

..mazingira unayopendekeza yanaweza kuleta migogoro haswa pale serikali itakapoanza kuyasumbua makampuni ya biashara ya vyama vya upinzani, au itakapokuwa inapendelea makampuni ya biashara ya chama tawala.

cc: Mchambuzi, Nguruvi3, Jasusi, EMT, chama, NasDaz, Mdondoaji
 
Last edited by a moderator:
hii ushauri wako na utaangaliwa na kuchambuliwa na viongozi sikivu wa cdm na wapenzi wa chama wote asante sana na karibu uchukue kadi yako kinondoni.
 
Mkuu The Fixer
Biashara kuu ya chama cha siasa ni kueneza sera na kuzitetea; hili la vyama vya siasa kujikita kwenye biashara sikubaliani nalo serikali inatakiwa iliweke wazi ili kulinda ETHICS; hivi itokee tenda ya kusafisha ikulu makampuni yaliyo chini CCM yawemo kwenye kugombea tenda hiyo kweli yale yaliyo chini ya Chadema na CUF yatashinda? Hapa lazima tuelezane ukweli; vyama vinaweza kuruhusiwa kuwa na vitega uchumi kama majengo lakini lazima iwepo sheria za kuvinabana tunaweza tukajikuta kuna CCM city; Chadema city na CUF city; sijaona mantiki ya vyama vya siasa kuruhusiwa kujihusisha na baishara hata kidogo kama kuna mwenye ufafanuzi wa kina na anieleweshe.

Chama
Gongo la mboto DSM
cc JokaKuu
 
Last edited by a moderator:
chama,

..nimelipenda hilo angalizo lako la biashara ya kufanya usafi ikulu.

..hebu fikiria CCM wapo madarakani halafu CUF ndiyo wanatenda ya kufanya usafi ikulu.

..au CDM imeingia madarakani lakini kampuni inayofanya ulinzi ikulu ni ya CCM!!
 
Last edited by a moderator:
Angalizo, vyama vya siasa vipige siasa na si uwekezaji na biashara kuepuka mgongano wa maslahi. Na ndio maana hata hao CCM wanatumia madalali kuendesha rasilimali kwa mfano kuna mzozo wa wafanyabiashara wa kkoo na makontena chama chenu kinamtumia HSC kama agent mkubwa na ukitaka kufanya business pitia kwa hawa jamaa, waliobisha na kuleta much know wanasaga meno kwani ushuru umepigwa mara mbili huku watukufu kodi wanasema wao watalipa kiasi gani lakini wengine hata bei ya mzigo wanapanga TRA.

Please waache wanasiasa wapige siasa tu, uadilifu huo unaosema sio bongo hapa kwa kipindi hiki. Nani atachagua wakurugenzi kwa hizi rough wanasiasa wengi hawana records katika biashara za maana, watatumia msuri kupata faida na matokeo yake wataharibu mazingira ya kufanya biashara na risk ni kubwa pia kama nyumba za wanachama watu wanatia kiberiti sembuse mali.

Mawazo yako mazuri further study is highly recommended.
 
hii ushauri wako na utaangaliwa na kuchambuliwa na viongozi sikivu wa cdm na wapenzi wa chama wote asante sana na karibu uchukue kadi yako kinondoni.

Bily,
Nakushkuru sanaa Mkuu !
Mie napenda zaidi kuwa mpiga kura na wala sio mwanachama wa chama chochoote...

Ahsantee !
 
chama,

..nimelipenda hilo angalizo lako la biashara ya kufanya usafi ikulu.

..hebu fikiria CCM wapo madarakani halafu CUF ndiyo wanatenda ya kufanya usafi ikulu.

..au CDM imeingia madarakani lakini kampuni inayofanya ulinzi ikulu ni ya CCM!!

• Mkuu !
Kama Kampuni ya ulinzi ya CUF & CHADEMA wangekuwepo kwenye viwanja vyetu vya ndege nadhani hata Rasilimali zetu nyingi kama Wanyama pori na Madini yasingetoroshwa nje kiujanja ujanjaa..

Hata zile pembe za ndovu zingekamatwa Dar es salaam Bandarini badala ya Malaysia ama Singapore hukoo...
 
Last edited by a moderator:
• Mkuu !
Kama Kampuni ya ulinzi ya CUF & CHADEMA wangekuwepo kwenye viwanja vyetu vya ndege nadhani hata Rasilimali zetu nyingi kama Wanyama pori na Madini yasingetoroshwa nje kiujanja ujanjaa..

Hata zile pembe za ndovu zingekamatwa Dar es salaam Bandarini badala ya Malaysia ama Singapore hukoo...

Mkuu umepagawa? CEO wa Chadema kapora mke wa mtu itakuwa maliasili zetu?

Chama
gONGO LA MBOTO dsm
 
Back
Top Bottom