Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,091
- 136,650
Nyie CHADEMA sikilizeni....amkeni sasa.
Anzeni kuwa mnafikiria kwa hatua kadhaa mbele.
Hatua zenye manufaa kwa mustakabali wa chama chenu na viongozi wenu.
Hivi nyie mna idara ya usalama kweli? Kama mnayo, iweje suala la ulinzi kwa Tundu Lissu mlikuwa hamjaona umuhimu wake?
Kwa nini Lissu hakuwa na ulinzi imara wa watu wenye silaha za moto?
Kwa kweli hapo mmeudondosha mpira. Na kama mna watu wanaohusika na usalama ndani ya chama chenu basi hamna budi kufanya maamuzi magumu na kuwatimulia mbali.
Haiwezekani kiongozi mkubwa kwenye chama kama Lissu asiwe na usalama wa kueleweka.
Sijui mlikuwa mnaitegemea serikali kwenye hilo!
Kiongozi wa juu tena mwenye mbwembwe na cheche kama Lissu kutembea tembea bila ulinzi wa maana ni upumbavu.
Ni upumbavu kwa sababu tayari yeye atakuwa ni mlengwa wa mashambulizi toka kwa wabaya wake. Anapotembea bila ulinzi anakuwa ni shabaha iliyo rahisi sana kuilenga.
Haiingii akilini kwa nini hadi siku ya lile tukio mlikuwa hamjampatia ulinzi huyo mwanasheria wenu mkuu.
Shame on you.