CHADEMA jiandaeni kisaikolojia kupokea matokeo

brightoscar

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
360
517
Kulingana na kampeni zao nimeona CHADEMA wamekuwa na matumaini makubwa kupata kura nyingi katika uchaguzi huu mkuu. Ila kwa watu wenye upeo na wenye uwezo wa kuona mbali tunajua mgombea wao hatafikisha hata kura milioni 3 akipata sana 2.8 milioni ambapo hatafikia hata nusu ya kura alizopata Lowassa.

CHADEMA ningependa kuwashauri uchaguzi ujao mjifunze kutoka CCM kuandaa wagombea maana wagombea wenu ni yule anayeibuka tu hana maandalizi yeyote hajui kuwaambia Watanzania atawafanyia nini zaidi ya kutafuta sympathy za watu tu.

Hata kama angeshinda hakuna watu wa kutengeneza serikali kutoka CHADEMA hakuna watu wenye sifa hata za kuwa wakuu wa mikoa sembuse kuongoza wizara.

Jamani kuongoza nchi sio kitu cha kubahatisha nchi haiwezi kuongozwa na chama ambacho ofisi zake imepanga mtajengea nchi nini kama kujenga ofisi na ruzuku zote mnazopata mmeshindwa.

Wanachadema wote jiandaeni kisaikolojia kupokea matokeo mgombea wenu hatafikisha hata 20%.
 
Kikubwa tume ijiondoe kwenye wizi wa kukusudia kwa kutoa fomu za matokeo pale pale kwa wakala, na huko Zanzibar wanaopiga kura tarehe 27 wasirudie kupiga kura maana washasema wanawahi ili wakasimamie uchaguzi Sasa nini kitawapeleka Tena tarehe 28? Kuna vitu wanasheria nao wawe wanasimamia kwa kujielewa.
 
Why CHADEMA and not CCM
??
Mzee mbona jibu liko wazi mitaani au unakaa nje ya Tanzania? Watanzania wameamua kumpa kura za kishindo Dkt Magufuli. Survey zote zilizofanywa kisayansi zimethibitisha ushindi wa kati ya 86%-90% kwa JPM. Watanzania wamemkataa mwakilishi mkazi wa Mabeberu. Jumatano weka kura yako kwa JPM maisha yaendelee ukiwa na amani ya roho na upunguze stress wakati matokeo yanatangazwa au jiandae kisaikolojia
 
labda umemkataa wewe mkeo na shemejio
 
Ni kweli wajiandae kisaikolojia... hilo halina shaka... lakini siasa si ofisi ya vioo... na ofisi si maghorofa pekeee...
 
labda umemkataa wewe mkeo na shemejio
Mkuu, JPM tayari anamtaji wa wana CCM milioni 22 na wanafamilia yao nikiwemo mimi. Jumuisha na watanzania wengine wasio na vyama na wengine wa vyama vya upinzani watakaompigia kura. Ni kura za mafuriko mkuu, kama uko upande wa wakala wa mabeberu jiunge nasi tumpe kura JPM au anza kujiandaa kisaikolojia
 
si kweli kwamba miongoni mwa watanzania M55+ eti M22 ni wanachama wa CCM si kweli hata kidogo...
 
Hivi unazani mleta maada CCM ilichokifanya Nini miaka yake yote,zaidi ya kuiba na kujilimbikizia Mali viongozi,ndio maana siasa wameifanya Kama biashara,kwa Nini wanalazimisha kushinda Kila siku,kwa Nini hawataki time huru
 
Kulingana na kampeni zao nimeona Chadema wamekuwa na matumaini makubwa kupata kura nyingi katika uchaguzi huu mkuu. Ila kwa watu wenye upeo na wenye uwezo wa kuona mbali tunajua mgombea wao hatafikisha hata kura milioni 3 akipata sana 2.8 milioni ambapo hatafikia hata nusu ya kura alizopata Lowassa.

Chadema ningependa kuwashauri uchaguzi ujao mjifunze kutoka CCM kuandaa wagombea maana wagombea wenu ni yule anayeibuka tu hana maandalizi yeyote hajui kuwaambia Watanzania atawafanyia nini zaidi ya kutafuta sympathy za watu tu.

Hata kama angeshinda hakuna watu wa kutengeneza serikali kutoka Chadema hakuna watu wenye sifa hata za kuwa wakuu wa mikoa sembuse kuongoza wizara.

Jamani kuongoza nchi sio kitu cha kubahatisha nchi haiwezi kuongozwa na chama ambacho ofisi zake imepanga mtajengea nchi nini kama kujenga ofisi na ruzuku zote mnazopata mmeshindwa.

Wanachadema wote jiandaeni kisaikolojia kupokea matokeo mgombea wenu hatafikisha hata 20%.
Hizo kura za Chadema muwekee magufuli. Maana ukweli ni kwamba Tundu Lissu anaenda kuzoa kura zaidi ya asilimia 65
 
Back
Top Bottom