Chadema itakufa lini ?

Chadema itakufa lini ?

Wakuu asalam Aleykhum , baada ya salamu hizi za upendo nijikite moja kwa moja kwenye hoja yangu

Kumekuwa kuna juhudi kubwa sana zilizo rasmi na zisizo rasmi za kuhakikisha Chadema inakufa , ziko hata juhudi za kishirikina zinazoendeshwa na maofisa na wachovu za kuhakikisha Chadema inakufa , haya yamefanyika kwa kipindi kirefu na yamefanywa wazi wazi na mengine yamefanyika gizani

Binadamu wamenunuliwa na wengine wamejiuza mchana kweupe , utu umewekwa kando unyama umechukua nafasi , wabunge na viongozi wengine wamefungwa jela na wengine kushambuliwa na kuuawa , pamoja na yote haya lakini Chadema haifi wala hata hakuna dalili ya kutundikiwa dripu la D5

Sasa nawauliza wanazuoni , hii Chadema itakufa lini , mbona hakuna hata dalili ya kifo chake , au Mtoa roho yuko likizo ?
Chadema bundi ashasogea kwenye paa lao,nadhani kwa wale wataalamu wa ulozi kama comrade mshana atakuwa ashajua nini maana yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watasubiri sana.CHADEMA ni mpango wa Mungu na ndio chama kitakachoitoa CCM madarakani.Ni swala la muda tu.
 
Chadema bundi ashasogea kwenye paa lao,nadhani kwa wale wataalamu wa ulozi kama comrade mshana atakuwa ashajua nini maana yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena bundi mweuc kukashifu viongozi wa din kunakoongozwa n mch msigwa kileo Lena heche Na wngne kutawagaragaza 2020
Siasa ina mbinu nyingi n mifumo mingi y kupata kura km wanafikiri n maneno ya jukwaani walioongea kwa mwez ndo yaliwapa ushindi wakazane think-tank yao n around draining level

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema ina roho ya paka kama unavyojua Mkuu imetabiriwa vifo miaka mingi iliyopita lakini bado inadunda tu na kumuweka dikteta na vikaragosi vyake roho juu

Kwanza walikuja na uzushi kwamba Chadema ni chama cha Wachagga na Wakristo lakini uzushi wao haukufua dafu kwani Chadema iliendelea kupata umaarufu kila kona ya nchi hata kule kwenye wachagga wachache sana pia wakristo wachache sana.

Kikwete aliwahi kutamka kwenye sherehe za mei mosi kwamba Chadema wanataka kusababisha umwagaji damu nchini lakini hilo pia halikufua dafu

Mfojaji vyeti mwingine mwigulu nchemba akatengeneza sinema UCHWARA dhidi ya Lwakatare ili kuonyesha Chadema ni chama cha magaidi lakini hili nalo halikufua dafu kwani kesi ambayo mwigulu alimbambikia Lwakatare ikapigwa chini mahakamani mara tatu pamoja na ushahidi FAKE wa mwigulu aliodai ungekubalika hadi mbinguni.

Wakaja na mkakati wa kumdhoofisha Mbowe kwenye biashara zake na ukulima kwa kuivunja Bilicana na kung’oa mazao kwenye shamba lake lakini Mwenyekiti pamoja na kujawa na majonzi makubwa ya kuonewa na huyu dikteta dhalimu hakukata tamaa akaendelea kuliongoza jahazi la Chadema kwa umahiri mkubwa sana.

Wakaja na mkakati mwingine wa dikteta na dhalimu kuwanunua Wabunge na Madiwani wa Chadema lakini huu uhuni wao pia ukagonga ukuta kwani idadi ndogo waliyoipata haikuwaridhisha pamoja na kuja na “dirisha dogo la usajili”

Wakaamua kuwabambikia kesi viongozi wote wa juu wa Chadema kwa kuandamana kudai haki yao wakati wa uchaguzi wa madiwani. Kesi ambayo inaendelea kwa miezi kadhaa sasa na ndiyo chanzo cha makamanda Mbowe na Matiko kuwekwa lupango kwa miezi miwili sasa. Hii kesi pia inaweza kuishia kwa viongozi wote katika kesi hii FAKE kufungwa kwa miezi sita au hata zaidi ikiwa ni mkakati wa kuidhoofisha Chadema kuelekea 2020.

Tukumbuke pia kuna viongozi wengi wa Chadema ambao waliwekwa lupango nyakati mbali mbali na wengine kufungwa na wengine kuuwawa. Kuna akina Ben Saanane, Kamanda Mawazo, lijualikali, Sugu, Lissu, Msigwa, Halima Mdee, Esther Bulaya, Heche, Msigwa na wengine chungu nzima.

Tusisahau shambulio la kutaka kumuua Lissu. Pamoja na kumminia risasi 38 lakini Mwenyezi Mungu mkubwa bado yuko hai na akili zake timamu.

Sasa huyo dikteta dhalimu amekuja na muswaada wa vyama vya siasa nia kubwa ni kuhakikisha wanaimaliza kabisa Chadema kupitia kikaragosi kingine cha dikteta wenyewe wanamuita msajili wa vyama vya siasa.

Chadema iko mioyoni mwa Watanzania wengi wenye mapenzi ya kweli na Tanzania na imesambaa nchi nzima na wala si chama cha magaidi, kinachotaka kuleta umwagaji damu nchini au cha Wachagga na wakristo. Chadema ni chama cha WATANZANIA wote bila kujali makabila yao au dini zao.

Mwenyezi Mungu ibariki Chadema [emoji1431][emoji1431][emoji1431]

Alutta continua! CONTINUA! [emoji1365][emoji1365][emoji1365]

[emoji115][emoji122][emoji106][emoji1374] Asante sana BAK!
 
Wanaweza iua CHADEMA lakini hawawezi ua imani na mawazo yao
Wakuu asalam Aleykhum , baada ya salamu hizi za upendo nijikite moja kwa moja kwenye hoja yangu

Kumekuwa kuna juhudi kubwa sana zilizo rasmi na zisizo rasmi za kuhakikisha Chadema inakufa , ziko hata juhudi za kishirikina zinazoendeshwa na maofisa na wachovu za kuhakikisha Chadema inakufa , haya yamefanyika kwa kipindi kirefu na yamefanywa wazi wazi na mengine yamefanyika gizani

Binadamu wamenunuliwa na wengine wamejiuza mchana kweupe , utu umewekwa kando unyama umechukua nafasi , wabunge na viongozi wengine wamefungwa jela na wengine kushambuliwa na kuuawa , pamoja na yote haya lakini Chadema haifi wala hata hakuna dalili ya kutundikiwa dripu la D5

Sasa nawauliza wanazuoni , hii Chadema itakufa lini , mbona hakuna hata dalili ya kifo chake , au Mtoa roho yuko likizo ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la mtu mwenye akili kiduchu anadhani mtu anaposema CHADEMA inakufa anadhani ni kama kifo cha binadamu.

Hata NCCR-Mageuzi ilikuwa ni chama kikuu cha upinzani lakini leo hii inabidi ufanye juhudi kubwa hata kuwapata wanachama wake achilia mbali mashabiki wake.

Kwa kukusaidia naomba uelewe kuwa Watu wanaposema kifo cha CHADEMA wanamaanisha ni kama ilivyo NCCR-Mageuzi ya sasa.

Subiri mazishi yake mwaka 2020 labda ndio utajua maana ya kifo cha CHADEMA.
Karibu tena mkuu
 
Shetani hajawahi kumshinda Mungu
 
Back
Top Bottom