Tatizo la mtu mwenye akili kiduchu anadhani mtu anaposema CHADEMA inakufa anadhani ni kama kifo cha binadamu.
Hata NCCR-Mageuzi ilikuwa ni chama kikuu cha upinzani lakini leo hii inabidi ufanye juhudi kubwa hata kuwapata wanachama wake achilia mbali mashabiki wake.
Kwa kukusaidia naomba uelewe kuwa Watu wanaposema kifo cha CHADEMA wanamaanisha ni kama ilivyo NCCR-Mageuzi ya sasa.
Subiri mazishi yake mwaka 2020 labda ndio utajua maana ya kifo cha CHADEMA.
Tuchukulie kuwa mwaka 2020 Chadema haipati kiti hata kimoja bungeni, (hypothetically), JE, ITAKUWA IMEKUFA?
Katika masuala ya kijamii, kama hili la vyama vya siasa, Chama cha siasa kinaweza kufa, kama ulivyotoa mfano halisi, (tena sahihi, in my view) kuhusu NCCR.
NCCR kilikuwa Chama kilicholeta na kujenga mawazo ya Vyama vingi katika zama ambazo WAZO LA VYAMA VINGI lilikuwa haligongi vichwa vya watu wengi kwa sababu wakati ule, haikuwa rahisi kuwafikia Watanzania wote kutokana na kutokuwepo teknolojia iliyopo hivi sasa.
Mapalala alikuwa akikamatwa na Polisi, zaidi ya robo tatu ya nchi haipati habari.
Leo hii, Mbowe akikamatwa, NCHI NZIMA inapata habari, kiasi kwamba, huzuni ya kukabwa demokrasia inatanda nchi nzima.
Ili Chadema ife, inabidi WATAWALA WA SASA, (read CCM), wawaachie WANANCHI wenyewe waikatae CHADEMA kwenye sanduku la kura.
HOW?
Kwa KUUNDA TUME HURU YA UCHAGUZI.
Swali, je, hili la kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, Watawala wanaliweza?
Wakiliweza, Chadema ikakosa kiti hata kimoja cha Ubunge, basi itakuwa imekufa.
Watawala wakiweza kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, CUF ikakosa kiti hata kimoja cha Baraza la Wawakilishi, basi itakuwa imekufa.
Vinginevyo, kwa kutumia Taasisi hizi zilizopo, CHADEMA na CUF hazitakufa kamwe, hata kama hazitapata kiti cho chote Bungeni na Baraza la Wawakilishi.
And you can see the truth about this in Zanzibar.
CUF is not in the House of Representatives, but is it true that CUF is extinct?