CHADEMA: Israel ituombe radhi

Tanzania bana inatukanwa na Israel, halafu inashambuliana yenyewe kwa yenyewe!
 
fanyeni yote semeni yote tanzania bila israeli haiwezekani nawaambia mtalalamika kutukanwa lakini ukweli unabaki pale pale..tanzania ni kama tripolitania tu[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif],hata m[/FONT]ukiombwa msamahaa hausaidii kitu kama[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif] hata nchi yenyewe haibadiliki kwa kitu chochote me na doa lishaingia.endeleeni kuchagua viongozi bora muone kama heshima haitarudi[/FONT]
 
Israeli walichosema ni ukweli mtupu, Rais wetu kila siku anazunguka akiomba omba misaada (hadi chandarua JK anaomba), kwa misingi hii kwa nini tusitukanwe?

Assume wewe mwana JF kila siku jamaa wako anakuomba msaada (mara pesa ya kula, pesa ya mtoto shule, watoto wangu wanaumwa), mtu wa namna hii utahacha kumzarau?

Naungana na wachangiaji wengine inabidi C.C.M watuombe radha watanzania kwa sera zao mbovu, mikakati yao mibovu ndani ya miaka hamsini ya uhuru.

Alafu wananiuzi na msemo wao eti "TUMEDHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE" Mmeweza nini C.C.M ninyi? Hicho mlichoweza mbona hatukioni?

Huu ni muda watanzania wenzangu tuidai Tanganyika yetu.
 
Nafikiri Mheshimiwa Mnyika kuwataka Israel kutuomba msamaha atakua amekosea sana, hapa nadhani watu wa kutakiwa kutuomba msamaha watanzania ni CCM na serikali yake kwa kusababisha thamani ya waTanzania kushuka kwa kiasi hiki.
 
jamani, tumedhalilika vya kutosha, tumenyanyswa na matamshi haya vya kutosha. Hatuwezi kuvumilia. Mimi kama mtanzania napendekeza tutangaze mgogoro na hiyo nchi sijui inaitwa Israel. Hiyo nchi haina maana yoyote katika medani ya maisha ya kila siku ya mtanzania. Nasi tuwaambie kuwa Israel si nchi muhimu Tanzania. kuomba radhi tu hakutoshi maji yakiisha mwagika hayazoleki. Huyu jamaa katamka haya maneno kutoka rohoni mwake hata akiomba radhi haitasaidia kesha tudharirisha. Cha muhimu tuangalie tumejikwaa wapi, kesho na mwingine atatamuka hivi hivi. Tatizo kubwa letu tumekuwa watu wa kuwasujudia hawa watu weupe. Mtu akisha kuwa mweupe sisi kila goti litapigwa sasa tukome. Kila siku tumebaki katika kushabikia siasa za maji taka basi.

Kama hujui JK ndio anaweza kwenda kuomba radhi,Serikali yetu ni ya ajabu sana.
 
Duh!Umasikini shida sana tena hasa ukijiendekeza kwa kuombaomba,hv tukiamua kuwa masikini jeuri kama North Korea na Zimbabwe tutashindwa kweli?Hii kauli ya Ehud Barak ni ya kidhalilishaji sana,mbona wengi tu wanatusaidia bila kutusema vibaya?Haya tumekoma ndugu this time bakuli hatutalipitisha huko!!
 
Ishi!Eti aombe radhi ya nini?Nyie CHEDEMA,Tanzania haitoondokana na matatizo yake kwa kuombwa radhi na Israel.Sasa ni kweli Tanzania ni sawa na France au Uk kwa maslahi ya Israel?Sisi ni wa maana kwa Rwanda na Burundi,jamani kila nchi na class yao.Hata Dar ni ya maana kuliko Rukwa.
 
Mkuu SOBY, hata siku moja sintonunua fikra kama hizo!!!

Hizo wenzangu kazipelekeni hukooo!!! Kinachotufanya tuwe irrelevant ni nini hasa kama taifa? Labda kama kuna baadhi ya mambo ambayo wakuu wetu hutenda kinyume na matarajio ya ulimwengu hivyo kutufanya tusukumwe moja kwa moja jalalani.

Lakini hata tukihisiwa jalala, ni jukumu letu kukataa huo muonekano wa ujala machoni mwa ulimwengu kwa kuwa sisi tunawathamini sana tu tena kwa uzito wote hivyo ni matarajio yetu kurudishiwa heshma endapo hakina cha ajabu kilichofichama machoni mwetu wananchi.
North Korea ni jalala,jela kuu baada ya gaza.

Lakini wote hao wakibweka..... ni kama bloodhoun Pitbuls!! Upo hapo?

bullpit1.jpg
 
Ishi!Eti aombe radhi ya nini?Nyie CHEDEMA,Tanzania haitoondokana na matatizo yake kwa kuombwa radhi na Israel.Sasa ni kweli Tanzania ni sawa na France au Uk kwa maslahi ya Israel?Sisi ni wa maana kwa Rwanda na Burundi,jamani kila nchi na class yao.Hata Dar ni ya maana kuliko Rukwa.

kuna thread nimesoma Barak kagoma kuomba radhi na nikaishia kuuliza kimsingi maswali amabayo na wewe umeuliza hapa.
 
My comrade Mnyika pole sana wote tunaumia.... Ila wakulaumiwa ni hao wanaojiita viongozi wa Tanzania!

Imagine a country as small as Israel, na jangwa lake lote; inatumia sehemu ndogo ya ardhi inauza matunda nje kwa faida kubwa!!! Tanzania pamoja na ardhi oevu yote iliyonayo inashindwa kulisha wilaya zake........ (naachia hapa nasikia machozi yananilengalenga....)

Nani asiyetudharau.... aliyetwambia tuwe mashoga.... ameishia wapi....!?

mwingine kaniambia "mapacha watatu.... jamani nchi hii.....!
 
Laiti tungelikuwa na Rais kama Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere, sasa hivi Balozi wa Israel angelikuwa tayari yuko kwenye ndege anarudi kwao na kupishana na Balozi wetu akitokea Israel. Potelea mbali, misaada yake isije, tukae tutumie vyanzo vyetu.
 
Waziri wa ulinzi wa israel yupo sahihi!
Wanaompinga waseme kwa sasa umuhimu wetu ndani na nje ya nchi ni upi?
 
Hizo ni hisia za Israel,hata kama tukiwalazimisha waombe radhi,hizo zitabaki kuwa hisia zao siku zote!
Na kwakweli heshima huwa hailazimishwi bali hutolewa kwa yule anaye heshimika.

Mnyika kaweka vizuri kuwa sera zetu mbovu ndiyo msingi wa haya na iwapo Membe kama waziri mwenye dhamana anataka Tanzania iombwe radhi basi angalau ashauriane na wenzake kuhusu jinsi ya kubadili sera mbovu zinazotoa upendeleo kwa watu wa mataifa ya kigeni na kuwaacha wazawa katika aibu ya umasikini usiotazamika wala kutamanika.

Vinginevyo itabakia kama taarab tu na kujirusha huku ukifahamu kuwa ndani mwako huna thamani wala heshima katikati ya watu na jamii ila kwasababu unamdomo unaoweza kuimba basi inabidi ujifariji kwa jinsi hiyo.
 
Ishi!Eti aombe radhi ya nini?Nyie CHEDEMA,Tanzania haitoondokana na matatizo yake kwa kuombwa radhi na Israel.Sasa ni kweli Tanzania ni sawa na France au Uk kwa maslahi ya Israel?Sisi ni wa maana kwa Rwanda na Burundi,jamani kila nchi na class yao.Hata Dar ni ya maana kuliko Rukwa.
aisee kumbe na wewe ni wa kule kwetu; aisee tupo wengi kumbe.
 
My comrade Mnyika pole sana wote tunaumia.... Ila wakulaumiwa ni hao wanaojiita viongozi wa Tanzania!

Imagine a country as small as Israel, na jangwa lake lote; inatumia sehemu ndogo ya ardhi inauza matunda nje kwa faida kubwa!!! Tanzania pamoja na ardhi oevu yote iliyonayo inashindwa kulisha wilaya zake........ (naachia hapa nasikia machozi yananilengalenga....)

Nani asiyetudharau.... aliyetwambia tuwe mashoga.... ameishia wapi....!?

mwingine kaniambia "mapacha watatu.... jamani nchi hii.....!
WE ACHA TUU MKUUU
TUNABANDARI INGETOSHA KULISHA RWANDA, BURUNDI, ZAMBIA, UGANDA NA DRC
TUNAMAZIWA NA BAHARI TUNGEWEZA KUUZA SAMAKI
TUNAMBUGA NZURI
TUNAMAENEO KIBAO YA KILIMO YENYE RUTUBA
MITO KIBAO HATA MAJI SAFI HATUNA
KWANINI TUSIDHARAULIKE EETI!:A S embarassed:
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Na kwakweli heshima huwa hailazimishwi bali hutolewa kwa yule anaye heshimika.

Mnyika kaweka vizuri kuwa sera zetu mbovu ndiyo msingi wa haya na iwapo Membe kama waziri mwenye dhamana anataka Tanzania iombwe radhi basi angalau ashauriane na wenzake kuhusu jinsi ya kubadili sera mbovu zinazotoa upendeleo kwa watu wa mataifa ya kigeni na kuwaacha wazawa katika aibu ya umasikini usiotazamika wala kutamanika.

Vinginevyo itabakia kama taarab tu na kujirusha huku ukifahamu kuwa ndani mwako huna thamani wala heshima katikati ya watu na jamii ila kwasababu unamdomo unaoweza kuimba basi inabidi ujifariji kwa jinsi hiyo.
huyu ndo bure kabisa pesa ya wizi anaiiita chenji hahhahhaa jamaa simtaki huyu duuu!
Eeeeti chenji yetu sema pesa ya ufisadi nyambafu!
 
Back
Top Bottom