Chadema isisimamishe mgombea Arumeru

Mbona siku hizi washauri wa Chadema wanazidi kuwa wengi? kulikoni!!!!
Umeshawahi kusikia waliofeli Ndoa wanavyojifanya washauri?

Basi ndio waliovamia JF, ya kwao yamewashinda, wanatimua hadi wazee wao wenyewe....
 
Ni ushauri wa mtu asiyejua maana ya siasa...na huu ushauri nadhani ungefaa kwa chama cha majambazi aka CCM..kwa chama makini kama CDM ni ushauri uharo....
 
Kwa upeo wa mleta hoja, uchaguzi ni gharama hivyo CDM isishiriki!Hayo ni maoni yake.
Kwa kuwa ameona apite kidogo barazani kwa Great Thinkers tusimfukuze ktk mazungumzo yetu , isipokuwa tumfanye ktk dakika chache atakazokuwa nasi aondoke na fikra sahihi na makini.
Awali ya yote afahamu kuwa demokrasia ni gharama ingawa matunda yake - ama Democratic dividends kwa kimombo- yanaleta uhuru wa kiuchumi,kisiasa,kijamii nk.Kwa kikifupi kabisa ,faida zake zinazidi gharama.
Aidha,anapoleta mifano ya Igunga wakati huu tunapojiandaa kwenda Arumeru, anafanya mchezo /mzaha ambao ni yeye pekee na wenzake wanauelewa vyema.
Igunga, CCM waliiba kura,kama walivyofanya Kilombero kwa Regia, Hanang, Shinyanga Mjini,Karagwe,Kinondoni,Mbozi Mashariki,Kigoma mjini,Kigamboni , Arumeru Mashariki na maeneo mengine mengi ktk uchaguzi wa mwaka 2010 .Kwake yeye matokeo ya uchaguzi ni yale yaliyotangazwa na wakurugenzi wa uchaguzi!
Yafaa tumkumbushe kuwa ,hata Samuel Kivuitu ,Mkurugenzi wa zamani wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Kenya, siku chache baada ya yeye kutangaza matokeo, amewahi kunukuliwa akitanabaisha kuwa hajui ni nani hasa alikuwa ameshinda uchaguzi wa Rais ,mwaka 2007!
 
Inawezekana ni ushauri mzuri lakini umetazama "financial risks and returns only", you have not looked at the "political implications". Labda nikuulize swali dogo ambalo wewe naamini hukujiuliza, CCM watasemaje baada ya CHADEMA kujitoa???
Mkuu shukran... Kujitoa kwa CUF Arumeru kumenisikitisha sana kutokana na sababu walizozisema. Kama wangejitoa na kusema hawana imani na NEC na hivyo kuviomba vyama vingine vijitoe vile vile ningewapa salute!...Kusema kweli binafsi sioni sababu kabisa ya vyama vya Upinzani kuendelea kugombea ubunge na Udiwani mdogo kupitia NEC ambayo inaendelea kutumia mfumo mbovu unaowakandamiza. Ni lini vyama hivi vitaweza kudai demokrasia ya kweli ambayo ni haki yao?... Nakumbuka sana kwamba Igunga watu wameuawa na sijui kama serikali inajali wala kufuatilia sheria ya vifo vile!.
Ndio maana nikasema bora hata hao madaktari waliodai haki yao sasa naanza kuelewa japokuwa napinga maamuzi yao yaliyokuwa makili sana kwa wananchi, lakini mwisho wa siku wamefanikiwa kupata walichokitaka.
 
=Suala la uanachama wangu CDM halina kificho,kama mwanachama nina haki ya kutoa ushauri, pia nimesema think critically unaweza kuona point, usiwe mwepesi kupinga mawazo hadimu. Tatizo lako mtu akiwa na wazo mbadala wajua ni CCM, BADILIKA KIMTAZAMO wewe

Kumbuka kwamba kutomsimamisha mgombea nayo chama kina kosa umaarufu kwa hiyo ni bora kupoteza pesa lakini chama kinapata umaarufu na KIMSINGI hiyo ndiyo siasa yenyewe, ni kweli tuna hitaji chama kujenga chama vijjin lakini hiyo nayo inahitaji spill over effect that is why ni lazima tumweke mgombea na ruzuku itumike vizuri
 
Mkuu shukran... Kujitoa kwa CUF Arumeru kumenisikitisha sana kutokana na sababu walizozisema. Kama wangejitoa na kusema hawana imani na NEC na hivyo kuviomba vyama vingine vijitoe vile vile ningewapa salute!...Kusema kweli binafsi sioni sababu kabisa ya vyama vya Upinzani kuendelea kugombea ubunge na Udiwani mdogo kupitia NEC ambayo inaendelea kutumia mfumo mbovu unaowakandamiza. Ni lini vyama hivi vitaweza kudai demokrasia ya kweli ambayo ni haki yao?... Nakumbuka sana kwamba Igunga watu wameuawa na sijui kama serikali inajali wala kufuatilia sheria ya vifo vile!.
Ndio maana nikasema bora hata hao madaktari waliodai haki yao sasa naanza kuelewa japokuwa napinga maamuzi yao yaliyokuwa makili sana kwa wananchi, lakini mwisho wa siku wamefanikiwa kupata walichokitaka.

At some point I have had ideas of this kind, lakini ni vizuri pia tuangalie siasa zetu na mapana yake. Well, politics is a dirty game but in Africa is even dirtier, personally siamini kama kususia uchaguzi kunaweza kuwa na impact kubwa sana na viongozi wetu, kitachofuatia ni wao kujisifu kuwa tumeshinda kwa kishindo na wao "Walikosa sera na wameamua kukimbia".

Nakumbuka Tambwe Hizza wakati wa uchaguzi mdogo wa Kiteto (if am not miskaten), aliulizwa sababu ya wananchi kutojitokeza kwenye uchaguzi, moja ya sababu alizotoa ni "watu wameridhika na utawala uliopo, hawakuwa na sababu ya kupiga kura". Chama tawala chenye watu wa aina ya Komba, Prof. Maji Marefu, Lusinde etc, unadhani kitasema nini Chadema ikijitoa?? Umesikia kauli ya Nape aliyotoa kuhusu Dr Slaa kugombea Arumeru Mash., ndio zitakazoendelea mpaka 2015 kama CHADEMA itajitoa.

Lakini hata ukiangalia the aftermath of Igunga elections, CCM won the seat, but politically CHADEMA won the contest. By elections are an indicator to the current political situation after the general election. Nina hakika CCM watapigana KUFA NA KUPONA ili washinde hichi kiti. LOSING WILL BE A POLITICAL DISASTER TO THEM, WINNING WILL BE A VINDICATION OF 'KUVUANA MAGAMBA'.

Umesahau kauli za CCM baada ya uchaguzi Igunga, eti wananchi wanakubali mabadiliko ndani ya chama, they didint even care kama wamepoteza kura nyingi sana from the 2010 general election. CHADEMA wasijitoe, never never
 
Nakubaliana na wewe sana tu lakini nadhani kwa vyama ni muhimu kutazama sababu za wananchi. Huyo Tambwe kasema anavyojua yeye kulingana na siasa za CCM lakini ukweli ulikuwa UPi?.. wananchi wanajua hata wakishiriki uchaguzi dhidi ya CCM bado CCM itashinda..Wananchi chaguzi zote inaonyesha wazi kwamba hesabu inazidi kupungua iwe ni kwa uchakachuaji wa CCM ama kweli na kushuka kwa wapiga kura ni SAUTI ya wananchi kutoridhika na mfumo wa Uchaguzi..

Kwa hiyo wewe jiulize hutakwenda kupiga kura kwa sababu gani?.. na waulize watu wengi kwa nini hawaendi kupiga kura utaambiwa sababu ni hii tu sii kwamba wananchi wanaridhika na CCM, wameichoka sema hakuna chama kinacho watazama wao isipokuwa maslahi ya chama. Wee soma hata hoja za watu hapa JF ni kuhusu maslahi ya Chadema au CCM au CUF wananchi tunajichopeka tu kukidhi matakwa ya vyama.

Kwa hiyo kikitokea chama ambacho kinapinga au kuwakilisha wananchi nina hakika wananchi watakuwa nyuma yao. Chadema wamepata Umaarufu kutokana na kuonyesha kujali maslahi ya wananchi iwe zile hotuba za Dr.Slaa na Zitto au Mbowe lakini wote hawa walizungumzia matatizo ya wananchi na kuanza vita dhidi ya Ufisadi kwa vitendo.. Kupinga Richmond, Buswagi, List of Shame na kadhalika lakini sasa hivi yamekwisha kila chama kinaangalia maslahi yake. Na utakuja nambia utaona hata Arumeru watu wakataoshiriki kupiga kura watakuwa wachache sana ukilinganisha na mwaka 2010.
 
Ushauri mwingine bana.........na sawa na kumwambia mmarekani aukane uraia wake ili awe mtanzania kitu ambacho hakiwezekani............kwani ccm na ccm-b wanaongeza nini wakipata arumeru?
Asante kwa ushauri wako

mi nadhani muanzisha thread hii ndiye aliye mshauri pinda awatishie kuwafukuza kazi madocta walio goma. hebu punguza kutumia MWANAASHA katika kufikiri.
 
Chaguzi ndogo mfano ule wa Igunga, Vyama vya CCM, CHADEMA na CUF vilitumia pesa nyingi sana kwa ajili ya Kampeni. Nikiwa mwanachama na mkereketwa wa UKWELI ya CHADEMA nashauri tusisimamishe mgombea ARUMERU badala yake fedha zilizotakiwa zitumike kwenye kampeni zitumike kueneza itikadi na mtandao wa chama nchini. Viundwe vikosi kasi 25 kwenda kila mkoa angalau kwa mwezi mzima kwa ajili ya kazi hii. Naamini tutavuna wanachama wengi, na kufungua matawi mengi sana kwa njia hii. Tunao Makamanda kibao tu wenye uwezo wa kufanya kazi hii, mfano, Mhe. Mbowe, Dr. Slaa, Mhe. Zitto, Tundu......Mwakajila, Mtela, Heche, Mdee, na wengine wengi tu.

Ni ukosefu wa umakini kutumia milioni 500 kwa Jimbo moja wakati kiasi kama hicho kinaweza kutumika kukijenga chama takribani katika kila Jimbo nchini. Swali la kujiuliza ni hili hapa, Tutabadilisha kitu gani Bungeni ikiwa tutashinda ARUMERU Mashariki?? Still the vast majority will remain to CCM. I have a point try to think critically
. CDM, Kimbilio Letu, wengine ni Wababaishaji Tu!

We mtoa mada daladala kwanza karibu sana jf.

Pili tunaomba utajevituo vya gari yako ili kuepuka usumbufu wa kupitiliza vituo.

Tatu gari lako bovu sana lipeleke garage kwa matengenezo.
 
Nakubaliana na wewe sana tu lakini nadhani kwa vyama ni muhimu kutazama sababu za wananchi. Huyo Tambwe kasema anavyojua yeye kulingana na siasa za CCM lakini ukweli ulikuwa UPi?.. wananchi wanajua hata wakishiriki uchaguzi dhidi ya CCM bado CCM itashinda..Wananchi chaguzi zote inaonyesha wazi kwamba hesabu inazidi kupungua iwe ni kwa uchakachuaji wa CCM ama kweli na kushuka kwa wapiga kura ni SAUTI ya wananchi kutoridhika na mfumo wa Uchaguzi..

Kwa hiyo wewe jiulize hutakwenda kupiga kura kwa sababu gani?.. na waulize watu wengi kwa nini hawaendi kupiga kura utaambiwa sababu ni hii tu sii kwamba wananchi wanaridhika na CCM, wameichoka sema hakuna chama kinacho watazama wao isipokuwa maslahi ya chama. Wee soma hata hoja za watu hapa JF ni kuhusu maslahi ya Chadema au CCM au CUF wananchi tunajichopeka tu kukidhi matakwa ya vyama.

Kwa hiyo kikitokea chama ambacho kinapinga au kuwakilisha wananchi nina hakika wananchi watakuwa nyuma yao. Chadema wamepata Umaarufu kutokana na kuonyesha kujali maslahi ya wananchi iwe zile hotuba za Dr.Slaa na Zitto au Mbowe lakini wote hawa walizungumzia matatizo ya wananchi na kuanza vita dhidi ya Ufisadi kwa vitendo.. Kupinga Richmond, Buswagi, List of Shame na kadhalika lakini sasa hivi yamekwisha kila chama kinaangalia maslahi yake. Na utakuja nambia utaona hata Arumeru watu wakataoshiriki kupiga kura watakuwa wachache sana ukilinganisha na mwaka 2010.

Nakuelewa ndugu, watu wengi hawana imani na mfumo uliopo wa kubadilisha viongozi i.e UCHAGUZI. Lakini kuna njia mbili tu za kubadilisha viongozi kwenye nchi, either kwa kura au kwa nguvu.

Sasa watanzania kuna mkanganyiko mkubwa hapa, hawaamini katika kutumia kura na hawataki kutumia nguvu. Tunasubiri huruma za Magamba katika hili, it wont happen.

Lakini binafsi bado naamini kama wananchi wakashiriki kupiga kura kwa wingi na kuhakikisha kuwa wanazilinda kura zao, hawa magamba wanang'oka tu. Hata wizi una ukomo wake, tumeona yaliyotokea Mbeya mjini, Ilemela, Nyamagana, Arusha Mjini nk. Hawakupenda, lakini mwamko wa wananchi katika kupiga kura na kuzilinda uliwapa ushindi Chadema.

Wajikite katika haya mawili, kuhimiza watu kupiga kura halafu ulinzi wa kura zenyewe.
 
Umeshawahi kusikia waliofeli Ndoa wanavyojifanya washauri?

Basi ndio waliovamia JF, ya kwao yamewashinda, wanatimua hadi wazee wao wenyewe....

hahahahahaaaa......
Hii ni mbinu mpya mkuu!!
Ya kujifanya mkereketwa wa CDM then unatoa ushauri wa kikenge.
Wamegundua ule utaratibu wa akina ritz na rejao na kupeng'e dont work.

Kenge.....over.
 
Nakuelewa ndugu, watu wengi hawana imani na mfumo uliopo wa kubadilisha viongozi i.e UCHAGUZI. Lakini kuna njia mbili tu za kubadilisha viongozi kwenye nchi, either kwa kura au kwa nguvu.

Sasa watanzania kuna mkanganyiko mkubwa hapa, hawaamini katika kutumia kura na hawataki kutumia nguvu. Tunasubiri huruma za Magamba katika hili, it wont happen.

Lakini binafsi bado naamini kama wananchi wakashiriki kupiga kura kwa wingi na kuhakikisha kuwa wanazilinda kura zao, hawa magamba wanang'oka tu. Hata wizi una ukomo wake, tumeona yaliyotokea Mbeya mjini, Ilemela, Nyamagana, Arusha Mjini nk. Hawakupenda, lakini mwamko wa wananchi katika kupiga kura na kuzilinda uliwapa ushindi Chadema.

Wajikite katika haya mawili, kuhimiza watu kupiga kura halafu ulinzi wa kura zenyewe.
Haaaa! Haaa CCM hawawezi kung'oka wanajua kugawa pilau ktk masinia ya kura. Chadema imeshinda majimbo ambayo CCM ilitaka kuonyesha wananchi na vyombo vya kimataifa kwamba Uchaguzi wao ni free and fair hakuna mushkeri lakini wakiona wanashindwa ubunge na Urais kama ilivyotokea Zanzibar wataiba tu, tena hawana haja ya kuiba NEC akitangaza mshindi mahakama ina nafasi ndogo sana ya kupinga japokuwa tunaaminishwa hivyo.

Nina hakika Chadema walishinda zaidi ya majimbo unayoyasema na mfano mzuri Seif Hamad alishinda kwa zaidi ya asilimia 80 na CUF walishinda majimbo mengi kuliko CCM tena wala sii kidogo lakini majibu yaliyotoka yangekuwa kashfa kubwa lakini wananchi wakapozwa na serikali ya mseto iliyoandaliwa mapema wakijua CCM ushindi Zanzibar haiwezekani. Leo hii CUF kushinda Zanzibar itakuwa kazi mpya maana tayari CCM wameisha chukua utamaduni wa Wazanzibar na kuongea kama Wazanzibar kuliko CUF waasisi wa mageuzi. That is CCM my brother!

Nakuhakikishia CCM haiwezi kuondoka madarakani kwupitia sanduku la kura, Chadema inaweza kushinda Arumeru na pengine CCM watatumia uchaguzi kama huu kuangalia upepo na kwa fikra zangu CCM haitakubali kulipoteza jimbo hili kutokana na kwamba liko karibu na Arusha hivyo hawataki kupoteza majimbo mengi sehemu muhimu kaa hiyo. Na ikitokea wakiachia bado wana majority bungeni lakini kama Arumeru ingekuwa ndio jimbo la kuamua ushindi wa bungeni CCM wasingekubali kushindwa..

Mimi nachotazama ni interest za wananchi, sioni sababu kabisa ya Chadema na vyama vya Upinzani kushiriki Arumeru wala majimbo yaliyopita badala ya kutumia nafasi kama hizi kuandaa mazingira bora ya uchaguzi wa mwaka 2015. Wakisusa leo ikatokea jimbo jingine na jingine huku wakieneza siasa za kutoridhika na NEC basi itabidi bunge libadilishe muundo wa NEC na mahakama ipewe mamlaka juu ya NEC ktk vipengele vyote. Wakati ndio huu na wananchi wakipata mwamko wanaweza kutumia nguvu za Umma maana kama unakumbuka siku zote wananchi wamekuwa wakiuliza viongozi wa vyama vya Upinzani kama kuna maandamano au maandalizi yoyote ya kupinga utawala huu.

Na mara zote JK na UWT wamekuwa wepesi kuzima maandamano ambayo wanajua fika chanzo chake kitatokana na vyama maana sisi wenyewe hatuaminiani kuna unafiki mkubwa sana. Mtu anacheka na wewe usoni tu ukimpa mgongo habari zako tayari zimeisha fika upande wa pili, bora siye kina Mkandara tukichukia kitu tunakiweka wazi hata mhusika anakisoma anajua msimamo wako na ndio wanatuona wabaya sana kuliko wale wanaowachekea lakini wanakunyonga bila wewe kujijua.
 
Chaguzi ndogo mfano ule wa Igunga, Vyama vya CCM, CHADEMA na CUF vilitumia pesa nyingi sana kwa ajili ya Kampeni. Nikiwa mwanachama na mkereketwa wa UKWELI ya CHADEMA nashauri tusisimamishe mgombea ARUMERU badala yake fedha zilizotakiwa zitumike kwenye kampeni zitumike kueneza itikadi na mtandao wa chama nchini. Viundwe vikosi kasi 25 kwenda kila mkoa angalau kwa mwezi mzima kwa ajili ya kazi hii. Naamini tutavuna wanachama wengi, na kufungua matawi mengi sana kwa njia hii. Tunao Makamanda kibao tu wenye uwezo wa kufanya kazi hii, mfano, Mhe. Mbowe, Dr. Slaa, Mhe. Zitto, Tundu......Mwakajila, Mtela, Heche, Mdee, na wengine wengi tu.

Ni ukosefu wa umakini kutumia milioni 500 kwa Jimbo moja wakati kiasi kama hicho kinaweza kutumika kukijenga chama takribani katika kila Jimbo nchini. Swali la kujiuliza ni hili hapa, Tutabadilisha kitu gani Bungeni ikiwa tutashinda ARUMERU Mashariki?? Still the vast majority will remain to CCM. I have a point try to think critically
. CDM, Kimbilio Letu, wengine ni Wababaishaji Tu!

mkuu kipimo cha chama chochote kukubalika ni kushiriki chaguzi na kushinda. Sasa cdm wasiposhiriki uchaguzi dhumuni lao litakuwa ni nini hasa? Hata kwenye mikutano ya injli lazima watu wahudhurie ili wahubiri wajipime kukubalika kwao.
Hata hivyo wapelekee ccm ushauri huo maana unawafaa sana wao.
 
mkandara, niseme tu sina wakati na nyenzo kwa sasa kwa ajili ya kujadili nawe swala hili.

Interesting!! Lakini wewe kweli wewe?........siasa hizi unazijua mkuu, dont start that!!
 
Nashukuru kwa michango wenu nyote (senior & junior JF members). Wazo langu halina na wala halikuwa na hila yoyote kwa CDM. Nimeeleza hivyo kutokana na ukweli kuwa kuna baadhi ya maeneo hapa nchini (Rukwa, Mbeya na Iringa) wananchi wameonyesha kuhitaji sana kutembelewa na viongozi wa CDM. Pili, ili tushinde general elections in 2015 maandalizi lazima yaanze sasa. Kiukweli kuna maeneo mengi nchi hii bado hayajafikiwa na siasa HAI za CDM. Sawa, nakubali kuwa wengi wenu mngependelea sana tushiriki uchaguzi A. Mashariki lakini natoa angalizo kwa viongozi wetu kuwa makini na matumizi ya fedha ili sehemu kubwa ielekezwe vijijini tena kwenye majimbo mengi zaidi. Mimi kwa shughuli zangu ninazofanya huwa natembelea sana maeneo mengi ya nchi hii nathubutu kusema kuwa kuna mikoa tunahitaji kufanya kazi kubwa kwani bado imelala sana kisiasa. Morogoro, Ruvuma, Tabora, Singida, Tanga, Lindi, Mtwara, Dodoma na Pwani. Acheni kuwa wepesi kutoa kashifa na matusi muwe mnatafakari mambo kwa upana. Na pia it is good to think out of the BOX. Hata nitukanwe bado mimi ni CDM damu damu.
 
Mkuu shukran... Kujitoa kwa CUF Arumeru kumenisikitisha sana kutokana na sababu walizozisema. Kama wangejitoa na kusema hawana imani na NEC na hivyo kuviomba vyama vingine vijitoe vile vile ningewapa salute!...Kusema kweli binafsi sioni sababu kabisa ya vyama vya Upinzani kuendelea kugombea ubunge na Udiwani mdogo kupitia NEC ambayo inaendelea kutumia mfumo mbovu unaowakandamiza. Ni lini vyama hivi vitaweza kudai demokrasia ya kweli ambayo ni haki yao?...

Mkuu umesema vyema.

Hata mimi uwa sivielewi hivi vyama vya upinzani,wakati wa uchaguzi vinalalamika na kupiga kelele juu ya rafu katika uchaguzi. Uchaguzi unaisha,mambo yanaendelea kama kawaida. Ukija uchaguzi mwingine,vyama hivyo hivyo vinavyolalama,navyo vinajitosa tena ndani,wakati zile rafu walizozilalamikia hazijafanyiwa kazi!!

Ushiriki wao unadhihirisha kwamba vyama hivyo vinakubali kuingia katika mechi ambayo vinaelewa fika kwamba haitakua ya huru na haki,kwani mwamuzi anajulikana yupo upande wa timu pinzani!

Hakika naungana nawe kwamba,ni heri C.U.F wangejitoa kutokana na mazingira ya mchezo kuwa si ya haki na usawa. Hata CHA.DE.MA. wakijitoa kwa grounds hizo hizo nitawaunga mkono. Nakumbuka Igunga vyama vililalamika juu ya daftari la wapiga kura kutoboreshwa. Katika uchaguzi wa Arumeru,NEC imesema haitaboresha pia daftari hilo! Sasa kwa hali hiyo,kuna haja ya kushiriki kweli?!

Hivyo wakishiriki katika mchezo wanaofahamu fika hautokua wa haki na usawa,mwisho wa siku wasilalame kuonewa kutokana na mwamuzi kuwa na upande wa pili.
 
Chaguzi ndogo mfano ule wa Igunga, Vyama vya CCM, CHADEMA na CUF vilitumia pesa nyingi sana kwa ajili ya Kampeni. Nikiwa mwanachama na mkereketwa wa UKWELI ya CHADEMA nashauri tusisimamishe mgombea ARUMERU badala yake fedha zilizotakiwa zitumike kwenye kampeni zitumike kueneza itikadi na mtandao wa chama nchini. Viundwe vikosi kasi 25 kwenda kila mkoa angalau kwa mwezi mzima kwa ajili ya kazi hii. Naamini tutavuna wanachama wengi, na kufungua matawi mengi sana kwa njia hii. Tunao Makamanda kibao tu wenye uwezo wa kufanya kazi hii, mfano, Mhe. Mbowe, Dr. Slaa, Mhe. Zitto, Tundu......Mwakajila, Mtela, Heche, Mdee, na wengine wengi tu.

Ni ukosefu wa umakini kutumia milioni 500 kwa Jimbo moja wakati kiasi kama hicho kinaweza kutumika kukijenga chama takribani katika kila Jimbo nchini. Swali la kujiuliza ni hili hapa, Tutabadilisha kitu gani Bungeni ikiwa tutashinda ARUMERU Mashariki?? Still the vast majority will remain to CCM. I have a point try to think critically
. CDM, Kimbilio Letu, wengine ni Wababaishaji Tu!

We dala dala we. CCM wataongeza nini bungeni wakichukua Arumeru? CDM mmoja gambaz 20. Sasa CDM wakiongeza kichwa kimoja utaona impact yake. Ushauri wako umesikiwa. Haupokelewi wala kutiliwa maanani!
 
Haaaa! Haaa CCM hawawezi kung'oka wanajua kugawa pilau ktk masinia ya kura. Chadema imeshinda majimbo ambayo CCM ilitaka kuonyesha wananchi na vyombo vya kimataifa kwamba Uchaguzi wao ni free and fair hakuna mushkeri lakini wakiona wanashindwa ubunge na Urais kama ilivyotokea Zanzibar wataiba tu, tena hawana haja ya kuiba NEC akitangaza mshindi mahakama ina nafasi ndogo sana ya kupinga japokuwa tunaaminishwa hivyo.

Nina hakika Chadema walishinda zaidi ya majimbo unayoyasema na mfano mzuri Seif Hamad alishinda kwa zaidi ya asilimia 80 na CUF walishinda majimbo mengi kuliko CCM tena wala sii kidogo lakini majibu yaliyotoka yangekuwa kashfa kubwa lakini wananchi wakapozwa na serikali ya mseto iliyoandaliwa mapema wakijua CCM ushindi Zanzibar haiwezekani. Leo hii CUF kushinda Zanzibar itakuwa kazi mpya maana tayari CCM wameisha chukua utamaduni wa Wazanzibar na kuongea kama Wazanzibar kuliko CUF waasisi wa mageuzi. That is CCM my brother!

Nakuhakikishia CCM haiwezi kuondoka madarakani kwupitia sanduku la kura, Chadema inaweza kushinda Arumeru na pengine CCM watatumia uchaguzi kama huu kuangalia upepo na kwa fikra zangu CCM haitakubali kulipoteza jimbo hili kutokana na kwamba liko karibu na Arusha hivyo hawataki kupoteza majimbo mengi sehemu muhimu kaa hiyo. Na ikitokea wakiachia bado wana majority bungeni lakini kama Arumeru ingekuwa ndio jimbo la kuamua ushindi wa bungeni CCM wasingekubali kushindwa..

Mimi nachotazama ni interest za wananchi, sioni sababu kabisa ya Chadema na vyama vya Upinzani kushiriki Arumeru wala majimbo yaliyopita badala ya kutumia nafasi kama hizi kuandaa mazingira bora ya uchaguzi wa mwaka 2015. Wakisusa leo ikatokea jimbo jingine na jingine huku wakieneza siasa za kutoridhika na NEC basi itabidi bunge libadilishe muundo wa NEC na mahakama ipewe mamlaka juu ya NEC ktk vipengele vyote. Wakati ndio huu na wananchi wakipata mwamko wanaweza kutumia nguvu za Umma maana kama unakumbuka siku zote wananchi wamekuwa wakiuliza viongozi wa vyama vya Upinzani kama kuna maandamano au maandalizi yoyote ya kupinga utawala huu.

Na mara zote JK na UWT wamekuwa wepesi kuzima maandamano ambayo wanajua fika chanzo chake kitatokana na vyama maana sisi wenyewe hatuaminiani kuna unafiki mkubwa sana. Mtu anacheka na wewe usoni tu ukimpa mgongo habari zako tayari zimeisha fika upande wa pili, bora siye kina Mkandara tukichukia kitu tunakiweka wazi hata mhusika anakisoma anajua msimamo wako na ndio wanatuona wabaya sana kuliko wale wanaowachekea lakini wanakunyonga bila wewe kujijua.

That's a good point, CUF wameshinda chaguzi za ZNZ toka 1995 lakini hawajawahi kuingia ikulu. Lakini tuna nafasi sasa hivi ya kubadilisha hii katiba yetu na naamini kubadilisha maisha yetu pia kama hatutafanya mzaha na hili jambo la tume huru ya uchaguzi. Tuanzie na hili, kwa sababu hapa ndio mwanzo wa kwenda mbele au kurudi nyuma kimaendeleo.
 
Haaaa!Haaa CCM hawawezi kung'oka wanajua kugawa pilau ktk masinia ya kura. Chadema imeshinda majimbo ambayo CCM ilitakakuonyesha wananchi na vyombo vya kimataifa kwamba Uchaguzi wao ni free and fairhakuna mushkeri lakini wakiona wanashindwa ubunge na Urais kamailivyotokea Zanzibar wataiba tu, tena hawana haja ya kuiba NEC akitangazamshindi mahakama ina nafasi ndogo sana ya kupinga japokuwa tunaaminishwa hivyo.

Nakuhakikishia CCMhaiwezi kuondoka madarakani kwupitia sanduku la kura, Chademainaweza kushinda Arumeru na pengine CCM watatumia uchaguzi kama huu kuangaliaupepo na kwa fikra zangu CCM haitakubali kulipoteza jimbo hili kutokana nakwamba liko karibu na Arusha hivyo hawataki kupoteza majimbo mengi sehemumuhimu kaa hiyo. Na ikitokea wakiachia bado wana majority bungeni lakini kamaArumeru ingekuwa ndio jimbo la kuamua ushindi wa bungeni CCM wasingekubalikushindwa..
Mkandara

Nikupongeze kwa mchango wako, kwanza umesema umesikitishwa kwa CUF kujitoa halafu hapohapo unashauri Chadema wasusie uchaguzi, ingawa umetaja sababu zagharama na NEC lakini mimi naziweka pamoja, zote hizo haziwezi kusababisha chama makini kikajitoa. Mosi unapojitoa unawanyima wanachama na wapenzi wako haki na uhuru wa kuchagua wanayemtaka, pili kujitoa au kususia ni kumpa faidaza bure mpinzani wako tatu kutoshiriki uchaguzi ni sawa na kuhudhuria darasaniila wakati wa majaribio hufanyi unatoa visingizio, je utapimaje mafanikio kama hufanyi mtihani.

Nilipobold, si kweli kuwa majimbo iliyoshinda Chadema walipewa na CCM kuonyesha uchaguzi ni free & fair, jimbo kama la Nyamagana CCM inalihitaji kwa udi nauvumba, jimbo la Arusha mjini, Mbeya mjini, Ubungo na mengine ya CDM ni majimboambayo ni hub ya uchumi wa Tanzania, level ya economic activities kwenye majimbo hayo ni za hali ya juu kwa hiyo si kusema CCM waliyaachia huku wakipenda, kama lengo lao lilikuwa hilo basi wangeachia majimbo ya pembezoni yasiyo na impact kubwa kwa uchumi.

Kuhusu CCM kuondoka kwa ballot box nakuhakikishia inawezekana, CCM ilipofikia kisiasa haina mbinu zozote mpya za kuwafanya wananchi waendelee kukiamini,inachokifanya sasa si siasa tena ila ni utawala wa kikomunisti (dominant-partyrule) wa mabavu do this or face the consequences haitawali kwa ku compromize nawananchi wake. Kwa hiyo itafikia/imefikia hatua hata wenyewe kwa wenyewe wanajiuliza kama wako kwa ajili ya wananchi, baada ya kugudua hilo ndio dhana ya uvuaji gamba ikaja wameona wasivyofanya hivyo come 2015 election wanaweza kupoteza dola.
 
Back
Top Bottom