Haya ni matokeo ya kamasi kujaa kichwani badala ya ubongo!
Huyu jamaa atakuwa amelala, plz jaman tumsubiri aamke...
mawazo ya kimagambamagamba peleka kwa magamba wenzio
Haya ni matokeo ya kamasi kujaa kichwani badala ya ubongo!
=Suala la uanachama wangu CDM halina kificho,kama mwanachama nina haki ya kutoa ushauri, pia nimesema think critically unaweza kuona point, usiwe mwepesi kupinga mawazo hadimu. Tatizo lako mtu akiwa na wazo mbadala wajua ni CCM, BADILIKA KIMTAZAMO wewe
HOJA YA KIGWANGALA KUWATAKA CHADEMA WASIWEKE MGOMBEA ARUMERU MASHARIKI KAMA ALIVYOIBANDIKA KULE WANABIDII:
Ndugu,
Nimejifikiria sana na kuona kwamba uwezekano wa CHADEMA kushinda jimbo la Arumeru East ni mdogo sana. Wataishia kupoteza fedha zao nyingi, muda na kuathirika kisaikolojia. Badala ya kutunza nguvu zao na kujipanga kwa ajili ya 2015 wanatunisha msuli kupambana na chama dume CCM. Mimi nimejiuliza maswali; hivi hawa wakishinda wanakuwa wameongeza nini? Nikaona kwa CCM ni muhimu kwao kushinda jimbo hili ili kulinda heshima ya Marehemu Sumari aliyetangulia mbele ya haki. Nikaona kwa precedence hii kuna umuhimu wa CCM kuendelea kuliwakilisha Bungeni jimbo lile kwa lengo la kulinda heshima tu hiyo basi, maana hata wakishindwa haina maana yoyote kubwa kwenye demokrasia ya ndani ya Bunge, maana tayari CCM ina majority, na majority ndiyo inatawala! Gharama ya uchaguzi mdogo inakadiriwa kufikia takriban bilioni 19! Kwa sababu gani, hii ndiyo gharama ya demokrasia kwenye nchi yenye changamoto nyingi za kiuchumi kama Tanzania, kwa faida ya nani? Kwa nini sasa CCM wenyewe ambao walishinda uchaguzi uliopita wasipewe fursa ya kuteua mtu na kumuweka pale? Hata aliyekuwa wa pili kwenye kura za maoni wa wakati ule?
Hapo sasa inakuja hoja ya uzalendo. Nchi ina changamoto ya pesa na mahitaji makubwa ya wananchi, kwa nini tunai-expose kwenye kuingia gharama kubwa kiasi hiki leo hii ili kuweka mbunge mmoja tu? Pili, chaguzi ndogo zinapoteza attention ya wananchi na kila kitu sasa kinakuwa ni uchaguzi tu, kwa nini tusiliepuke hili na kutumia muda huu kama Taifa kujadili mengine ya maendeleo zaidi kwa nchi? Tayari CUF wametangaza kutoweka mgombea. Sijasikia vyama vingine vikiwa na ratiba ya kuingia kwenye mchakato zaidi ya CHADEMA, sasa kwa nini na wao wasiihurumie nchi wakaacha kuweka mgombea tuka-save gharama hizi?
Rai yangu, vyama vya upinzani tumieni busara, zuwieni pesa
Wakatabahu,
HK.
Unaweza dhani kuwa unapoint, lakini nachokiona hapo unajaribu kujenga hoja ili chama chako cha CCM kijishindie kilaini. CDM tunasema ili mshinde huko inabidi jasho la kwapa liwatoke kwanza, hakuna ushindi wa mezani.. Swali la kujiuliza ni hili hapa, Tutabadilisha kitu gani Bungeni ikiwa tutashinda ARUMERU Mashariki?? Still the vast majority will remain to CCM. I have a point try to think critically. CDM, Kimbilio Letu, wengine ni Wababaishaji Tu!