CHADEMA isiposhinda Urais 2015 itakufa

CHADEMA isiposhinda Urais 2015 itakufa

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,209
Title ya thread yangu inaweza kunifanya nionekana masalia au buku saba group lakini si hivyo, mimi ni mwanachadema hai mwenye mapenzi ya dhati kabisa kwa chama changu na hili natoa kama angalizo kwa kuzingatia historia.

Kwa kawaida vyama vya upinzani hupata umaarufu mkubwa sana kutokana na utawala mbaya wa vyama tawala. Hapa nchini kwetu tayari tuna uzoefu wa nguvu ya NCCR mageuzi mwaka 1995 wakati nchi ilipokuwa chini ya utawala mbovu wa Ali Hassani Mwinyi. Katika utawala wa Mwinyi, nchi ilikuwa haina mwenyewe. Nchi ilikuwa inanuka rushwa, kazi zilikuwa hazilipi, ujambazi na mauaji ya kutisha vilikuwa ni vitu vya kawaida kabisa. Wakati huu Mrema alipata umaarufu wa kutisha, akaonekana ni chaguo na kimbilio la wale wasio na mtetezi. Kwa bahati mbaya wanyonge wakashindwa, wenye nazo wakashinda. Mkapa akaingia madarakani. Akaanza kurekebisha mambo, na kuirudisha nchi kwenye mstari. Ndani ya miaka mitano ya awali, watu wakajenga imani kubwa kwake, term ya pili ya uchaguzi mwaka 2000, Mkapa akapata ongezeko la kura kwa asilimia kumi ukilinganisha na zile za mwaka 1995. Watu wakarudisha imani kubwa kwa CCM. Kiasi cha kwamba ulipokuja uchaguzi wa mwaka 2005, hakuna aliyekuwa anawataka wapinzani. Watu walijiaminisha kwamba CCM yatosha. Kikwete akaingia madarakani kwa ushindi wa zaidi ya asilimia 80.

Hivi sasa Kikwete kavurugavuruga mambo, nchi ipoipo tu kama isiyo na mwenyewe. Inakwenda tu kama ndege isiyo na rubani. Hali ya maisha imezidi kuwa ngumu, mfumko wa bei umeongezeka mara dufu huku njia halali za utafutaji hela zikizidi kufungwa. Kama ilivyokuwa wakati wa Mwinyi ambapo watu walitozwa hadi kodi za baiskeli, hali inajirudia tena hivi sasa kwenye utawala wa Kikwete, watu sasa wanatozwa hadi kodi ya laini ya simu. Kama ilivyokuwa wakati wa Mwinyi ambapo wenye nacho walizidi kuwa nacho wakawepo matajiri wa kutisha na masikini wanaotia huruma hali ndiyo ilivyo wakati wa Kikwete. Kama ilivyokuwa wakati wa Mwinyi, wakati ambao ilikuwa ukilala hadi asubuhi na kuamka salama unamshukuru Mungu kwamba majambazi hawakupita kwako siku hiyo, ndivyo hali ilivyo sasa.

Watu wamejaribu kuonyesha hasira zao kwenye sanduku la kura mwaka 2010, ambapo kura zilishuka kwa karibu asilimia 20. Lakini hiyo haijatosha. Hali ya maisha imezidi kuwa mbaya na yenye kukatisha tamaa. Polisi wameacha kufanya kazi ya kushughulika na wahalifu na kuwalinda watu na mali zao, hivi sasa wanafanya kazi ya kubambikia watu kesi, wanaua na kuwashitaki watu wasio na hatia. Haya mambo yanawachosha na kuwakatisha tamaa sana wananchi dhidi ya CCM. Watu hivi sasa wanaichukia CCM kwa dhati, kiasi cha kwamba kama ambavyo Mrema alionekana kuwa mkombozi wa wanyonge kwa wakati ule, ndivyo ambavyo CHADEMA inaonekana kuwa ndiyo mkombozi wa hali za maisha ya sasa ya watanzania.

Watanzania wanaiona CHADEMA kama chama chenye uwezo wa kubadilisha hali ya mambo nchini kwa kuwa chama tawala kimekuwa chama mfu. Kimeiacha nchi iende kama ndege isiyo na rubani au meli isiyo na nahodha. Nchi inasombwa na mawimbi ya ujambazi, ufisadi, mauaji ya kutisha na umasikini mkubwa huku waliopewa mamlaka ya kuinusuru wakiwa wapo busy na mambo yao. Katika mazingira haya wananchi wataipa kura CHADEMA.

Huu ni wakati mhimu kwa CHADEMA kuchanga karata zao vema, wakishindwa tu kufanya hivyo, CCM inaweza kupata Rais makini mwaka 2015, na watu wakarudisha tena matumaini kwa CCM. Na ikifikia hatua hiyo, basi CHADEMA inaweza kuanza kupotea katika ramani ya siasa za Tanzania kama vile ambavyo NCCR na CUF vilipotea. Maana kitakachotokea hivi sasa ni kwamba CHADEMA itazoa kura nyingi sana 2015, lakini kisiposhinda akaingia Rais makini kutoka CCM, wananchi wakamwamini, inamaana mwaka 2020 wananchi wataipigia kura nyingi CCM na kuinyima kura CHADEMA. Na hivyo itawezekana kwa kuwa CHADEMA kitakuwa hakina serikali katika muda wa miaka mitano na hivyo kutokuwa na impact kubwa kama ambavyo chama tawala kitakuwa nayo chini ya Rais makini atakayeingia wakati huo.

Tufanye kazi usiku na mchana wanachadema wenzangu. Napendekeza tuanzishe vyombo vyetu vya habari vitakavyosaidia kukiuza chama. Ndani ya hii miaka miwili ya utawala dhaifu uliopo madarakani, tufanikiwe kuteka nyoyo za watanzania. Kwa hakika tutashinda. Failure of that, tuandike maumivu. Naamini CCM watamleta mtu wa tofauti, asiyetajwa tajwa kama alivyoletwa Mkapa, ili kuiokoa nchi na chama pia. Kwa sasa nchi ilipo si salama kabisa. Tunamuomba sana Mungu atusaidie tufike salama 2015. Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki CHADEMA.
 
CHADEMA kwa sasa hakina dira wala mwelekeo. Kinategemea siasa za matukio tu ambazo nazo hawaziwezi. 2015 wategemee anguko kubwa sana. Rasharasha zitaanzia mwaka 2014. CHADEMA kitapoteza wabunge wengi na kwa upande wa rais hali itakuwa mbaya zaidi kama ilivyomtokea Tsvangirai wa zimbabwe
 
Endelea kujipa Moyo labda CUF na CCM wanaweza ku-fit hapa
 
Utakufa uiache chadema
Asilimia 80 ya watanzania wana matatizo kama ya kwako. Ya kujibu asichokijua. Maana kwa hakika inaonekana umesoma tu title bila kusoma ujumbe uliopo ndani.
 
At leat i have noticed a point, but 1995 nyrere aliingilia kati ili mkapa achukue nchi, now hakuna tena mwenye uwezo wa kufanya hivo bali pesa ndo itatumika,,,,staili ya uongozi ya kikwete na mwinyi ni sawa,but mwinyi hakuwa mdini na alikubali kukosolewa, rais aliyetangazia taifa kuwa anawajua wauza mihadarati anaomba waache,,,,,,,,,,dhoooooofu
 
Asilimia 80 ya watanzania wana matatizo kama ya kwako. Ya kujibu asichokijua. Maana kwa hakika inaonekana umesoma tu title bila kusoma ujumbe uliopo ndani.
Huo ndo uelewa wa vijana wa bavicha. Yaani mtu anayewatahadhalisha kama afanyavyo HAMY D wao humwona kama ni kikwazo. Hata Lukolo alitoa angalizo mapema kuwa kuna watu watamwita masalia na wameanza kujitokeza kama akina Kazitunayo
 
CHADEMA kwa sasa hakina dira wala mwelekeo. Kinategemea siasa za matukio tu ambazo nazo hawaziwezi. 2015 wategemee anguko kubwa sana. Rasharasha zitaanzia mwaka 2014. CHADEMA kitapoteza wabunge wengi na kwa upande wa rais hali itakuwa mbaya zaidi kama ilivyomtokea Tsvangirai wa zimbabwe
That is totally wrong! Kama ingekuwa hivyo wananchi wasingeiamini CHADEMA kuliko CCM. CCM ndiyo chama kisichojitambua kwa sasa, kipo madarakani kwa kuwa tu kinatakiwa kuwa madarakani, lakini hakijui hata ni kwanini kipo madarakani. Ndiyo maana ninasema kwa sasa ni kama nchi haina Rais, CHADEMA ndiyo wanaongoza nchi kutokea nje ya system. Ndiyo wanaopiga ngoma, CCM wanaicheza. Tunachosisitiza sasa, ni kufanya bidii ya kuuza sera za chama chetu ili kuhakikisha kwamba 2015 watanzania wanatuelewa, na kutupa dola. Tukiingia tu madarakani, basi mjue CCM haitakaa iongoze tena nchi kwa kuwa wananchi wataridhishwa na kazi nzuri ya CHADEMA, na watajuta kuchelewa kuichagua. Lakini tusipoingia, halafu nyie mkabahatisha kumpata Rais bora basi kutakuwa na walakini kwa CHADEMA kuingia madarakani tena kwa kuwa wananchi watakuwa wamepata satisfaction.
 
At leat i have noticed a point, but 1995 nyrere aliingilia kati ili mkapa achukue nchi, now hakuna tena mwenye uwezo wa kufanya hivo bali pesa ndo itatumika,,,,staili ya uongozi ya kikwete na mwinyi ni sawa,but mwinyi hakuwa mdini na alikubali kukosolewa, rais aliyetangazia taifa kuwa anawajua wauza mihadarati anaomba waache,,,,,,,,,,dhoooooofu
Kwa hiyo hoja yako iko wapi?
 
Huo ndo uelewa wa vijana wa bavicha. Yaani mtu anayewatahadhalisha kama afanyavyo HAMY D wao humwona kama ni kikwazo. Hata Lukolo alitoa angalizo mapema kuwa kuna watu watamwita masalia na wameanza kujitokeza kama akina Kazitunayo
Dah, Lizaboni, nipe tano!! Leo umeongea vizuri. Kesho si unamaliza mfungo? Nitafute nikupe serengeti baridi!
 
Last edited by a moderator:
Hii ni sawa na kusema chadema imeshakufa kwa sababu swala la kushinda Urais 2015 HALIPO...
 
That is totally wrong! Kama ingekuwa hivyo wananchi wasingeiamini CHADEMA kuliko CCM. CCM ndiyo chama kisichojitambua kwa sasa, kipo madarakani kwa kuwa tu kinatakiwa kuwa madarakani, lakini hakijui hata ni kwanini kipo madarakani. Ndiyo maana ninasema kwa sasa ni kama nchi haina Rais, CHADEMA ndiyo wanaongoza nchi kutokea nje ya system. Ndiyo wanaopiga ngoma, CCM wanaicheza. Tunachosisitiza sasa, ni kufanya bidii ya kuuza sera za chama chetu ili kuhakikisha kwamba 2015 watanzania wanatuelewa, na kutupa dola. Tukiingia tu madarakani, basi mjue CCM haitakaa iongoze tena nchi kwa kuwa wananchi wataridhishwa na kazi nzuri ya CHADEMA, na watajuta kuchelewa kuichagua. Lakini tusipoingia, halafu nyie mkabahatisha kumpata Rais bora basi kutakuwa na walakini kwa CHADEMA kuingia madarakani tena kwa kuwa wananchi watakuwa wamepata satisfaction.

Mkuu Lukolo, inavyoelekea wewe hujui kabisa nini maana ya chama kuitwa cha upinzani. Kwako unaona kuwa upinzani ni uadui au unaona kuwa wapinzani ndo wana sera nzuri kuliko chama tawala. Mkuu Lukolo, kusema kuwa CHADEMA kinaongoza nchi nje ya system huko ni kukosa kuelewa. Ujue kuwa viongozi wa CHADEMA na CCM wote ni watanzania na wanapigania maendeleo ya mtanzania. Kwako unaona kuwa jambo zuri likitekelezwa na serikali basi ni la CHADEMA. nilidhani utaipongeza serikali kwa kuwa sikivu kusikiliza hoja za wananchi kumbe nawe ni kama hawa bavicha ambao uelewa wao ni pungufu
 
Mimi ninachohitaji ni maisha bora. Hata raisi akitoka CCJ au mgombea binafsi, kwangu ni sawa. Sitapiga kura kuchagua chama, nitapiga kura kuchagua mtu makini kwa nafasi ya diwani, mbunge na hata Raisi. Kuendekeza mahaba kwa vyama badala ya mtu makini ndo yamemwingiza Kikwete ikulu muhura wa Pili.
 
chdm hakina dira na falsafa inayo eleweka! kimekua na siasa za kudandia matukio yanayo tukia. sasa hivi chdm kimetoka wkenye siasa na kuelemea kwenye uanaharakati. ukabila, ukanda, ubabe, kibri, dharau na ugaidi haviwezi kukiacha salama. kwa hali hii chdm itapata mpasuko kabla ya 2015. zitto hasalimiani vizuri na slaa, mnyika ameota mapembe kama mwenya chdm, lissu anatak uenyekiti, lwakatare analalamika kususwa kiujanja, prof baregu anawatukana akina slaa kila siku kuwa hawana akili na anadharau kwa sasa, marando amevuta pumzi anasoma mazingira. ccm itashinda 2015. baada ya hapo chdm kitasambaratika kishenzi kutokana na uchache wa wabunge
 
Chadema Kama hakitashinda urais na kikawa na wabunge wengi kitapita salama na hakiwezi sambaratika
 
Mkuu, umegusia maeneo ya msingi japokuwa kuna upotofu katika hoja juu ya vyama vikuu vya upinzani kupoteza nguvu baada ya kushindwa uchaguzi. Vyama kama NCCR Mageuzi na CUF havikupoteza nguvu kwa sababu ya CCM kuimarika bali kwasababu ya uongozi wa vyama hivyo kudhoofika.Vyama hivyo vilikuwa mifukoni mwa viongozi ndiyo hadi sasa ujiulize CUF bila Lipumba kinaendaje? Mpaka sasa, CHADEMA kwa asilimia zaidi ya 70 kimevuka mstari huo kwani kinazidi kujengwa katika mfumo wa kitaasisi na ndiyo maana kuna viongozi wanaosimamia chama kutoka kila kanda. Lakini pia focus ya CHADEMA siyo Ikulu tu bali pia kuongeza idadi ya wabunge na madiwani kwa ajili ya kuwatumikia wananchi hivyo nguvu ya chama haipo mikononi mwa mgombea urais kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF. Kuna watu wanadhani Mhe.Kikwete peke yake ndiye aliyeshindwa lakini si kweli kwani ni CCM.
 
Back
Top Bottom