CHADEMA isianzishe kanda kwa papara...

CHADEMA isianzishe kanda kwa papara...

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,355
Naomba nitofautiane moja kwa moja na mpango huu wa chama changu wa kuanza kuzindua kanda kwa kuanzia kaskazini. Kimsingi naunga mkono hoja ya kupeleka madaraka kikanda ya CHADEMA. Hata hivyo, kama nilivyosema siku CDM inatangaza mpango huu, implementation yake uwe kwa umakini mkubwa sana ili isiwe na reputational impact kwa chama. Na hapa naona kama chama kimeshaanza kuvurunda.
Hoja yangu ni kwamba
  • kwa kuwa zipo kanda ambazo CDM, haijaimarika kama kanda ya kaskazini
  • kwa kuwa CDM imeimarika zaidi katika kanda ya kaskazini (idadi ya wabunge na madiwani wa kuchaguliwa ni ushahidi)
  • kwa kuwa maadui zetu wanatumia propaganda(dhaifu), kuwa CDM ni chama cha kikanda (ya kaskazini)
  • Kwa kuwa mwenyekiti na katibu wa CDM wanatokea katika kanda hii
  • kwa kuwa mpango huu wa kuanzisha kanda ni mgeni kwa CDM

Napendekeza kuwa CDM kisithubutu kuruhusu kanda ya kaskazini iwe ya kwanza kuzinduliwa kwa mpango huu.

Mpango huu uliasisiwa na uongozi wa juu wa CDM, na kiukweli, huku chini wengi wanasubiri kuelimishwa utendaji wake. Kwa kanda ya kaskazini kuanza moja kwa moja kuzindua mpango huu, tena akiwepo mwenyekiti, ni wazi kwamba CDM, hasa kwa maeneo ambapo haijaimarika sana, wameachwa kwenye mataa. Kesho na kesho kutwa kanda nyingine zitakapoanza kufanya mpango huu, bila kuelimishwa, watachemsha, na endapo wakienda kuelimishwa itaonekana kuwa wanaelimishwa kitu ambacho wametoka nacho huko kanda ya kaskazini, maana wao bila hata kuelimishwa wameweza kufanya hivyo.

Narudia tena, chonde chonde, mheshimiwa Mbowe, mheshimiwa Slaa, sitisheni zoezi la uzinduzi wa kanda yeyote kwa sasa, undeni timu ya watu maalumu, watakaoandika terms and conditions za uanzishwaji na uendeshwaji wa kanda za CDM, timu hii izunguke nchi nzima ikiwasomesha wadau viongozi, na baada ya hapo utaratibu wa kuanzishwa kanda uanzishwe, na usimamiwe kwa karibu na viongozi wa juu, na usianzie kaskazini.

Lakini pia tukumbuke kuwa ni majuzi tu katibu katangaza mpango kabambe wa M4C. Sasa endapo haya mambo hayatatekelezwa bila interactions za hali ya juu, then yanaweza kuleta negative impacts kwa chama. Hii ina maana kwamba viongozi (wote) kuanzia hivi sasa watakuwa bize na kuanzisha kanda, at the same time kuendesha M4C. Probably performance ya moja au yote itaathirika kwa kiasi kikubwa. Kwa kuwa suala la zonalization ni muhimu sana, then liendeshwe kwa umakini, na kusiwepo na papara yeyote. Viongozi, wanachama, na umma waelimishwe kwanza kuanzia sasa, na kwa maoni yangu zonalization ianze pengine mwakani, tena baada ya uchaguzi wa ndani wa chama.

This is a technical advice, mkitaka uchukueni, la hamtaki uacheni, but impacts zake mtaziona...
 
KASKAZINI KWANZA TANZANIA BAADAYE. We piga kelele tu lakini hakuna atakayekusikiliza. Ni sawa na kumshauri mtu aache dini yake.
 
Mkuu Tuko unajitahidi kweli kuwasaidia maadui wa Chadema propaganda za kijinga kabisa.Haya maneno uliyaleta kwenye thread ya Crashwise ukashindwa hoja umekimbilia kuanzisha thread mpya ya kitu kilekile.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Tuko ngoja nikuwahi kabla hujalala.Viongozi wetu walipoanza M4C kuvamia mkoa kwa mkoa wewe ni miongoni wa waliotoa ushauri kwamba operesheni hii isisimamiwe na makao makuu bali iratibiwe na watu wa maeneo husika.

Viongozi wetu wakaitisha Baraza kuu na kuamua M4C iratibiwe kikanda na sio makao makuu tena.Yaani ipelekwe kwa wanachama wenyewe.Na walioamua kumbuka ni Baraza kuu lenye wajumbe wa kutoka nchi nzima.Huu si uamuzi wa Mbowe wala Dr Slaa.

Utekelezaji wa Baraza kuu unaanza Mkuu wangu Tuko unasema hapana unashauri viongozi wasitishe.Kwa maana yako Baraza Kuu liitishwe tena lifute mpango wa awali lirudishe tena majukumu yote Makao makuu.Hii ni Haki kweli?

Kwanini tusivumilie kwanza tupate mrejesho baada ya miezi 6 ndiyo tuone mpango huu umefanikiwa ama haujafanikiwa? Baraza kuu limesema li takaa Septemba kupima mafanikio ya mpango huu kwa awamu ya kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Tuko tatizo lako unadhani kila mtu ana nia njema na Tanzania. Kuna watu wanajali maeneo fulani tu.
Watu kama wewe mnaojali nchi yote mmebaki wachache ndani ya chadema. Nakushauri ugombee uongozi wa kitaifa ili umsadie Zitto kataka kazi ngumu anayoifanya ya kukipa chama dira ya kitaifa...
 
Last edited by a moderator:
mda tulio nao ni mdogo so inabidi tujibanebane hadi tufanikiwe marengo yetu. hakuna kurudi nyuma coz hata kasikazini ni tanzania. sasa kwanini tuwabague wakaskazini? acha waanze frontline wengine watafuta. Uoga unaturudisha sana nyuma watanzania. mia
 
Mkuu Tuko kusema Chadema ianze kufanyia kazi utaratibu huu wa kanda mwakani ni kupotea njia.Hivi anajua uchaguzi wa Serikali za mitaa ni mwakani? Ni lazima mwaka huu ipigwe kazi ya kufa mtu.

Pili kuhusu uzinduzi kwanini uanzie Kanda ya kaskazini ni swali ambalo halina msingi wowote kwa sababu matayarisho yote yamefanywa na wanachama wenyewe bila ya kupewa hata senti tano na makao makuu.

Lakini nimfahamishe zaidi tu kwamba Kanda zote nyingine 9 ziko kwenye hekaheka kubwa za uzinduzi.Zitto alisema wiki iliyopita anashirikiana na Mzee Arfi na wanachama wa kanda yake na wako katika hatua za mwisho za uzinduzi.Pia nina taarifa kwamba kanda ya nyanda za juu kusini watazindua wakati wowote.

Labda aniambie kosa la Kanda ya Kaskazini ni kututaarifu wanaJF kinachoendelea kwenye kanda yake.Kwa hiyo wafanye kimya kimya.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Tuko ninachokiona kwako ni kile waingereza wanasema "fear of the unknown"
Kila mwanachama mahali popote alipo anawajibika kutekeleza matakwa haya ya kikatiba. Nakushauri na wewe hapo ulipo uhamasishe wanachama wenzako muanze utekelezaji wa mpango huu. Kadri navyofahamu kianda ya mashariki (Dsm, Pwani na Tanga) wanakutaja hivi karibuni kuweka taratibu za kuwapata waratibu ili shughuli za chama ziznze mara moja.

Kwahiyo kinachotakiwa kufanywa kwa sasa na wanachama wote nchi nzima ni9 kuhakikisha kwamba wanaanza kujipanga katika kanda zao na kupata waratibu wa muda ili kuandaa taratibu muhimu kwa uanzishwaji wa kanda ikiwa ni pamoja na makao makuu na ofisi. Ili sasa ndani ya muda mfupi ujao wapate waratibu wa kudumu na shughuli za ujenzi wa cha,ma ziendelee kama kawaida.

Kama kanda ya kaskazini wametangulia kuzindua kanda yao hiyo ni changamoto kwa kanda nyingine ili nazo zipige makasia kwa kasi kubwa na kuenenda na mahitaji tuliyonayo ya kukua kwa chama. Hizi tuhuma unazojaribu kuzitengeneza hapa ni kama vile wewe si mwanachadema kwaku unazungumza lugha inayozungumzwa siku zote na maadui zetu. Kila mara kufikiria na kuona kila kinachotoka ama kuanzia kaskazini kwa jicho la husda kunawafanya baadhi ya wanachama kujibweteka na kudhani kila kitu wafanyiwe na makao makuu, it;s your tuirn now to show that you are capable Tuko.

Mimi nawapongeza sana kanda ya kkaskazini na kwa muktadha huu nawataka waratibu wa kanda ya mashariki kuharakisha mchakato wa kupata waratibu wetu ili kazi ianze mara moja.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Tuko kama haya ndio mawazo yako wewe binafsi basi wewe hukitakii mema chama chako unachojinasibisha nacho, kwanza umeshafikiria juu ya muda mfupi sana tulionao kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka kesho? umefikiria juu ya zoezi la uchaguzi ndani ya chama mwaka huu, kama unayafikiria na kuyaona hayo siatarajii uendelee kushabikia kwa namna yoyote mkakati wowote ambao utatifanya tuingie mwaka 2014 tukiwa na viporo vya 2013.
 
Last edited by a moderator:
mkuu tuko unajitahidi kweli kuwasaidia maadui wa chadema propaganda za kijinga kabisa.haya maneno uliyaleta kwenye thread ya crashwise ukashindwa hoja umekimbilia kuanzisha thread mpya ya kitu kilekile.

ukweli unaumiza sana, hoja ya ndugu tuko ina ukweli mwingi, mbona nyinyi wengine munashida sana hamtaki hata wanachama wenzenu wakikikosoa chama chao, mnampiga vita. Wacheni kufunga macho penye ukweli.
 
Tuko tatizo lako unadhani kila mtu ana nia njema na Tanzania. Kuna watu wanajali maeneo fulani tu.
Watu kama wewe mnaojali nchi yote mmebaki wachache ndani ya chadema. Nakushauri ugombee uongozi wa kitaifa ili umsadie Zitto kataka kazi ngumu anayoifanya ya kukipa chama dira ya kitaifa...

Ukikua utaacha ufitini uzuri kila mtu anakufahamuwewe ni MR handle with care no wonder unakauka nyama
 
Ni vema sana ki mkakati kuanza na pale mahali penye nguvu kuliko kuanza na pale palipodhaifu. Ni busara kwa CDM kuanza Aruasha ndo uende Kanda nyingine. Naunga mkono!
 
Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, hiyo ikiwa ni mara ya pili (first time ilikuwa 2009) nilitoa changamoto hapa JF kwamba ni kwanini basi CHADEMA wasiitekeleze sera yao ya majimbo kwa kuanzia na majimbo ya kiungozi kwa chama badala ya kusubiria kushika dola! Nilisema kwamba, inaonekana wazi sehemu ambako CHADEMA imetoa viongozi ngazi za juu basi nako huwa wanakuwa na nguvu kubwa sana. Nikatoa mifano ya Kigoma, Arusha, K'njaro! Aidha, nikashauri kwamba viongozi waliopo ambao ni influencial kv Mnyika, Zitto, Heche, and the like ndio wawe viongozi wa awali kwenye kanda hizo bila kuangalia origin! Kwamba, eti kv Zitto anatoka KGM basi akaongoze kanda ya huko!! Kwamba viongozi watoke pale Kinondoni makao makuu na waende kuongoza kanda hizo mpya! Hii maana yake ni kwamba, endapo Watanzania wanavutika sana na viongozi wenye majina makubwa, basi uwepo wa viongozi hao kwenye kanda hizo unge-stimulate shauku ya watu kutaka kujiunga nao.

Hili, limefanyika and the pleasure is mine hata kama si maoni yangu ndiyo yaliyowafanya wao walete mpango huo! Pamoja na yote hayo, lazima nitamke wazi kwamba CHADEMA wamekurupuka na hawakutumia busara hata kidogo! Hakuna upungufu wa busara uliotumika kama kuanza na Kanda ya Kaskazini! Yaani hili limefanyika katikati ya tuhuma mzito kwamba CHADEMA ni chama kinachoendekeza ukanda! Mtoa mada ameita "PROPAGANDA DHAIFU!" Msijidanganye, hii si propaganda ya kupuuzwa hata chembe na itakuwa ni kituko kujiaminisha kwamba ni propaganda dhaifu wakati kila siku inaendelea kumea kwenye mioyo ya Watanzania! Na hali inakuwa mbaya zaidi pale CHADEMA wanapozindua jambo linaloashiria hizo hizo mnazoita propaganda dhaifu! It's very unfortunately, utawala wa awamu ya kwanza ulituaminisha kwamba utawala wa majimbo ni hatari kwa mustakabali wa taifa hili....this means that suala zima la utawala wa majimbo halifahamiki vizuri na Watanzania. So unapoanza na uzinduzi wa Jimbo la Kaskazini, kwa chama kinachotuhumiwa Ukaskazini, hapo bila shaka ni kuwapa gazeti la Uhuru best Headline of the Week!! So what, hapo Nape akisimama jukwaani na kusema "si mmeona, tuliwaambia kwamba hawa wana ajenda ya Ukaskazini....!!" je, mtamkejeli kama ilivyo silika yenu?!

Binafsi nilitarajia CHADEMA wangeanza na jimbo la Kusini kwa maana ile ile! Kwamba, pamoja na kujidanganya mnakojidanganya hapa jamvini kwamba mna wanachama wa kutosha nchi zima lakini ukweli bado unabaki pale pale kwamba kuna maeneo, hususani kusini; CHADEMA hamna chenu kule!! So kwa kuanza na Kusini, tena unamweka mtu kama Zitto Kabwe kuwa Katibu Mkuu wa Southern Province, basi sina shaka kwamba angebadilisha status ya maeneo hayo kwa hali ya juu sana! By the way, kuanza na sehemu kama hiyo ingetoa positive justification...! Sizani kama kuna jibu la kuvutia as to why mmeanza na Kaskazini lakini the answer could be short and clear kwamba mmeamua kuanzisha uongozi wa Kikanda na kuanzia Kusini coz' you don't have enough supporters kule!!
 
NASDAZ,

Suala la kwa nini kanda fulani ianze badala ya nyingine ni suala la Ratiba tu.Tukiogopa sana na kuchukua tahadhari pasipostahili ni kubariki propaganda za mahasimu wetu.Imefikia hatua sasa CHADEMA kichukue maamuzi bila kuogopa propaganda za maadui.Wakieneza uongo sisi tueneze ukweli hadi watakapochoka kueneza uongo

Hata kama tungeanza kanda ya kusini,bado wangesema tunajitafutia umaarufu kwenye suala la gesi.juzi maandamano yamefanyika na kuhitimishwa Temeke chama cha CUF(kama UPND ya Zambia) nacho bila aibu kinaibuka na kudai ni ngome yake

Sasa tusikubali tena kufanya kazi kwa kufuata midundo ya ngoma za mahasimu wetu.Tuendelee kuchukua misimamo mikali katika maamuzi yetu.Bravo CHADEMA,Aluta continua
 
Mkuu Tuko ninachokiona kwako ni kile waingereza wanasema "fear of the unknown"
Kila mwanachama mahali popote alipo anawajibika kutekeleza matakwa haya ya kikatiba. Nakushauri na wewe hapo ulipo uhamasishe wanachama wenzako muanze utekelezaji wa mpango huu. Kadri navyofahamu kianda ya mashariki (Dsm, Pwani na Tanga) wanakutaja hivi karibuni kuweka taratibu za kuwapata waratibu ili shughuli za chama ziznze mara moja.

Kwahiyo kinachotakiwa kufanywa kwa sasa na wanachama wote nchi nzima ni9 kuhakikisha kwamba wanaanza kujipanga katika kanda zao na kupata waratibu wa muda ili kuandaa taratibu muhimu kwa uanzishwaji wa kanda ikiwa ni pamoja na makao makuu na ofisi. Ili sasa ndani ya muda mfupi ujao wapate waratibu wa kudumu na shughuli za ujenzi wa cha,ma ziendelee kama kawaida.

Kama kanda ya kaskazini wametangulia kuzindua kanda yao hiyo ni changamoto kwa kanda nyingine ili nazo zipige makasia kwa kasi kubwa na kuenenda na mahitaji tuliyonayo ya kukua kwa chama. Hizi tuhuma unazojaribu kuzitengeneza hapa ni kama vile wewe si mwanachadema kwaku unazungumza lugha inayozungumzwa siku zote na maadui zetu. Kila mara kufikiria na kuona kila kinachotoka ama kuanzia kaskazini kwa jicho la husda kunawafanya baadhi ya wanachama kujibweteka na kudhani kila kitu wafanyiwe na makao makuu, it;s your tuirn now to show that you are capable Tuko.

Mimi nawapongeza sana kanda ya kkaskazini na kwa muktadha huu nawataka waratibu wa kanda ya mashariki kuharakisha mchakato wa kupata waratibu wetu ili kazi ianze mara moja.

The same Mwita Maranya i've known for couple of years now hapa JF.....the same Mwita Maranya ambae hamkubali kukosolewa!! Na mara nyingi u've similar justification: "Kila mwanachama mahali popote alipo anawajibika kutekeleza matakwa haya ya kikatiba. Nakushauri na wewe hapo ulipo uhamasishe wanachama wenzako muanze!" Mwita, say mie nimeamua kuiunga mkono CHADEMA just kwa kupitia sanduku la kura; kwanini unilazimishe kuingia kwenye uongozi na ama harakati za ujenzi wa chama moja kwa moja wakati sina interest kama hizo?! Why should you drag me to the playground I don't deserve? Usijidanganye, not everyone is motivated to become a political leader in any way, so it's up to wale walioamua kuingia kwenye uongozi ndio wafanye hayo unayotaka supporters wa kawaida wafanye! So, kama nyinyi viongozi hamuwezi kuyafanya hayo basi mfahamu kwamba hamfai or you're fit somewhere else and not as a frontline political leader. Kama wewe ni Mhasibu mzuri basi inatosha tu kufanya kazi ya kujitolea ya Uhasibu kwa chama chako badala ya kutaka kuwa kwenye political frontline while u're a weak fighter! If u're a good lawyer, provide legal advice to your party, that's it !! Don't go into the forest if you can't fight the wolf. Acheni kujidanganya kwamba spirit waliyokuwa nayo Watanzania katika kuiondoa CCM madarakani ni spirit ile ile kama ambayo walikuwa nayo Watanganyika kumuondoa Mkoloni! So, wale waliokata shauri la kuwa frontline leaders basi hawana budi ku-drive na kutekeleza jukumu hilo to the point they realise they're not fit for the positions!
 
NASDAZ,

Suala la kwa nini kanda fulani ianze badala ya nyingine ni suala la Ratiba tu.Tukiogopa sana na kuchukua tahadhari pasipostahili ni kubariki propaganda za mahasimu wetu.Imefikia hatua sasa CHADEMA kichukue maamuzi bila kuogopa propaganda za maadui.Wakieneza uongo sisi tueneze ukweli hadi watakapochoka kueneza uongo

Hata kama tungeanza kanda ya kusini,bado wangesema tunajitafutia umaarufu kwenye suala la gesi.juzi maandamano yamefanyika na kuhitimishwa Temeke chama cha CUF(kama UPND ya Zambia) nacho bila aibu kinaibuka na kudai ni ngome yake

Sasa tusikubali tena kufanya kazi kwa kufuata midundo ya ngoma za mahasimu wetu.Tuendelee kuchukua misimamo mikali katika maamuzi yetu.Bravo CHADEMA,Aluta continua

Nakubaliana na wewe lakini si busara hata kidogo kuzipuuza propaganda za CCM! Ben, wewe unafahamu fika athari za propaganda in political arenas!! The best way to deal with destructive propaganda is not to give ur rival a say! Kusini ni kama mfano tu, and I strongly agree with u kwamba wangesema u're looking for cheap popularity lakini bado kuna maeneo mengi ambako mpango huo ungeanzia but NOT NORTHERN ZONE!! Propaganda has proved to be the best fighting tool in any political battle so kupuuza propaganda pasipo na kuwa na mikakati ya kukabiliana nazo ni sawa na kujipeleka kwa simba aungurumae kwavile tu ulipata kusikia ya kwamba "simba mpole ndie mla watu!" Unamposikia Mwenyekiti wa Chama na wakati huo huo ndie Rais anawaagiza vijana wake waanze kujibu kila kinachosemwa na/au kuandikwa na wapinzani basi ufahamu tayari wameshakuwa badly defeated na propaganda zenu.
 
Hoja Nyepesi sana kijana, Mimi nawasupoti waendelee hivyohivyo na hiyo ndio dawa ya Ukanda na Udini kwani kila kanda itakapo pewa uwezo wake wa kimahamuzi na kiutawala, hoja dhaifu ya ukanda itakuwa chali na pia ya udini itafifia.
Maji yako sasa :-
1. Ni kweli kuna kanda ambazo hazijaimarika na imekuwa hivyo kwa vyama vyote vya upinzani na kwa Chadema ni miaka 20 sasa na hawajafanikiwa na dawa ya kuimarisha hizo kanda nyingine ni hii ya kutambua uwepo wa hizo kanda na kanda zote zikipata resource sawa naamini mambo yatabadilika. Ila kumbuka hata hiyo Kaskazini unayosema imeimarika is kweli Tanga, Moshi, Manyara Chadema bado hawapo sawa kihivyo hata hiyo arusha yenyewe bado sana. Tatizo unaangalia Arusha mjini tu.

2.Nadhani nishakujibu hapo juu, kwa kifupi tena ni kuwa chadena Tanga, Manyara Moshi bado sana.

3. Jibu ya hoja zote ni hili la kabda ndungu yangu kwani tabia ya kuamini kuwa chgadema ni makao makuu tu, wakati wake wa hoja hiyo kufa ni sasa, kwani kanda zikishamiri ni kuwa mtakkosa hoja maana itakuwa chadema ni nchi nzima na Inshalaah pengine hili linaweza kusaidia chadema kuwika pemba ambapo ccm wameshindwa kwa miaka yote. Nadhani hata wao hawana hata Diwani huko pemba.

4. Nadhani pia nimeji u hapo juu kwani sasa chadema inaonekana ni mwenyekiti na katibu tu, kitu ambacho is kweli, mikoani kuna viongozi wengi wenye uwezo wa kuwika lakini walifunikwa kwa sababu ya huu utaratibu wa chama makao makuu, na wakati ni wao sasa kutokelezea.

5.Mpngo mgeni, Sijuhi unaumri gani au umeanza kufuatilia siasa lini ndugu yangu ila mimi nayeijua chadema tokea miaka ya 90 na slogan yao ya Chademaaaa, VyemaaaaA!! Najua kuwa hii ni sera yao na wamekuwa wakihubiri miaka yote, na sasa wameamua kuifanya kwa vitendo.
Kiukweli kushindana na Ma CCM inahitaji resource nyingi sana na hili la kutegemea makao makuu kuhamasisha chama nchi nzima kiukweli sio zuri na tumeona jinsi hali inavyokuwa mbaya endapo makao makuu wakishambuliwa na wapinzani wao.

All in all ndugu yangu tuwaunge mkono Chadema kwenye jambo hili na tuwaombee mungu wapate makamanda wa kweli wenye kujitoa muanga na kujitambua ili Ma CCM watoke madarakani na tuone wqengine watatutendea nini.

Na sisi wakosoaji tuendelee kuwa hukumu na kuwashitaki kwa wanachi hata hao chadema watakapo fanya vibaya.
 
Tuko tatizo lako unadhani kila mtu ana nia njema na Tanzania. Kuna watu wanajali maeneo fulani tu.
Watu kama wewe mnaojali nchi yote mmebaki wachache ndani ya chadema. Nakushauri ugombee uongozi wa kitaifa ili umsadie Zitto kataka kazi ngumu anayoifanya ya kukipa chama dira ya kitaifa...
Sijui ni lini ulianza kuwa na mapenzi na CHADEMA maana post zako zote humu zinakutambulisha kama kundi la kwanza lisiloitakia mema CHADEMA na chama chako unajitambulisha Nacho.Unadhani ushauri wako unaweza kuchukuliwa serious kiasi hicho na wapenda mabadiliko?
ukweli unaumiza sana, hoja ya ndugu tuko ina ukweli mwingi, mbona nyinyi wengine munashida sana hamtaki hata wanachama wenzenu wakikikosoa chama chao, mnampiga vita. Wacheni kufunga macho penye ukweli.
Mkirindi,

Kuwa makini,jaribu kusoma post za nyuma za mtu kabla hujahitimisha kwamba huyo mtu ni mwanachama wa CHADEMA.Pia kuhusu suala la kukosoa kwa kweli nakuunga mkono lakini ukosoaji wenye lengo la kutimiza matakwa ya propaganda za mahasimu wetu unakua sio ukosoaji wenye nia njema tena
 
Nakubaliana na wewe lakini si busara hata kidogo kuzipuuza propaganda za CCM! Ben, wewe unafahamu fika athari za propaganda in political arenas!! The best way to deal with destructive propaganda is not to give ur rival a say! Kusini ni kama mfano tu, and I strongly agree with u kwamba wangesema u're looking for cheap popularity lakini bado kuna maeneo mengi ambako mpango huo ungeanzia but NOT NORTHERN ZONE!! Propaganda has proved to be the best fighting tool in any political battle so kupuuza propaganda pasipo na kuwa na mikakati ya kukabiliana nazo ni sawa na kujipeleka kwa simba aungurumae kwavile tu ulipata kusikia ya kwamba "simba mpole ndie mla watu!" Unamposikia Mwenyekiti wa Chama na wakati huo huo ndie Rais anawaagiza vijana wake waanze kujibu kila kinachosemwa na/au kuandikwa na wapinzani basi ufahamu tayari wameshakuwa badly defeated na propaganda zenu.

Thank you,

I agree with you kuwa njia bora ya kupambana na propaganda ni kutompa nafasi adui/hasimu wako ya kuieneza kwa urahisi na kuepuka mambo yanayochochea propaganda.Katika sayansi ya Siasa zipo aina 3 za propaganda ingawa mbinu zake zimeongezeka juzi na njia bora ya kukabiliana nazo kwenye kitabu cha Prof.Ben D'Moir

CCM na vyama hasimu pamoja na vikundi vichache vimekua vikitumia propaganda ya kijivu (kuchanganya Uongo Mwingi na kupotosha ukweli kidogo in their favour) na kuufanya uonekane ndiyo ukweli mtupu.Kitengo chao cha propaganda kime-fail miserably na sasa wanahama katika ule mkakati wao wa kutumia propaganda ya kijivu sasa wanatumia propaganda nyeusi(Kusema uongo waziwazi na kwa ujasiri ili kulazimisha umma uamini kuwa ndiyo ukweli) na hata hivyo kwa bahati mbaya aina hii ya propaganda wangeitumia kipindi kile ambacho watanzania wengi hawakuwa wameelimika,kipindi kile ambacho tulipotoka tu kwenye mfumo wa chama kimoja.Sasa hivi si Rahisi kuitumia propaganda hii na wamefanya opposite ya walichotakiwa kufanya muda huu.Siwapi siri

Propaganda ya ukabila haina nguvu tena hata waseme kitu gani.Imeshachuja.Sasa hivi wanatumia mbinu zilizopitwa na wakati katika propaganda Card stacking(hawataki bunge lionyeshwe,hawataki CHADEMA watoe elimu ya Uraia ili kuwanyima wananchi taarifa na kuelimika),Namecalling imepitwa na wakati.Testimonials-Inajulikana kuwa hivi karibuni watawatumia wale waliohamia huko juzi baada ya kufukuzwa kuzunguka nchi nzima kueneza propaganda hii.Wathubutu waone,tutawafuata wananchi kuwaeleza ukweli.CCM inawatumia vijana wao akina Nape na Mwigulu wanaosoma vitabu vya IPA(Institute of propaganda Analysis) ambazo ni nadharia zilizovumbuliwa tangu mwaka 1938.Sisi tunaenda na trend na latest version ya nadharia mpya zilizovumbuliwa juzi baada ya Arab spring na nyingine zilizovumbuliwa kwenye trend ya kampeni za uchaguzi wa Marekani,Zambia,Ghana,Georgia,Russia na Venezuela.Wakitaka tutawaazima vitabu hivi ili wafanye propaganda za kistaarabu bila kuhatarisha Umoja wa kitaifa

Sasa hivi Propaganda walizozifanya vibaya kisiasa zimehama zenyewe kwenye vyama vya siasa zimehamia kwenye Dini.Hapa wanapambanishwa jamii ya watanzania wa dini mbali mbali dhidi ya wenzao kutokana na ukatili wa wanasiasa waliofeli.Now you can see how another propaganda has taken over minds of innocent Tanzanians

CHADEMA kimeweza kukabiliana na propaganda dhidi yake muda wote na kuchukua tahadhari.Sasa kazi ni kuendelea kuelimisha umma ili hawa wanaotoka madarakani wasituachie nchi ambayo ipo katika vipande vipande.Ni jambo baya na ukosefu wa uzalendo kuchochea udini na kuiacha jamii ikiwa imeharibika vibaya kisa unajua unatoka na unataka kumuharibia anayekuja kuongoza.CHADEMA sasa kinafanya kazi ya kukiondoa CCM na pia kuhakikisha kwamba hawatumia njia hii ya mpito kuvunja taifa.Kazi ya kuijenga tutaifanya sisi kwa hiyo kwa kuwa CCM wameonyesha kuwa careless na kukosa uzalendo basi ni lazima tuwasimamishe katika mpango huu wa kuhujumu uongozi mpya utakaochukua dola 2015 kutoka upinzani.Healing social fabrications is not easy.Kagame alipata Shida sana kuijenga upya Rwanda
 
NASDAZ,

Suala la kwa nini kanda fulani ianze badala ya nyingine ni suala la Ratiba tu.Tukiogopa sana na kuchukua tahadhari pasipostahili ni kubariki propaganda za mahasimu wetu.Imefikia hatua sasa CHADEMA kichukue maamuzi bila kuogopa propaganda za maadui.Wakieneza uongo sisi tueneze ukweli hadi watakapochoka kueneza uongo

Hata kama tungeanza kanda ya kusini,bado wangesema tunajitafutia umaarufu kwenye suala la gesi.juzi maandamano yamefanyika na kuhitimishwa Temeke chama cha CUF(kama UPND ya Zambia) nacho bila aibu kinaibuka na kudai ni ngome yake

Sasa tusikubali tena kufanya kazi kwa kufuata midundo ya ngoma za mahasimu wetu.Tuendelee kuchukua misimamo mikali katika maamuzi yetu.Bravo CHADEMA,Aluta continua
Well Said Comred
 
Back
Top Bottom