CHADEMA Iringa wamjia juu Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Iringa wamjia juu Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asha Abdala, Apr 12, 2009.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  na Francis Godwin, Iringa
  ZIKIWA zimepita siku chache tangu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Said, kuifuta mahakamani kesi ya Diwani wa Kata ya Itunundu-Pawaga, Philipo Mkumbata, aliyekuwa akituhumiwa kuhujumu miundombinu, kwa madai kuwa kumfikisha mahakamani diwani huyo ni kuwapa nguvu wapinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Iringa, kimeonyesha kulipinga agizo hilo kwa kumtaka kulifuta.

  Akitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa, Mwigongo Kapwani na Katibu Pascal Bella, walisema wamepokea kwa masikitiko makubwa agizo hilo la Waziri Mkuu na kuweka bayana kuwa jambo hilo ni kuingilia uhuru wa mahakama.

  Kapwani alisema wanaamini kuwa katika kushughulikia suala hilo Waziri Mkuu amedanganywa na baadhi ya watendaji waliokuwa na malengo ya kisiasa zaidi lakini pia agizo hilo limemdhalilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Said, kwa kumfanya aonekane kiongozi asiye na mamlaka baada ya kuruhusu diwani huyo afikishwe mbele ya sheria.

  “CHADEMA inaamini kuwa mahakama ndicho chombo cha mwisho cha kutafsiri sheria na kwamba hakipaswi kuingiliwa utendaji wake kwa misingi ya ushabiki wa kisiasa, na kwamba diwani huyo ni mhalifu kama wahalifu wengine, hivyo Pinda hakupaswa kumtetea bali alitakiwa kuacha sheria ifanye kazi yake,” alisema Kapwani.

  Kapwani alisema kuwa Waziri Pinda anataka kutoa tafsiri mbaya kwa wananchi ambao walianza kuwa na imani kubwa na utendaji kazi wake katika kushughulikia masuala mbali mbali ya nchi bila ubaguzi, ila kwa picha aliyoionyesha Iringa imemvurugia imani hiyo iliyoanza kujengeka.

  Hata hivyo alisema kuwa bado Pinda ana nafasi kubwa ya kubatilisha uamuzi wake, kwa sababu suala lolote lililopo mahakamani halipaswi kuongelewa au kutolewa uamuzi nje ya mahakama.

  “CHADEMA tunataka kesi hiyo namba 335/2008 iendelee kama ilivyoanzwa kusikilizwa na kwa sababu mali iliyoharibiwa ni ya Watanzania wote na si mali ya CCM,” alisema Kapwani.

  Naye Katibu Pascal Bella, alisema wana tuhuma nyingi za diwani huyo na wapo tayari kuzitoa na hapaswi kupewa msamaha na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kama inavyofanyika hivi sasa.

  Bella alisema wapo tayari kuwasiliana na uongozi wa taifa wa CHADEMA ili kuhakikisha suala hilo linakwenda kwa misingi ya sheria na kuondokana na mizengwe iliyoanzwa kufanywa hivi sasa kwa lengo la kupindisha sheria ili kulifanya liwe la kisiasa.

  Alisema ni vema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akawa makini zaidi na matamshi yake anapofanya ziara mikoani ili kauli zake zisije zikamsababishia matatizo mbele ya jamii ambayo ina imani na utendaji wa kiongozi huyo.
   
 2. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nyie CHADEMA mna nini na Pinda? Kila siku kumfuata fuata kuhusu kauli zake. Mara maalbino. Mshindwe na mlegee, Pinda ni waziri mkuu anayefuata misingi ya Nyerere. Pinda ni kama Sokoine

  .....ndiyohiyo
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na wewe ...ndiyo hiyo una kisa gani na CHADEMA?
   
 4. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  CHADEMA nao hawakuwa makini katika kemeo lao hili, upinzani nchini kwetu kwa kweli umechoka. Pinda hakuingilia "tafsiri za sheria" za mahakama. Pinda hakuagiza hakimu aseme mtuhumiwa hakuvunja sheria. Ameagiza kesi iondolewe mahakamani. Ukigombana na ndugu yako halafu baba yenu akamwagiza mmoja akafute kesi mliyofunguliana mahakamani huyo mzazi atakuwa hajaingilia mahakama, ila ameingilia ugomvi wa hawa ndugu kwa kuwaagiza wakaondoe kesi mahakamani, isipokuwa kama Baba yao amemwagiza hakimu afute kesi.

  Tatizo hapa, kosa la Pinda, ni kuonyesha kwamba hajali vitendo vya jinai iwapo vimetendwa na CCM mwenzake. Hajali uhujumu na uharamia wa mali ya umma, kwamba wavunja sheria wa CCM wasipelekwe mbele ya sheria. Hiyo sio "kuingilia utendaji...tafsiri ya sheria."

  Upinzani wetu unalegalega kwa sababu wanashindwa kuelezea udhaifu wa CCM wakaeleweka na wananchi.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Na wewe una statement kama za hao SISI Mafisadi. Umeanza maelezo yako vizuri tena ukiwa unaeleweka. Lakini hayo maandishi mekundu yamekuangusha kabisa kwa sababu husemi ukweli kwa kauli hiyo. Yamenitia kinyaa maana naweza tapika.
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Pinda naona kama anachemka maana anadhani mali ni ya CCM kumbe ni mali ya wananchi .Huyo ni diwani wa watanzania wa eneo hilo kwa ticket ya CCM na si Diwani wa wana CCM pekee hadi aingiwe na hofu .Misingi ya mwalimu hapa ni ipi ?
   
 7. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu Asha,
  Mimi bado ni kihiyo wa computer,naomba uweke pia maoni ya wasomaji yaliyopo chini ya habari hiyo kuongeza utamu wa mjadala huu.
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  habarindiyohiyo sijaelewa unachosema.PM anapokuwa anaongeaongea na kutoa maagizo yasiyo na mantinki i doubt about his capacity in making judgements before he spoke things
   
 9. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pale pale pa mwanzo Kwahiyo ina maana alitoa matamshi na hayaja tekelezeka?

  Maoni yangu hii ita unfold kidogo...labda kuna mengine, only time will tell.

  Na kama hayo yametekelezeka basi Waziri Mkuu ni cheo kizuri sana:D Yaani kama Yule jamaa anayeonekana nakutokuonekana (Invisible)akiamua anawadhalilisha ma mods wake halafu anawarudisha wale wanaopayuka!(Walio kuwa banned) Wapayukaji!

  Kwa kweli Mh. Pinda atakuwa ndie yule tu wa kupindisha pindisha sheria!:D
   
Loading...