Logo
Nitatumia fursa hii kujibu sehemu ya pili ambayo bila shaka unataka kuendeleza malumbano na Katibu Mkuu bila sababu yoyote. Sitakujibu ile sehemu ya kwanza kwa sababu tayari umeshajibiwa.Mtu akikusoma vyema, hasa baada ya comment yako ya pili, anakuona kama mtu mpenda mabadiliko. Kwenye comment yako ya awali mtu angeweza kukuona kama mpenda mabadiliko na mwana CHADEMA!
Lakini baada ya kurudi kwa nia ya kulumbana na Katibu Mkuu (wako?) ni dhahiri hauko kwenye kundi la wanachama.Tuje kwenye hoja yako ya pili, baada ya ile ya kwanza kujibiwa. Hivyo nitakujibu kama mtu unayetaka kuonesha kuwa unapenda mabadiliko. Ingawa hujalionesha hilo wazi, hivyo hata hiyo 'penda' yako inaweza kuwa tooo questionable.Kweli ni bahati mbaya sana kuwa mtu kama wewe unayeonekana unapenda mabadiliko ya dhati unashindwa kutambua wajibu ambao viongozi wa CHADEMA, kwa kushirikiana na wanachama na wafuasi wa chama wamekuwa wakitimiza kwa ajili ya kuwapigania Watanzania!
So unataka kuonesha kuwa hujui kesi ambazo zinawakabili viongozi kadhaa waandamizi wa juu kule Arusha (kabla hazijazuiwa baada ya kufunguliwa kesi nyingine ya kikatiba) zilikuwa zinahusu kuipigia makofi CCM kwenye mikutano ya hadhara!?!? Hujui kabisa kuwa mbili zinatokana na wao kushiriki wakiwa mstari wa mbele kwenye maandamano ya Januari 5, kupigania haki ya watu wa Arusha kumpata Meya aliyechaguliwa kihalali, bila kujali anapatikana kutoka chama gani!
Aidha, unataka kuinesha hujui kuwa nyingine inatokana na mkesha wa Novemba 7 wakati wa sakata la Lema kuwa mahabusu! Tena ilikuwa baada ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Lissu na viongozi wengine, kuwaongoza maelfu ya wanachama na wafuasi kushiriki mkutano huku mvua kubwa ikinyesha.
Ni mkesha huu ambapo CCM waliona wazi Tahrir Square inanukia...Unataka kuonesha kuwa hujui kuwa viongozi waandamizi wa CHADEMA wameshtakiwa pamoja na wanachama na wafuasi wa chama hicho Mahakama ya Wilaya Mufindi baada ya tukio la Nyololo, eti wakishtakiwa kwa mkusanyiko usio halali, wakati walikuwa wanafanya vikao vya ndani, baada ya kufungua matawi, kabla polisi hawajamuua Daudi Mwangosi! Mmojawao ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Mussa Yusuf.
Je unataka kuonesha kuwa hujui viongozi wa CHADEMA (wa juu, wa kati, wa chini) wamekuwa wakipambana bega kwa bega na wananchi, wanachama na wafuasi wa chama hicho kupigania haki na matumaini ya wananchi wanyonge kila mahali, hivyo kujikuta wakikamatwa pamoja na kufunguliwa mashtaka yasiyokuwa na kichwa wala miguu, kwa nia tu ya kusumbua na ku-distabilize vuguvugu, iko migano mingi tu, huko Tarime, hapa Dar es Salaam, Masasi, n.k, n.k, n.k, n.k, n.k, maeneo ni mengi kwa maana ya kwamba ni nchi nzima. Nilichofanya ni kukupatia samples tu...
Hakuna wakati CHADEMA imewahi kupoa. It has been always active, kila wakati kwa namna tofauti, kwa agenda tofauti au zile zile, alimuradi kwa ajili ya kuwatumikia au kutoa utumishi bora kwa watu. Hivyo hoja yako kuwa kuna CHADEMA ya zamani na mpya, haina mashiko hata kidogo, unless imejengwa katika msingi mbovu wa hoja, bila ushahidi yakinifu. Ukisema hivyo utaulizwa, zamani inaanzia lini hadi lini na 'sasa' (mpya yako) inaanzia lini hadi lini.
Ungemsoma Katibu Mkuu Dr. Slaa vyema kwa utulivu ungeweza kuona ujumbe mzito aliokupatia kuwa si lazima kutumia mbinu ile ile kila wakati kumkabili adui yule yule. This is war. You need Tsa Nzu kaka. Mkuu Logo, hao wachache ambao wewe unawabeza na hao unaowaita wavuta bangi na wasiokuwa na kazi (shukuru wewe unayo na bangi huvuti) ndiyo jeshi la ukweli. Ndiyo wapiganaji wa ukweli. Wanajua wanachokipigania. Wanajua wajibu wao. Wanajua nidhamu ya jeshi ni kumlinda kamanda, si kuombea ukamatwe pamoja na kamanda.
Sasa kamanda naye akikamatwa nani apiganishe vita au unataka morale ishuke na adui ashinde!?!? Kaka hizi ni principles za kawaida kabisa katika medani za vita.Hao unaowabeza na kuwaita wachache, ndiyo kila siku wakija kwenye mikutano, wakija kwenye maandamano, wakiandika hapa, wakitoa maoni yao kwenye sanduku la kura, wakihoji mambo kila mahali, serikali ya CCM na chama hicho wanazidi kupata hofu! Wanatetemeka.
Hakuna wakati katika maisha ya siasa za upinzani na kudai mabadiliko na uhuru wa kweli, CCM imewahi kupata hofu kama inayoonesha sasa. Imefikia mahali wanaogopa hata kuitisha uchaguzi wa vijiji na vitongoji! Kwa sababu wanajua CHADEMA imetapakaa kila mahali, wananchi wameijua na wameikubali, wamekataa propaganda zote, zote kabisa za watawala, ikiwemo hii ya sasa ya ugaidi.Hao ambao wewe unawabeza, ndiyo waliokwenda kupiga kura za mabadiliko kwenye uchaguzi mkuu uliopita. Ndiyo waliolinda kulinda bila kujali mabomu, silaha na kila hila za watawala wakilitumia Jeshi la Polisi. Ni bora jeshi la watu wachache wanaotanguliza moyo mbele kabla ya silaha.Wanotanguliza dhamira ya dhati kabla ya maslahi.
Ni wale wanaoona wanachopigania si kwa ajili ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu, au kiongozi yeyote. Wanaona bigger picture, wanaiona Tanzania na Watanzania wanahitaji ukombozi, wanahitaji uhuru, wanahitaji haki, wanahitaji matumaini. Wanahitaji mabadiliko ya kimfumo na kiutawala.
Wakati wewe unadiriki hata kusahau kuwa viongozi wa CHADEMA wa ngazi zote wamekuwa mstari wa mbele kupigania haki, sambamba na wanachama na wafuasi wa chama, wenzako hao wanataka mabadiliko ili wasivute hizo bangi na wapate hizo kazi ambazo sasa hawana kutokana na sera mbovu za CCM zilizoshindwa na ufisadi uliokithiri hadi kuachia mianya ya viongozi kushirikiana na wauza mihandarati ambayo ndiyo vijana unadai wanavuta!
Yote uliyoyasema huwezi kuyatenganisha na ubovu na kushindwa kwa utawala unaoporomoka wa CCM.Watu hawako mahabusu, magerezani au mahakamani kwa sababu ya maandamano. Tangu lini maandamano yakakamata watu! Watu wako huko kwa sababu serikali hii ya CCM imeamua iwe hivyo.
Kwa sababu sasa ukionekana kuhoji, kuuliza maswali magumu, kudai haki, kutetea matumaini ya wanyonge, kupinga unyanyasaji na dhuluma za watawala dhidi ya wananchi, kwanza unakuwa lebeled, kisha unabambikiwa kesi. U give a dog bad name before u kill it. Lakini Watanzania wanaangalia na wanajua kuwa CCM haiwezi kufanya tena siasa. Haiwezi kujibu hoja kwa hoja, bali matusi na kutengeneza propaganda.
Zikiwemo za kupalilia udini, ukanda na ukabila bila kujali kama taifa laweza kuparanganyika. Kwa sababu kile si chama cha siasa tena. Kilichobaki pekee ni vitisho, manyanyaso na hata kuua, ili kuwatisha wapigania mabadiliko. Hivyo watu wanahoji kwenye maandamano, mikutano au kwenye vyombo vya habari, wanafuatiliwa, wanakamatwa, wanafungwa na kunyanyaswa. Badala ya kuwatisha, hiyo imekuwa ikiongeza mori na hasira na ukubwa wa jeshi la wapambanaji.
Maandamano ya CHADEMA ni moja ya forums ambayo Watanzania wameiamini na kutumaini kuwa ndiyo mahali pa kutoa hisia zao za kutofurahishwa na status quo. Sehemu ya kuendeshea haraki za kuuondoa mfumo huu unaoatamiwa na CCM, ukilea ufisadi na ubadhirifu, matokeo yake kukwamisha maendeleo.
Na kwa sababu hiyo forum haijawahi kuwaangusha wala kuwatupa, imekuwa nao kwenye kila hali, wataendelea kuiamini na kuitumikia ili nayo iwatumikie vyema, hadi kieleweke. Na kitaeleweka.Hivyo kamanda Logo, usikate tamaa. Usipungukiwe kama wewe ni miongoni mwa wapiganaji kweli. Pigania Tanzania na Watanzania. Hila za kuulinda mfumo huu mbovu, kukilinda chama kilichokwisha kuacha misingi yake na kinaporomoka kwa kasi ndiyo maana tuna serikali legelege, ziko nyingi sana.
Hivyo CHADEMA lazima wawe na mikakati anuai pia ya kupambana (pro-active na reactive) huo ndiyo ujumbe mkubwa na mzito aliokupatia Katibu Mkuu, Dr. Slaa. bahati mbaya hukuelewa. Kuiondoa CCM madarakani si harusi mkuu. Tushikamane na twende pamoja.
Makene
0752 691569 /
0688 595831