Logo na WanaJF,
Awali niombe radhi kwa usumbufu mliopata kutokana na Reply yangu ya Jana kwa thread aliyoanzisha Logo. Ni kweli jibu lile ni la kwangu.
Nimepata tatizo na network na hata sasa ninajaribu ku post kwa Mara ya tatu, nikitumaini kuwa labia nitafanikiwa. Network imenisumbua sana na Kama mmetazama kwa makini jibu lilikuwa na 1) kuashiria kuwa ilikuwa inaendelea. Naomba niweke wazi kabisa kuwa nimejibu kwa ukali kwa misingi ifuatayo.
I) kusema chadema ipo hatarini ni kuamsha hofu ya lazima. Katibu Mkuu makini, hawezi kuachia hofu inajengwa miongoni maw wanachama wake na yeye akakaa kimya. Siyo. katibu Mkuu wa Chama makini Kama Chadema.
2) kukitaka chama kiitishe mkutano mkuu si jambo dogo. Kinachoonekana ni kuwa mhusika hata nafahamu Katiba ya Chadema na wala hakujisumbua kuitafuta. Si kitu haijui, basi angalau angelipiga hata simu au kuwauliza wail karibu naye, jambo ambalo hakufanya. Ni vigumu sana kushauri wakati hujui hata abc ya Chama husika.
3) Logo anasema wananchi wameanza kukata tamaa. Nimemhoji Logo, anazungumzia wananchi wa wapi? Wakati Chadema wanazidi kukasirika dhidi ya vituko vinavyofanywa na Serikali ya CCM? Sisi tunahaki ya kusema wananchi kwa kuwa ni juzi tu tumefanya maandamano na mikutano mikubwa ya hadhara. Logo anazungumzia wananchi gani. Hizi zinaitwa fallacies katika falsafa, na Katibu Mkuu makini siwezi kuacha kukemea Kama nitakavyoeleza pia hapa chini. Ni vema logo afahamu kuwa kila siku tunawatuliza kuonyesha hasira Yao dhidi ya Serikali. Kuna siku itafika na sisi tutachoka, na tutawaacha wafanye wanalotaka. Kwa bahati mbaya TISS wanajua Hali hails na hasira ya wananchi lakini sina hakika Kama wanafikisha unwell kwa Rais. Kuna siku watajutia!
4) Logo anakejeli kauli kuwa " tuna Mungu".... Hata siku mmoja siwezi kuwa na huruma na mtu anayemkufuru Mwenyezi Mungu. Angelikuwa sahihi Kama Chadema ingetamka tu hiyo kauli na kukaa bila kufanya kazi. Hata hapa ninapoandika, timu za Chadema ziko kazini, sasa Logo anaongelea Chadema ipi! Labda kama Ana ya kwake anayoifikiria kwa malengo tusiyofahamu.
5) mwisho anasema " amkeni"... Tafsiri yake nini. Haya ndiyo yaliyonifanya nijibu kwa ukali lakini bahati mbaya majibu yakakatika njiani.
Hivyo basi kwa taarifa tu ya Logo na wapenzi wetu ambao wamepata usumbufu.
a) utafiti unampa mtu uhalali wa kuzungumza. Logo au hajafanya utafiti, au kakurupuka, au Ana agenda ya siri. Kitendo cha kuficha jina lake la kweli, na kuwa kaonyesha kutojua katiba ya Chadema inanipa wasiwasi wa Nia na malengo yake hailisi.
b) katika jibu langu, poppet sikusema maandamano hayafai, wala sasa basi Kama winging walivyoandika. Hoja yangu ni kuwa, Maandamano na mikutano ya hadhara siyo njia pekee ya kuhamasisha watu wala kuwaelimisha. Chama makini ni lazima kiwa bunifu. Kwa kuwa Logo hakufanya utafiti wowote, kabuki na mawazo ya 47, kuwa kwa kuwa mbinu ya Chadema huko nyuma ni maandamano, basi itakuwa hivyo milele. Huu ni upungufu mkubwa wa kutofanya utafiti na huwezi kushauri wakati hujui unamshauri anajua nini na anafanya nini.
c) Logo Kama Ana nia njema asingelisahau kuwa ni takriban miezi miwili tu, tangu niliposema, Chadema imefanikiwa katika malengo yak ya maandamano kwa asilimia 99.99999. Huhitaji kwenda shule kuelewa Katibu Mkuu aliyetoa kauli hiyo juzi tu, leo hawezi kugeuka. Tatizo la utafiti au la kutofuatilia kwa makini matukio ya kisiasa. Siyo kosa langu, na mtu ambaye anajiweka mshauri, ten a kwa kauli nzito Kama alizotoa Logo, au ni mzembe au hafuatilii isipokuwa tu yenye kumfurahisha yeye. Hakuna maelezo yeyote ya kistaarabu isipokuwa kumjibu kuwa bado anafikiri ki mwaka 47, na Hilo sikulitamka kwa bahati mbaya, nalirudia tena. Mwanachama asiyefahamu na dhamira ya kushauri unamtambua fika, ndiyo maana ya kuzomea falsafa, logic, metaphysics, cosmology na kadhalika. Nawasikitikia wanaobeza elimu ya udaktari wakati hawajui wanazungumzia nini. Mungu awasamehe Kama nia Yao ni njema. Siku hizi unaweza kuingia tu kwenye Google ukajua Kama mtu Ana dhamira ya kujua.
d) Logo angelipenda kusema ukweli kuanzia mwisho wa February hadi wiki mbili zilizopita kwenye uzinduzi wa Kanda ya Kaskazini, Ziwa Magjaribi, Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Ziwa Mashariki, kite kumefanyika maandamano makubwa yakifuatiwa na Mikutano mikubwa ya hadhara. Kama hakufuatilia ni tatizo lake, lakini kamwe Hana phalli wa kupotosha umma wa Watanzania, wala kuwatisha kuwa Chama chao ambacho ni ztumaini jipya kiko "Hatarini". Nitajuaje Logo kuwa ni mbwa mwitu kava a tu ngozi ya kondoo, au panya anayeuma na kupooza. Mwanachedema hails anafuatlia matukionya chama chake, na Kama kuna kitu hajui Ana PM, au ana pig simu. Si utaratibu aliotumia Logo.
e) Logo angelikuwa mtafiti na mshauri mzuri, angegundua kuwa chaguzi zote ndogo baada ya Arumeru, Chadema imekuwa ikiinyanyasa CCM hata Kama si kwa kushinda overall, lakini tumewanyanganya vijiji vingi na vitongoji, wajumbe wa Serikali kwenye gnome zao kiasi kuwa Leo hakuna tena unachoweza kukiita "gnome ya CCC" kona zote za nchi. Mapigonya hivi Karibuni ni Chato, Muleba, Mbeya, Ruvuma,Rukwa/katavi na Lushoto Jumapili iliyopita. Kwa huo kwenye gnome za CCM mwanachadema makini, ten a anayejivika ushauri atatumia lugha ya Chadema ipo hatarini". Hawa ingelikuwa vitabu vitakatifu ni wale walioitwa "manabii wa uwonga", na chadema muda wala nafasi kwa manabii wa uwonga. Hii haina maana ya kukataa ushauri, lakini ushauri ni tofauti na upotoshwaji wa makusudi, kukatisha tamaa na kuwatisha wanachama wetu. Kwenye vitabu vitakatifu, hawa ni wale ambao tumeambiwa wafungiwr mawe shinbone na kutipwa baharini kwa sababu madhara Yao ni makubwa mno.
f) Logo sina Imani hakusoma magazeti wala Tv juzi nilipoweka sauna mbele ya vyombo vya habari na kutangaza kuwa msaada tuliopata kwa Conservative Oeoples Party of Denmark utawanufaisha kwa kuwajengea uwezo viongozi wa Bavicha 9,700 na wa Bawacha 9,700 kuanzia ngazi ya Kanda hadi Jimbo, na Chama chenyewe, nacho kitajenga uwezo viongozi wetu Kati ya April na Decemba 2013, viongozi 30,000. Tafsiri ya hii angelikuwa mtafiti na angelikuwa na nia njema angeliunganisha Tamko letu la January kuwa ifikapo Septemba tutakuwa tumesimika Misingi, na Matawi hadi uongozi wa Kata katika vijiji 18,000 ambayo ni takriban asilimia 100 ya vijiji vyote nchini( Tamisemi haijatoa idadi ya vijiji vyote baada ya kuviongeza). Kauli hizi zilimpita wapi Logo? Haidhuru zilimpita mbona hajawahi kuuliza mipango na mikakati ya Chama, Kama ni yake ni njema? Chama chenyewe sura na mikakati hiyo ipo kweli hatarini Kama Logo anavyotaka Watanzania waamini. Ningelimwelewa sana angelikuwa anatushauri namna bora zaidi ya kutekeleza mipango na mikakati hiyo? Sasa kwa mipango hiyo, Logo anataka tuitishe Mkutano Mkuu ili ufanye nini? WanaJf greatbthinkers, I think it is time, to take the challenge of being great thinkers and we should not be taken for a ride!
Finally, ninataka nirudie kauli niliyotoa juzi, hata Logo ni agent wa TISS, au TISS yenyewe, natal niwajulishe wasihangaike kuwarubuni, wala kuwanunua maofisa na vijana wetu wa Makao makuu. Hawatafanikiwa. Hawatafanikiwa kwa kuwa mmegawanyika kwa misingi ya 2015, na ninawapa tahadhari migawanyiko yen itaipeleka Taifa pabaya. Mkiendelea kwa mwendo mbaoenda nao mtajuta Watanzania watakapofika mahali na kukataa hujuma zenu. Ushauri wa Bure, usalama wa Taifa ni wa "taifa" na kamwe si wa mtu hata angelikuwa Rais wa Nchi. taifa nizaidi ya Rais, au kiumbe chochote Serikalini. Aidha ninawapongeza sana TISS ndani ya TISS wanaofanya kazi zao kwa dhamira, kwa kutumikia Taifa, na kukataa upuuzi unaofanywa na wachache kwa maslahi binafsi.
Nawaomba viongozi wa CHADEMA amkeni, ITISHENI mkutano mkuu mkae mpange mikakati thabiti ya kukinusuru chama chenu kwani hali ya sasa inaiweka CHADEMA hatarini sana.
Suala la Lwakatare, Polisi kuiminya CHADEMA, mara Kigoma, mara wapi. Msikubali kunyanyasika kiasi hiki hata kwa damu. Unajua saivi wananchi wameanza kupoteza matumaini sababu wanaona ni kama CHAMA kinachowafanya wateseke sana,I maana wakiandamana tu wanapigwa na kunyanyaswa sana, na CCM inawapaka matope mbaya kupitia polisi nyinyi mnasema tuna Mungu bila kujishughulisha?
Amkeni wekeni mikakati ya kukabiliana na nguvu hii ya CCM ya kuhakikisha CHADEMAinayeyuka kabla ya 2015. Mkikaa mkapanga mikakati yenu hata ikitangazwa tu kwenye vyombo vya habari adabu itarudi.
Jibu la LOGO
Kwanza siamini kama @Dr W Slaa anaweza kujibu hivi, nahisi akaunti yake imeingiliwa na wezi. Kama ndiyo wewe mheshimiwa Dr. W. Slaa, ukweli uko hivi:-
1. CHADEMA kinapoa tofauti na zamani kwa maana ya kwamba uhamasiashaji unapungua, vijana nikiwemo na mimi tulikuwa tunafurahi sana kuona CHADEMa wakija na mikakati ya nguvu kupinga unyanyasaji. Juzi yale yalikuwa maandamano ya nchi nzima hata kama yangeruhusiwa mngepata asilimia kubwa ya wavuta bangi, na vijana wasio na kazi na wachache ambao kweli wanaipenda CHADEMA. Tatizo ni moja tu, TUNAPOTOKA KWENYE MAANDAMANO TUNAOKAMATWA NI SISI RAIA WA CHINI NYINYI WAHESHIMIWA MNARUDI KULA MATUNDA NYUMBANI. Mpaka ninavyokwambia hivi kuna watu wamo ndani sababu ya maandamano ya CHADEMA, kwanini msisimame kimkakati kupinga unyanyasaji huu?