CHADEMA inavyoliangamiza Taifa!

CHADEMA inavyoliangamiza Taifa!

Arusha ni mji wa kitalii na mlango wa kuingia TZ kwa watalii na wageni! walalahoi wengi hujipatia mkate wao tokana na sifa hizi za Arusha!
Kwanini chama cha upinzani CDM wanaitumia Arusha kuwa kitovu cha machafuko na misukosuko? kwanini hawaendi Kilimanjaro kulikoasisiwa Chadema? walalahoi wa Arusha wanataabika kwasababu Chadema wameamua kuwaadhibu wananchi wa Arusha kwa kuifanya Arusha kuwa mji wa maasi na machafuko ili Arusha iathirike kiuchumi na lengo lao la kuhujumu uchumi wa Arusha lifanikiwe!

Ombi langu kwa Wana Arusha wasikubali kutumiwa na CDM kuhujumu uchumi wa Arusha kwani watakaoathirika niwao na familia zao huku wenzao wa Kilimanjaro wakineemeka kwa kulinda amani na mshikamano wao!

Hujakua tu Kadogoo.
 
Mkuu halafu kwa nini arusha nadhani kwenye andiko lako kunakitu cha kujifunza mkuu.
 
Mkuu kilmanjaro kule kunandugu wengi vurugu zatawaathiri acha zifanyike arusha ambako hakuna mjomba,shangazi,bibi wala babu kazi kwao arusha wanapaswa kutafakari na kuchukua hatua.
 
akili yako ni ndogo saana ila SIYO KOSA LAKO MKUU BALI KOSA LA WAZAZI KUKULEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTOKUJIAMINI NA ELIMU YA KUUNGA NA KUTUMIA MAJINA YA WATU POLE SANA ILE CCM WATAONDOKA TU.
 
Arusha ni mji wa kitalii na mlango wa kuingia TZ kwa watalii na wageni! walalahoi wengi hujipatia mkate wao tokana na sifa hizi za Arusha!
Kwanini chama cha upinzani CDM wanaitumia Arusha kuwa kitovu cha machafuko na misukosuko? kwanini hawaendi Kilimanjaro kulikoasisiwa Chadema? walalahoi wa Arusha wanataabika kwasababu Chadema wameamua kuwaadhibu wananchi wa Arusha kwa kuifanya Arusha kuwa mji wa maasi na machafuko ili Arusha iathirike kiuchumi na lengo lao la kuhujumu uchumi wa Arusha lifanikiwe!

Ombi langu kwa Wana Arusha wasikubali kutumiwa na CDM kuhujumu uchumi wa Arusha kwani watakaoathirika niwao na familia zao huku wenzao wa Kilimanjaro wakineemeka kwa kulinda amani na mshikamano wao!

Mawazo ya kijinga + upumbavu + ccm=ccm daima.
Ungekuwa timamu ungetuambia kwa mawazo yako kuna mikoa hapa tanzania ni ya mwisho kiuchumi je na huko chadema ndio tatizo?kama vile mkoa wa singida,wilaya ya bunda,wilaya ya bagamoyo.kondoa na nyingine nyingi tena hata chadema unaitafuta kwa tochi,kama ungekuwa timamu ungesema lamaana kuwa mikoa ama wilaya zisizo na upinzani ndizo zina hari ngumu kiuchumi kulko.
Kenya wana andamana,ufaransa wana andamana je tunawazidi uchumi? Ccm yenu mmekuwa majizi,maharamia,manyan'ganyi na madharimu mmeshindwa hata kutatua tatzo la madawati shuleni ni miaka 50 sasa,umaskini umekubuhu maradufu,enzi ya nyerere maadui walikuwa ni watatu ambao ni UJINGA,MARADHI na UMASKINI leo mnasema adui wa kwanza ni chadema je hayo ni matumizi ya akili?au makamasi?
Kwenu kusema ukweli ni dhambi kuliko mwizi wa madin,cdm wakiambia watz kuwa watoto wenu wanapewa bora elimu huku watoto wa wakubwa wanasoma ulaya,chama cha wajinga utawaskia wakibweka cdm wanapandikiza chuki wakati kinachosemwa ni ukweli,kama hutambui mabaya ya ccm kwa leo, utajua lini?jitambue hakuna mtu atawaza badala yako wewe.
 
Kuwa mwelewa co unaandika kwa ushabiki tu bila kufikiri, moshi halmashauri ccm walikubali kuiachia chadema ndio mana ni shwari, jiulize halmashauri ya arusha kunani mpaka wananga'ngana na kumpandikiza meya wa kichina
 
Kwa kawaida watu makini hawaongozwi na Ubinafsi katika kujadili masuala mbalimbali muhimu ya kitaifa. Hawasukumwi na Umimi, ukabila, ukanda na Udini katika kutoa michango na maoni katika ujenzi wa Taifa, hali ipo tofauti kwa Waumini wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wanajitambulisha kwa Udini,ukabila,ukanda,Umimi na Ubinafsi katika kujadili mambo nyeti ya Kitaifa.

Aidha Watu wanaojipofisha jicho la kulia na kuacha la kushoto kuangalia mambo mabaya tu hawawezi kuitwa 'Great Thinkers' kama wanavyojidanganya Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Mitandao ya Kijamii.

Naam! Ndugu wapendwa, kabla ya kusogeza Mguu mbele, naomba kusema kuwa, ni Ibara ya 18(a)ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo inayonipa haki ya kuandika Makala hii kwani Ibara hiyo inatoa Uhuru wa Mtu kutoa Mawazo na Fikra zake kuhusu Nchi yake

Ndiyo! nimeamua kuandika Makala hii kutokana na maoni na michango mbalimbali iliyotolewa na Waumini wa CHADEMA katika Mtandao wa Jamiiforums ambapo walikuwa wakichangia Makala iliyoandikwa na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk. Khamisi Kigwangalla. Michango na maoni hayo ni Ushahidi tosha kwamba CHADEMA inawahujumu Watanzania na Taifa kwa Ujumla.

Siku ya Alhamisi ya tarehe 30,May 2013, Mbunge wa Jimbo la Nzega,Mkoani Tabora, Dk. Kigwangwalla aliandika Makala katika Mtandao wa Jamiiforums. Katika Makala hiyo Dk. Kigwangalla alieleza Matatizo mbalimbali yanayolikabili Taifa letu huku akipendekeza njia mbadala kuyakabili Matatizo hayo.Kubwa zaidi Dk. Kigwangalla aliwataka Watanzania kubadilika Kifikra huku akisema kuwa,"Uoga wa kubalika ni sumu kwa Wapenda Maendeleo". Ngoja niendelee kumnukuu Mbunge huyo ili kwayo Maoni yake yaweze kulinganishwa na kile kilichochangiwa na 'Wanamagwanda'.

"Napenda kuona Watanzania, Sote kwa pamoja tukibadilika kifikra. Tuanze kuwa Wabunifu zaidi, wenye Uthubutu,Wachapa kazi, Waaminifu, kuweka mbele Uzalendo kwa faida ya wote badala ya Umimi zaidi kwa faida yangu. Napenda kuona Watanzania Wenzangu tukizaliwa Upya leo na kuanza nguvu mpya leo ya kuleta mabadiliko ya kifikra na Kiutendaji. Tuondoke kwenye Umbumbumbu wa kuamini kuwa,kila kitu kitaletwa na Serikali. Tuanze kuamini kuwa, tunaweza kubadilisha maisha yetu kwa kuchukua hatua sahihi katika maisha yetu binafsi na katika jamii yetu. Tuanze kuamini vingine kuwa, tunaweza kuamua kuibalisha Nchi yetu sisi wenyewe na kutoka hapa tulipo leo na kuingia Dunia nyingine kabisa kiuchumi na kijamii".

Bila shaka Mawazo yaliyoandikwa katika Makala hiyo ni ya kupongezwa,kuungwa mkono,kuhamasishwa na kufanfanyiwa kazi kwa Watu wenye Ujenzi wa Fikra kwani Mwandishi wa Makala hiyo ameonekana kuandika kwa hisia kali na hivyo kudhihirisha kuwa, ameguswa na kukerwa na matatizo yanayolikabili Taifa letu. Hongera sana Kigwangalla.

Lakini tazama! hali inakuwa tofauti kwa Wafuasi wa CHADEMA,baada ya kuunga mkono,kuhamasisha na kufanyia kazi mawazo hayo, wametumia Wino wao kubeza na kutweza mawazo hayo kwa kuwa tu yamesemwa na Mtu wa CCM. Yangesemwa na Kiongozi wa CHADEMA yangekuwa lulu. Huu ni Uzandiki wa Fikra unaoweza kuliangamiza Taifa letu kwa Misingi ya Uchama, Ubinafsi na Umimi na kwamba vitendo hivi vya hovyo hufanywa na Wasomi Uchwara na Wanasiasa Makapi wasiolitakia Taifa mema na haya ni matokeo ya kushindwa kujenga hoja na kutumia hoja za nguvu kuyafanya mambo yao yakubalike.

Aidha, ni bora kuwasilisha kwenu baadhi ya michango na maoni ya baadhi ya Wanamtandao huo wa Jamiiforums ambao mara nyingi wanajitambulisha na kujigamba kwa Uchama badala ya Utaifa kama ifuatavyo:

Mchangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Steven Robert Masatu amesema "Huwezi kuhubiri Fikra mbadala ilihali wewe upo kwenye fikra mgando. Mkuu toka kwanza huko uliko( CCM)". Evi ni kweli kwa mfano si sahihi kwa mnyonge kuwatetea wanyoge wenzake kwa kuwa tu naye ni Mnyoge? kama hivyo ndivyo basi Mwalimu Nyerere asingeliwatetea Watanzania maana alikuwa Mnyonge, kama si upotoshaji nini?.Ingawa hata hivyo Kigwanga haonekani kuwa na Fikra mgando maana aliyoyanena hapo hunenwa na wachache tu.

Nderingosha kama anavyojitambulisha katika Mtandao huo amesema "Hizi Makala ungekuwa unawaandikia Wabunge wenzako wa CCM maana wao ndio wanatakiwa kubadilika kifikra na siyo Wananchi". Huu ni ukweli au kuwahujumu Watanzania?

Vilevi Meningits amesema kuwa "Badiliko la kwanza ni kuitoa CCM mwaka 2015" huku akifuatiwa na mwenzake anayejitambulisha kwa jina la Verified na kusema kuwa, "Tatizo ni CCM" hawa ndio wasomi wetu wanaoyaangalia mambo kwa jicho moja tena la kushoto. Ewe Mwenyezi epusha janga hili katika Taifa letu.

Hivyo,Wachangiaji hawa wanne ni wachache kati ya Wengi wanaojitambulisha kwa Uchadema katika mtandao huo wa kijamii ambao wanaonekana kukifia chama kuliko Taifa, kupinga 'Constructive Ideas' kwa sababu tu yamesemwa na Mtu wa CCM na kuyaangalia mambo kwa jicho la kushoto huku wakiziba la kulia wasione mazuri. Huku ni kulitafuna Taifa kwa Misingi ya Uchama, Umimi na Ubinafsi.

Nisingependa kumaliza makala hii pasi na kuwashauri viongozi wa CHADEMA na Wafuasi wake kuwa, wawe tayari kulifia Taifa kuliko Chama, Wawaunge mkono viongozi wetu pale wanapokuja na mikakati ya kuljenga Taifa,kuwapa moyo viongozi wetu kwa mawazo yao pale yanapoonekana ni ya tija kuliko kuwabeza, tweza na kuwakatisha tamaa kwani kufanya hivyo kwaweza kupelekea viongozi wetu kujihusisha na malumbano badala ya kusisimamia shughuli za kimaendeleo na hatimaye kulipeleka Taifa kwenye Mdomo wa Mamba. Kwa faida ya nani?

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Ninaitwa BAKARI MADAYA (Mwanatunduru).
Ninapatikana simu: 0789357823 au barua pepe madayabakar@hotmail.com

Kaka hongera kwa maono mapana nitakupigia simu tuongee mkuu.
 
tafuta hotuba ya mwalimu NYERERE alipo kuwa ansisitiza uwepo wa vyama vingi,alisema kuwa ukiona chama cha siasa tena cha upinzani kina kaa meza 1 na serikali tena kina anza kuisifia ujue kimepoteza sifa ya kuwa chama cha upinzani.so kosa la chadema kufanya kampeni za kuhitimisha kuwa kubwa au kosa ni polisi ccm kurusha risasi ovyo,rejea ushaidi wa mtoto aliyepigwa risasi na polisi akitokea madrasa
 
Tunashukuru umaitambua na umeitumia haki yako ya kikatiba kutuwekea utumbo humu
 
Karibu jamii forum. If that is your line of thinking you still have long way to go though
 
sna tatzo na cdm wana sera nzur sana ila kero yangu kubwa ni kwa nn kla kukicha vurugu wanazfanyia arusha kwa nn waszpeleke kwao moshi w r tyd na hz vurugu wakaarbu soko la utalii mosh penye kampun za kna mbowe na ndesamburo si arusha kila sku
 
Katibu mkuu wa CHADEMA taifa kwa sasa yuko hoi bin taabani kuongoza chama chake, ambacho hivi karibuni kiliweza kujizolea sifa hapa nchini, kwa kile kinacho daiwa kuwa kiliweza kutoa changamoto kubwa kwa chama tawala (CCM).

Jambo la kushangaza na kushtua kuhusu hiki chama, ni kuporomoka kwa umaarufu wake nchini, baada ya watanzania kugundua kuwa sio chama cha 'demokrasia' na 'maendeleo' kama wanavyo jipambanua, ila ni chama cha vurugu, fujo na maandamano yenye kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.

Sifa hizi mpya kwa chama hiki, ambazo ni fujo na vurugu, zimetolewa na wananchi baada tu ya CHADEMA kumpa mamlaka Dr Slaa ya kuwa mtendaji mkuu wa chama hicho, Dr Slaa kwa siasa na mbinu zake, alidhani kwa kutumia maandamano basi ndio itakuwa njia pekee ya kuzidi kuinua jina na hadhi ya chama, kumbe imekuwa kinyume chake.

Mikakati ya Dr Slaa ya kuleta mageuzi ya siasa hapa nchini kupitia chama chake (CHADEMA) na washirika wake IMEDODA, na badala yake mikakati hiyo imefanikiwa kuondoa na kutokomeza kabisa sentensi isemayo "Tanzania ni kisiwa cha amani", na kwa sasa kuwa kisiwa cha wahanga wa mabomu.

Hoja ya msingi hapa ni kwamba, kama Dr Slaa amechemka na yuko hoi kuiongoza CHADEMA kwenye kufanya siasa za kistaarabu na safi. Je, atawezaje kuongoza nchi yetu yenye changamoto za kila aina?, haya ni mambo ya msingi sana kuhoji, kwani kushabikia uozo ambao utaenda kuliangamiza taifa sio UZALENDO hata kidogo.

Kwa hiyo Mkuu Kuwaachia CCM wachezee Nchi ndiyo uzalendo?Kuwakosoa tu ugaidi? mnang'ang'ani kama kupe.Nchi zote zilizotekeleza mauwaji ya kimbali yalitekelezwa na Vyama Tawala vilivyopigania uhuru havikutaka kabisa kuondoka madalakani vikaamua kuuwa raia wake vikidhani kwamba ni kujiimalisha visiondolewe madalakani.lakini viliondoka na nyinyi mtaondoka tu,usingeamini kama Mtu mweusi angeitawala afrika kusini na Marekani.
 
Ni mambo ya kusikitisha sana watanzania wanaumia wanawadanganya wanaandamana na hatimaye wanaumia.
jamani inasikitisha sana wenyewe wala wahamo watanzania wanauizwa halafu wanaleta mizaha na kuwahadaa
watanzania. Hivi mnafikiria amani ikitoweka mtaweza irejesha?

jamani tunaipenda nchi yetu. CHADEMA CHADEMA. Mnajua kabisa kile mkifanyacho sio sahihi
hivi mnajari kweli utu wa mtu.

inauma sana ukifikiria kwa undani.
hii nchi yetu tuweni na mshikamano tuacheni mambo haya nchi yetu
inahitaji maendeleo na amani ya kizazi hiki na kijacho

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRICA
 
yani umenena ndugu...tatizo watanzania wengi wana mgomo baridi wa kutotumia akili zao.....tusubiri tu.
 
Chadema wanataka nchi kwa kutumia mbinu zote wanazoweza. Jamaa wapuuzi kweli hawa.
 
Ni mambo ya kusikitisha sana watanzania wanaumia wanawadanganya wanaandamana na hatimaye wanaumia.
jamani inasikitisha sana wenyewe wala wahamo watanzania wanauizwa halafu wanaleta mizaha na kuwahadaa
watanzania. Hivi mnafikiria amani ikitoweka mtaweza irejesha?

jamani tunaipenda nchi yetu. CHADEMA CHADEMA. Mnajua kabisa kile mkifanyacho sio sahihi
hivi mnajari kweli utu wa mtu.

inauma sana ukifikiria kwa undani.
hii nchi yetu tuweni na mshikamano tuacheni mambo haya nchi yetu
inahitaji maendeleo na amani ya kizazi hiki na kijacho

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRICA

Una kiwango gani cha elimu maana kauli yako inatisha na sikuelewi elewi, au na wewe ni Lumumba Project
 
najua hawawezi kukubali kuwa ndio wahusika lakini ukweli ni huu hapa chini :

Mambo yaliyotokea juzi nchini hasa arusha yana chimbuko lake...ni mambo ambayo hayaji hivi hivi na kwa gafla...yana mzizi wake . lengo la mambo yote haya tageti yake kubwa ni kuimaliza chadema kisiasa na kuhakikisha kufika mwaka 2015 kinakuwa chama jina. Huu ndio mkakati mahususi ambao uliasisiwa mwaka jana na deadline yake ni june 30 mwaka huu .
Kuna mambo mengi yametokea huko nyuma yenye kuwa na lengo la kuimaliza chadema .. na katika mambo hayo kulikuwa na mbinu nyingi zimetumika lakini zilishindwa na hazikufanikiwa kuzima na kuififisha chadema..

Baada ya hapo ndipo sasa ukabuniwa mkakati huu unaoendelea na ambao taget yake kubwa katika tukio la juzi ilikuwa ni kumuua mh.Mbowe. (unampiga mchungaji na kondoo wanatawanyika)...Bahati nzuri Mh.mbowe yuko hai lakini ajiangalie sana tena sana maana wamepania kummaliza. .

Kwa kuwa chadema imejipambanua kwa wananchi kuwa ni chama kinachotetea wanyonge na kinakubalika zaidi; hili ndani ya ccm halifurahiwi hata kidogo na hasa ikizingatia kuwa isingekuwa kufanya utaratibu mwingine mwaka 2010 katika uchaguzi wasingeweza kushika dola maana mshindi wa uchaguzi ule hakuwa kikwete.

Wafuatao ndio wanatakiwa kukamatwa mara moja na kama hawakatwi chadema na wananchi wanaolipenda taifa hili wahakikishe watu hawa wanavuliwa madaraka yao mara moja.

1. Emmanuel Nchimbi.....huyu ndiye anajua chanzo cha jambo hili na hasa tukio la juzi la ulipuaji bomu huko arusha.. anajua aliyesafirisha bomu toka china hadi kulifikisha nchini pamoja (mzizi)

2. Mwigulu nchemba...huyu ndiye aliyepewa maazimio ya utekelezaji na ufanikishwaji wa matukio hayo ya mlipuko na ahakikishe yanatekelezeka..akikamatwa huyu ataeleza kwa ufasaha pia namna alivyoipata kofia ya jeshi la china anayoonekana kuivaa hivi karibuni ..huyu ndiye mratibu .

3. Mtela mwampamba....huyu ameshirikishwa jambo hili na mwigulu nchemba ..kuna baadhi ya majukumu amepewa ikiwa ni pamoja na kuwalipa pesa vijana wanaotekeleza mashambulio hayo kupitia akaunti zao za benki.

4. Advocate Nyombi....huyu kama kiongozi mkubwa katika jeshi la polisi ndiye anahusika na kupanga mbinu za namna ya kutekeleza mashambulio na pia jukumu lingine ni kuhakikiha anapata vijana wanaoweza kuifanya kazi hiyo ambao wanatoka katika jeshi la polisi,

5. Afande pasua....huyu anahusika kwa kulisafirisha bomu hilo hadi arusha akitokea Dsm na pia ndiye anahusika na kuendesha gari lililowabeba walipuaji mara baada ya mlipuko kutokea hapo soweto

6. Afande benjamini.....huyu pia kama iliilivyo kwa afande pasua nae ni mmoja wa vijana waliotafutwa na nyombi. Huyu anahusika kwa kubeba na kusafirsha silaha (bastola &SMG) hadi arusha kwa gari binafsi na alipofika huko arusha alikutana na askari wengine watatu ambao ndio walikuwa wakirusha risasi siku ya mlipuko na mmoja alirusha bomu.

Ili kuzuia machafuko haya yasijirudie hawa watu ni muhimu wakamatwe mara moja ..la kama hawakamtwi basi wananchi hakikisheni wanavuliwa madaraka waliyo nayo vinginevyo haya mambo yataendelea na hakuna atakayekamatwa na watakuja na mbinu nyingine

Tarehe 10 /4/2015 ukiondoa Emmanuel nchimbi hawa wengine waliopo hapa katika list hii walikutana Dodoma na kupanga mbinu na kugawiana majukumu ya kufanikisha tukio la mlipuko na waliendelea kuwasiliana kwa njia za kielectroniki..
siku moja kabla ya kikao hiki kulikuwa na kikao kingine hapo hapo Dodoma kilichofanyika tarehe 9/4/2015 ambacho waliohudhuria kulikuwa na makada wengine ambao wamewahi kuwa chadema kisha kufukuzwa , waliohudhuria ni pamoja na:

1. Mwigulu nchemba
2. Henry matata
3. Mtela mwampamba
4. Adamu chagulani
5. Advocate nyombi
6. Afande pasua
7. Afande benjamini
Kikao hiki hasa kililenga kupanga ushahidi wa kesi zinazoendelea hasa za tukio la lwakatare na pia la kesi ya huko igunga ya umwagiaji tindikali.. ushahidi mwingi ulipangwa na kutungwa siku hiyo.
 
visauti vya kishetani utavijua tu......hata mtoto wa shule ya msingi anajua ccm kupitia polis ndio wanao vuruga aman katika taifa letu. ..wana wanawaondolea haki ya kuishi watanzania wenzao,
 
CDM wanataka kukukomboa kwa wakoloni!Tulia kama uko kwenye send-off!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom