Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,904
- 7,746
Arusha ni mji wa kitalii na mlango wa kuingia TZ kwa watalii na wageni! walalahoi wengi hujipatia mkate wao tokana na sifa hizi za Arusha!
Kwanini chama cha upinzani CDM wanaitumia Arusha kuwa kitovu cha machafuko na misukosuko? kwanini hawaendi Kilimanjaro kulikoasisiwa Chadema? walalahoi wa Arusha wanataabika kwasababu Chadema wameamua kuwaadhibu wananchi wa Arusha kwa kuifanya Arusha kuwa mji wa maasi na machafuko ili Arusha iathirike kiuchumi na lengo lao la kuhujumu uchumi wa Arusha lifanikiwe!
Ombi langu kwa Wana Arusha wasikubali kutumiwa na CDM kuhujumu uchumi wa Arusha kwani watakaoathirika niwao na familia zao huku wenzao wa Kilimanjaro wakineemeka kwa kulinda amani na mshikamano wao!
Huko nyuma hukuwa hivi....wamekuharibu sana siku hizi