Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 305
"Off side trick" ni mojawapo ya mbinu za mchezo inayotumika kuichosha timu pinzani hasa inapotokea kuwa na nguvu kuliko timu inayocheza nayo.
Mbinu hiyo ya ‘off side' ambayo hutumika kwenye mchezo wa kandanda inaonekana kuingizwa na kutumiwa na Chadema kwenye mchezo wa siasa.
Hilo linatokana na CCM kuwa na mabavu kuliko CHADEMA kwa maana ya CCM kuwa na serikali, uwezo wa pesa nk, hivyo inabidi Chadema kitumie akili za ziada ili kiweze kuyamudu mabavu ya chama tawala na kuufanya mpambano usionekane ni wa upande mmoja.
Mbinu hiyo inaiwezesha CHADEMA kuyamudu makeke ya CCM kwa kutumia nguvu kidogo tu.
Kazi kubwa ambayo ingebidi ifanywe na CHADEMA katika kujijengea uhalali wa kisiasa kwa wananchi jambo linafanywa na mpinzani wake CCM pasipo kujielewa.
‘Off side trick' ya CHADEMA inakuja hivi, chama hicho kinaandaa maandamano ya amani, kwa mfano, kama yale yaliyofanyika kule Arusha, CCM kwa woga usio na sababu inaviweka tayari vyombo vya dola kwa tahadhari na vyombo vyote vya habari.
Ni katika hali hiyo chama tawala kinajikuta kimeongeza idadi ya wapenzi wa chama pinzani hata ambao walikuwa hawajasikia wanakisikia. Hiyo ni mbinu ambayo imezaa matunda kwa CHADEMA kuyatumia mabavu ya chama tawala kujiimarisha kimtandao.
CHADEMA ni chama kichanga kimfumo na kiuchumi. Kwa maana hiyo inakuwa vigumu kujinadi kwa kila mwananchi nchi nzima ikizingatiwa kuwa mashina yake ndiyo kwanza yanachipua nchi nzima, kazi ya kumwagilia ili yasikauke inafanywa na CCM. Maana kila wanakopita makada wa CCM nchi nzima hawana jingine la kuongea bali kuiimba CHADEMA.
Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Jakaya Kikwete akihutubia taifa zaidi ya asilimia sabini ya hotuba yake ni lazima ikihusu CHADEMA.
Katibu Mkuu Makamba katika maneno yake 20 anaweza kutamka neno CHADEMA mara 10 bila kutamka neno CCM hata mara moja! Kwa namna hiyo kwa nini tusiamini kuwa CCM inaifanyia CHADEMA promosheni?
Hivi majuzi CHADEMA wakiwa mkoani Kagera katika jimbo mojawapo la mkoa huo wananchi waliwaeleza matatizo yanayowakabili likiwemo la kuuziwa kilo moja ya sukari kwa shilingi 2,000.
CHADEMA waliahidi kulishughulikia tatizo hilo bila kuchelewa. Baada ya CHADEMA kukamilisha Operesheni Sangara katika kanda hiyo, Waziri Mkuu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, akapanga ziara ya kwenda mkoani Kagera kwa lengo la kwenda kufuta nyayo za CHADEMA.
Kitu cha kwanza alichoanza kukilalamikia Waziri Mkuu baada ya kufika Kagera ni bei ya sukari akaagiza bei ya sukari mkoani Kagera ishushwe hadi shilingi 1,700.
Kama agizo hilo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda litakuwa limetekelezwa nani atakayepaswa kupewa shukrani? Ina maana CCM muda wote ilikuwa haijaliona tatizo hilo mpaka walipoenda CHADEMA? Kinachoonekana ni kama Chadema kimeamlisha waziri mkuu akatii amri wakati chama tawala kimelala usingizi.
Hiyo ndiyo kazi wanayoifanya Chadema kwa sasa wanacheza‘off side trick' na CCM kwa asilimia kubwa baada ya chama hicho tawala kuchezewa mtego wa kuotea kinajikuta kinazuia badala ya kushambulia.

Prudence Karugendo