CHADEMA inamiliki vitega uchumi Gani?

Mali zote za CCM ni za serikali! Majengo yamejengwa na serikali, viwanja ni vya serikali, mashamba ni ya serikali nk.

Kwa taarifa yako hakuna mradi hata mmoja wa ccm umetokana na michango ya wana ccm! Hakuna mradi wo wote umeanzishwa kutokana na ruzuku pamoja na kwamba ndiyo chama kinachokomba zaidi ya 70% ya ruzuku yote ya vyama vya siasa!
 
Mkuu hujajibu swali!
 
Nipo hapa kinondoni Uhuru peak napata supu. Kwa mbele naiona mipango mikubwa ya UVCCM ya uwekezaji pale ilipokuwa mango garden.Najiuliza Chadema wana uwekezaji wowote hata wa boda boda tu?!...... niishie hapo!
Yaani bila aibu miaka 50!!mko madarakani leo ndio unazungumzia eti UVCCM wana taka kuwekeza hapo eneo la mango garden kweli??na hata hivyo vinavyoitwa eti vitega uchumi vya ccm viko wapi zaidi ya maeneo ya wazi ambayo ki uhalisia sio yao yalitakiwa yasiwe yao!!halafu eti yanatumika kulaza magari nacho chama chakavu kinaina bonge la vitega uchumi!!hahaha!!viwanja vya mipira nyie ni kuchukua pesa tu ikija kwenye ukarabati tabu tu!!!jengo la makao makuu hadi serikali ya CHINA isaidie!!
 
Dilimulaina hapa kazi tu
 
Mkuu Chadema ina mwaka 26!
 
Chadema wamewekeza sana Wana kiwanda kikubwa mno cha majungu pale makao makuu ya chadema .Kiwanda kinaitwa Majungu Industries limited.Na ndicho kiwanda pekee wanachomiliki.
Hahahaha mbavu zangu jamani jamani uwiii
Hahahaha
Eti MAJUNGU INDUSTRIES
 
Mleta mada hata kama ni CCM kindakindaki lakini ametoa changamoto nzuri sana kwa chadema.

Ukweli Mimi hua naihurumia sana Chadema kwa sababu kufikia 2025 itakua imebaki kama NCCR Mageuzi.
Hili halina ubishi.
Kwa kuwa wameshindwa kubadilika kulingana na Siasa za awamu ya Tano.
Siasa zilizoshikana na dola kama mnyororo wa baiskeli.

Makao Makuu ya nchi yapo Dodoma lakini Chadema mpaka sasa hawana Jengo la maana pale kama makao makuu ya Chama.

Ukifika Leo makao makuu ya chadema ni kama vile umeenda kwenye ofisi za Saccos za soko la Tandale.
Hakuna mvuto wa kumfanya MTU mwenye akili zake ajikite kuona kuwa hiki ni chama zaidi ya kukitumia tu kama ngazi za kupata umaarufu kisha warudishwe CCM na kupata madaraka.

Chadema waliwahi kuwambiwa kuwa wanaishi kama makambale Kila MTU ni mbishi na mjuaji. Jambo la kusema kwa busara tu basi wanafoka na kutoa mapovu kama mtu anayepiga mswaki.

Utetezi wanaoutoa ni wakitoto kabisa eti CCM ofisi zao zilijengwa na serikali. Huu ni uongo na upotoshaji mkubwa.
Mimi sio mwanachama wa CCM lakini tangu enzi za chama kimoja serikali ilijenga ofisi zake na chama kilijenga ofisi zake kwa kuchangisha watu. Tena watu wakati huo walikua ni maskini sana.

Leo hii Chadema kina wanachama na mashabiki wasiopungua mil.5. Tens wengi wakiwa ni wasomi na watu kwenye shughuli za maana mana chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaungwa mkono zaidi mijini. Hivyo watu wenye uwezo wao wengi ndio wanaokiunga mkono.
Sasa tujiulize inakuaje Kabisa moja tu la Agape lisilo na waumini hata 50000 nchi nzima lakini wanaofisi nzuri,wanamiliki Radio na Television kupitia michango ya waumini wao lakini Chadema chenye wanachama Mil .5 Hakina ofisi inayolingana na jengo la kabisa la RC Kimara au Msikiti wa Magomeni Mapipa unwotokana na michango na juhudi za watu wachache.

Kama Chadema kinashindwa kutumia Rasilimali watu kujiletea maendeleo ndani ya chama kama mfano wa namna watakavyofanya kwa maendeleo ya nchi endapo watapewa ridhaa ya kuongoza nchi basi Chadema hakijafikia kiwango cha kukabidhiwa nchi.
Watu mil.5 wanatosha kabisa kujenga ofisi za chama nchi nzima na bado kuna ruzuku ya Kila mwezi.
Mbowe na viongozi wa chadema waache ubinafsi waajiri wataalamu wa mipango na uchumi na pia waajiri watu wa propaganda waliopitia kwenye idara mbalimbali na kujua mengi wasitegemee tuu vijana waliomaliza vyo vikuu wanaopinga pinga Kila kitu bila hata kuangalia kuwa jamii inasemaje.

Pia chadema wajifunze namna ambavyo Nyerere aliweza kutafuta Uhuru bila kumwaga damu na alitumia mbinu gani mpaka wazungu wakamwamini na kumkabidhi nchi kidogo safi kabisa na baadae akawageuka bila vurugu wala nini. Sasa Leo hii hata udiwani tu wanashindwa kukabidhiwa hata pale waliposhinda kwa sababu hawataki kufanya kazi na wakurugenzi na maDC ambao ni waafrika wenzetu wanafanya ubabe kama watawala ambao kinga yao Siku zote ni ubabe.

Chadema badilikeni na mpokee ushauri wa kutafuta maendeleo ya chama kwa kuwa mtaji mkubwa wa watu mnao msitegemee huruma ya wananchi .
Na hata Sikh Chadema kikishika nchi kisifikiri kitaweza kuwaburuza CCM kwani CCM bado kitakua na wabunge na madiwani wengi. Haitakuwa rahisi kuifuta CCM kwa wananchi kwa kuwa kimejijenga sana vijijini.
 
Nipo hapa kinondoni Uhuru peak napata supu. Kwa mbele naiona mipango mikubwa ya UVCCM ya uwekezaji pale ilipokuwa mango garden.Najiuliza Chadema wana uwekezaji wowote hata wa boda boda tu?!...... niishie hapo!
Watapata wapi nafasi hiyo ya kumiliki au kuwa na wazo la kuanzisha vitega uchumi wakati mnawapiga mabomu kila kukicha?
 
Back
Top Bottom