Chadema inakokwenda kisiasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema inakokwenda kisiasa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MANGUNGO, Oct 30, 2012.

 1. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Nimesoma vichwa vya magazeti mbalimbali yote leo,nimeona magazeti ya serekali na yale yanayo milikiwa na makada wa ccm na CCM yenyewe yakibeza ushindi wa chadema katika uchaguzi wa madiwani,kwa kifupi nitoe mtazamo wangu na mawazo yangu juu ya mwelekeo wa chama cha demokrasia na maendeleo,kwanza kuwapongeza viongozi wote wa chadema pasipo kutaja majina yao isipokuwa SHIBUDA.

  kwa kazi waliofanya hasa kuweza kutetea kata zao na kikubwa kuongeza kata 3 kwa kuinyang'anya ccm hakika sio jambo dogo,hii inatoa mwelekeo kuwa 2015 chadema kinaweza kuinyang'anya ccm viti vingi vya ubunge,udiwani na hata urais na kufanikisha kushika dola,chadema kinatakiwa 1.

  kuongeza nguvu katika harakati zake za vuguvugu la mabadiliko,yaani movement for change(m4c) kuingia vijijini zaidi hadi ngazi ya mitaaa hadi kata kuwaelimisha wananchi juu ya sera zake na hata kuwapa wananchi elimu juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kupiga kura na kushiriki zaidi kataka kupiga kura kwani vijana wengi hawakushiriki katika kupiga sababu hawana shahada za kupigia kura kwa kupoteza shahda au kutokujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,2.

  Kufungua matawi katika kila mtaa,na ikiwezekana kuwa na mabalozi wao kabisa kama ccm inavyofanya ngazi ya shina,ili wananchi wapate elimu kupitia mabalozi huko huko ngazi ya shina na sio kusubiri mpaka viongozi wa kitaifa wa chadema waje kutoa elimu na hata kuuza kadi kwa wananchi,matawi yaliopo kwasasa ni machache sana na hayaendani na kasi ya mda ukidhingatia kuna miaka 2 imebaki nchi ingie ktk uchaguzi mkuu sasa nguvu kubwa inahitajika kuhakikisha chama kinafika chini kabisaa na kina kuwa na mabalozi wake.

  Wakati umefika sasa chama kiweke vigezo vya wagombea hasa kielimu,kinidhamu na maadili,uwajibikaji na hata mvuto(nguvu ya ushawishi) kwa kuwashindanisha wagombea watarajiwa kwa wanachama ili kuchuja wanachama na kupata mgombea ambaye kweli atakua competance na amejitoa kwa dhati,,kwani uchaguzi huu wa udiwani kuna baadhi ya wagombea wa chadema hawakuwa na mvuto kwa wananchi ktk nyanja zote za kielimu,nidhamu na maadili n.k 4.

  Kubaini mbinu zzote chafu zinazo fanywa na ccm kama rushwa na wizi wa kura ikishirikiana mawakala na hata tume ya uchaguzi kuhujumu kura za chadema,kwani ktk uchaguzi huu wa madiwani rushwa na michezo michafu imefanywa na ccm ikishirikiana na vyombo vya dola ili kuhujumu uchaguzi,5.

  Hivi sasa kuibika ukatishaji tamaa viongozi wa chadema kupitia matokeo haya kupitia vyombo vya habari na mitandao wanachadema na viongozi wote wasikatishwe tamaa au kukubali kusimangwa kutokana matokeo haya udiwani ambayo kwangu nimeona ni mazuri japo sio kwa kiwango kilichotegewa lakini ikubalike kuwa chama kimepigana vya kutosha kimelinda viti vyake na kimeongeza viti sio jambo dogo ni jambo kubwa kwanini hata ccm ambaye amepoteza viti hivyo kisaikolojia hayupo safi ni sawa na mtu mwenye kidonda kibichi sasa tusikubali mtu wa namna hii atengeneze propaganda za ajabu kuhusu chadema kama alivyosiskika NAPE akikejeli eti chadema kinakufa na hata kuita movement for change kuwa movement for death,chadema isimwache mtu huyu atambe hata kidogo.bali imwadhibu kwa hoja na vitendo.

  Mwisho niseme maisha yanaendelea kukata tamaa ni sawa na kukubali kifo mashabiki wa chadema na viongozi wa chadema sasa tuanze aharakati yaani kama ndio moto umemwagiwa mafuta,moto uliwashwa wa vuguvugu la mabadiliko ukabe kila kona ya nchi,2015 DOLA ITAKUWA CHINI YA CHADEMA,MUNGU IBARIKI CHADEMA,MUNGU IBARIKI TANZANIA.asanteni naomba kuwasilisha.
   
 2. B

  Baba Hellen JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 764
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  makamanda vita vinaendelea
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mlitegemea Nape aseme chadema mmefanya vizuri eeee, 4ril chadema imepanda ngazi,M4C mbeeeele
   
 4. N

  NAMBEKE Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera CDM kwa ushindi wa kishindo, kati ya viti 29 umepata 5 sawa na asilimia 17.2 CHADEMA HOYEEEEEE.

  Ni vizuri kuambizana ukweli hata kama unauma. Hivi kweli kwa matokeo haya unapongeza!
   
 5. Kilimo

  Kilimo JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  kila la kheri kwa CDM
   
 6. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  ahsante kamanda
   
 7. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Jambo moja kubwa ambalo CCM hawalifahamu ni kuwa sehemu kubwa ya wananchi watakaowaondoa 2015 hawamo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Kuna jeshi la mapinduzi litakalo jiandikisha 2014/2015, hao ndio watakaoifurumisha kwa kutumia sanduku la kura, sio hawa wahaohongeka kwa kanga na chumvi.
   
 8. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,738
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 280
  Fanya kazi ya ziada kuhamasisha uandikishaji basi!!
   
 9. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Bahati mbaya tu sijaweza kujumlisha kura zote zilizopigwa, CCM wasijidanganye kuna wameshinda kwa viti vingi lakini idadi ya jumla ya kura tofauti ni kidogo mno hayo ndo NAPE anapaswa ayatumie kutathmini chama chake kama kinapanda au kinashuka
   
 10. franksarry

  franksarry JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 1,107
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mwana jamvi Mbalinga umenena, khs wapiga kura wapya watakaoandikishwa ktk daftari la wapiga kura....!
   
 11. piper

  piper JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Thanx kwa uzi mzuri, cha msingi CDM wasife moyo bali mapambano yaendelee, despair is a moral suicide na hata mbuyu ulianza kama mchicha.
   
 12. josam

  josam JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 1,754
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  moja ya vitu vinavyochangia ushindi wa ccm ni pamoja na daftari la kupiga kula. Tangu 209/2010 kwa nini daftari halifanyiwi maboresho? Si sahhi kusema kuwa watu waliotimiza miaka 18+ ni wengi kukiwezesha cdm kushinda lakini ni ukweli pia watanzania wengi hawakujiandikisha miaka hiyo chini ya 2010. Kwanini kwasababu watu hawakuona umuhimu wa kupoteza muda, kuota jua kujiandikisha, kupiga kura ili hali wakijua ccm ndiyo watakao shinda kwa vyovyote vile. Ikumbukwe pia kwamba vyombo vya dola na mfumo mzima wa chaguzi zetu siyo huru na ni pendeleo kwa chama tawala. Rushwa inahalalishwa na mwenye kiti wa chama, rais ndani ya chaguzi zao, wao kwa wao...!? Unategemea nini watu hao hao wanapokuwa wanashindana na watu wengine wa vyama tofauti na katika hali ya sasa ya kutaka kuaminisha watanzania kwamba vyama visivyotawala si chochote??? Tafakali kabla ya hatua
   
 13. josam

  josam JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 1,754
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Moja ya vitu vinavyochangia ushindi wa ccm ni pamoja na daftari la kupiga kura. Tangu 2009/2010 kwa nini daftari halifanyiwi maboresho? Si sahhi sana kusema kuwa watu waliotimiza miaka 18+ ni wengi kukiwezesha cdm kushinda lakini ni ukweli pia watanzania wengi hawakujiandikisha miaka hiyo chini ya 2010. Kwanini kwasababu watu hawakuona umuhimu wa kupoteza muda, kuota jua kujiandikisha, kupiga kura ili hali wakijua ccm ndiyo watakao shinda kwa vyovyote vile. Ikumbukwe pia kwamba vyombo vya dola na mfumo mzima wa chaguzi zetu siyo huru na ni pendeleo kwa chama tawala. Rushwa inahalalishwa na mwenye kiti wa chama, Rais ndani ya chaguzi zao, wao kwa wao...!? Unategemea nini watu hao hao wanapokuwa wanashindana na watu wengine wa vyama tofauti na katika hali ya sasa ya kutaka kuaminisha watanzania kwamba vyama visivyotawala si chochote??? Tafakali kabla ya hatua
   
 14. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 80,785
  Likes Received: 79,877
  Trophy Points: 280
  ndio tunapongeza ulitaka tubeze?
   
 15. K

  KIBE JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unapongeza kupata viti 5 kati ya 29???..kweli akili za maji hivi nguvuyo waliotumia cdm kwenye kampeni ukilinganisha na ccm kweli walistahili hayo matokeo??..mana hadi viongozi wa taifa walishiriki..ukweli ingawa ni mchungu cdm mumeanguka vibayaa na sioni hayo matumaini mliyo nayo ya kuchukua nchi 2015 yanatoka wapi kama chaguzi hizi 29 ambazo ni chache mumeshindwa je ingekuwa nchi nzima mngeweza wapi mana ili cdm ipate ushindi lazima viongozi wa kitaifa waende...je 2015 mtazunguka kupiga kampeni kwa kila mgombea wa kata ..... Jipangeni upya acheni siasa za kwenye vyombo vya habari...jengeni chama na acheni kuwaza madaraka zaidi kwani uwezo wenu wa kushinda kwa sanduku la kura bado ni mdogo sana 10%
   
Loading...