CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
CHADEMA INA DEMOKRASIA YA MIUJIZA
Nimemsikiliza mtani wangu Mbowe ambaye hujinadi kuwa CHADEMA kuna demokrasia lakini nchi haina demokrasia. Alichosema nikajiuliza hivi hii ndio demokrasia ndani ya CHADEMA?
Mbowe anasema hivi: baada ya yeye kushauriana na viongozi wenzake amemshauri Lissu achukue fomu ya kugombea Umakamu Mwenyekiti wa chama chake! Hivi hii ndio demokrasia sampuli ya wapi? Mwenyekiti kumshauri mtu agombee kuwa msaidizi wake! Kuna maswali mengi! Hivi wenzake wenye nia ya kugombea nafasi hiyohiyo wana chao?
Mwenyekiti pamoja na hao viongozi alioshauriana nao tayari wameshampa mgombea mmoja kura zao! Na hakika wamewatangazia wapiga kura kuwa huyu ndiye mumpe kura! Hii kwa kweli kama ni demokrasia basi udikteta ni mzuri mno!
Swali jingine ni hili: Kwa nini Mbowe hakumshauri Lissu agombee nafasi yake? Alijuaje Lissu anataka umakamu na sio kiti chake? Haiwezekani Mbowe kahami kiti chake dhidi ya mtu aliyehisi anakinyemelea? Hii nayo ni demokrasia ya mtori nyama kuzama chini
Katika hotuba hiyo Mbowe anaendelea kusema: Nilitaka kujiuzulu lakini sioni WA kumuachia chama! Toba maulana!
Mbowe kasahau si muda mrefu aliwahi kusema hawezi kuachia kwa kushinikizwa na CCM isipokuwa kwa kuambiwa na wanachama wake? Hili wazo kuwa alitaka kujiuzulu limemjia lini? Tushike lipi? Alitaka kujiuzulu au hatajiuzulu kwa shinikizo la CCM?
Lakini tujiulize tena! Si huyu Mbowe anaijitapa kajenga chama imara? Chama imara kinakosa mtu wa kumpokea uenyekiti? Ina maana kuanzia kina Lema, Heche, Selasini, Sugu, Msigwa, Halima, Bulaya na wenzao woote hawafai kushika uenyekiti? Ni Mbowe Tu?
Lakini Lema hakubaliani na Mbowe! Leo wakati akijaribu kushawishi wajumbe wampe kura kuwa Mkiti kanda ya Uchagani kasema hivi: anataka uenyekiti Kanda ili ajiandae kuja kuwa Mkiti Taifa! Aisee kweli mbwa usiyemlisha humtumi!
Linakuja swali: Ina maana labda Lema keshaambiwa akitoka Mbowe ni yeye? Kiruuu! Ni kupokezana kichaga kama kata ya mbeke? Hii kweli saccos ina wenyewe!
Pole yao kina Sumaye na ambao sio members wa inner circle!