Itakumbukwa Chadema waliwafukuza madiwani wake watano waliokataa kutii maagizo kamati kuu ya kumtambua meya wa Arusha mwaka jana. Na hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa jiji madiwani walionekana kwa mara ya kwanza hadharani wakishiriki shughuli za uzinduzi wa jiji na kuandikwa kwenye vyombo vya habari.
Baada ya taarifa ile ikaonekana kama mpya kwa viongozi wa chama na ndipo Dr. Slaa akasema amewapa nafasi ya kujieleza kwanini nao wasifukuzwe kwenda kinyume na msimamo wa chama ingawa kwa wakazi wa Arusha wanajua kuwa hao madiwani huwa wanaingia kwenue vikao na vinaongozwa na huyo huyo Meya wanaosema hawamyambui.
Jana tarehe 31/12/2012 kulikuwa na kikao kingine cha Full Council na madiwani wa Chadema walihudhuria wote hata kabla chama hakijatoa msimamo wake wa ama wamewaruhusu au la.
Hata hiyo bado haijaweka hadharani majibu ya barua zilizoandikwa na madiwani baada ya kuamriwa kufanya hivyo na chama kupitia kwa Dr. Slaa.
Swali langu: Je chama kimemtambua meya wa Arusha?
2. Na kama wamemtambua vipi waliwafukuza wale madiwani watano?
3. Je hiki nacho ni kiburi cha madiwani kukaidi maagizo ya chama kupitia kwa katibu mkuu Dr. Slaa?
Kwa sababu viongozi wengi mnapita hapa Jf tunaomba mtufafanulie kwani inatufanya sisi watu wa Arusha tuwe na maswali mengi kuliko majibu.