CHADEMA imelinda heshima ya Sosopi

Ahahahaha! Hii kali!
 
..YES.

..kama hali halisi inalazimisha hivyo ili kukiwezesha chama kuongeza ushawishi ktk kanda ya Nyasa.
Du! Nyie wazee mna mahaba na unafiki sana...
Mbowe akikacha katiba ni sawa na unaipamba kabisa kuwa ni kutumia busara ikitokea pande ya pili ni udikteta, kweli wa Tz ni wa Tz tu.
 
Ilipaswa UKUTA nao uhusike ndani ya CDM, maana kwa mtindo huu ni wazi katiba imesiginwa kwa kisingizio cha 'maamuzi ya busara'.

Ila haya yote Mbowe anayafanya kutokana na aina ya wanachama alionao. Ukiwa na wanachama makini basi maamuzi yote yatafanywa kiumakini, ila mburula/maamuma wakiwa ni wengi basi matokeo yake ndio kama hayo unawaburuza unavyotaka na bado watashangilia maamuzi yako.
 
..Ole Sosopi angechaguliwa mashambulizi kwamba cdm inapendelea watu wa "kaskazini" yangepamba moto.

..sikubaliani na siasa za kikabila , lakini ni ukweli usiopingika kwa siasa hizo zipo hapa Tz, na ni mtaji mkubwa kwa CCM.

Cc Gamba la Nyoka

Mkuu hayo ndo Matakwa ya Democracy.
Na kumbe kelele za Ccm ndo zinakua msingi wa Maamuzi ya Cdm?
Kumbe ni sahihi Mh. Alipozuia mikutano maana ana nia njema ya kuinyoosha nchi na hata kelele za kumyumbisha.
 
Hivi waliotangaza kuwa maisha ni magumu sana mabasi yamepaki hamna abiria wa kusafiri, wanajisikiaje kuona watu wamekosa mabasi ,na wengine wakidandia coaster kwa nauli mara mbili.

Aibu ya kufungia mwaka hii.
 
mbona tulisha jua, ajenda ya mbowe ni kukwepa makada ya lowasa kuwa wajumbe wa baraza kuu, kwa kuwa sasa mbowe haliziki na uwepo wa lowasa
 
Sosopi ni Team lowassa Msigwa ni Team Mbowe...finito.

WACHA MANENO WEKA MUZIKI
Unafikiri siku hizi kuna watu wanagombanishwa kitoto hivyo?

We kweli jinga lao lumumba
 
Hayo mkazungumzie huko kwenu maamuzi yaliyofanywa yamezingatia mambo Mengi sana kwa akili yako ndogo huwezi kujua
 
Acha uongo na unafiki, tupo naye kila siku Iringa, labda kama kuna dar ya Iringa.
Na si muongo tu bali ni juha kabisa wabunge wa Ccm ndiyo wanoishi dar hiyo ni toka zamani mpaka sasa ndiyo maana hata nyumba tu hawana hapa Iringa tofauti na Msigwa hajawahi ishi dar kama ambavyo wamekudanganya waliokwambia
 
Sasa kwanini mnampinga Rais akifanya ivo kwa maendeleo ya taifa.

..kwangu mimi katiba za vyama hazina uzito kama Katiba ya NCHI.

..hata ccm wakifanya mambo yao ya ndani kwa maslahi ya chama chao siwezi kuwapinga.
 
Du! Nyie wazee mna mahaba na unafiki sana...
Mbowe akikacha katiba ni sawa na unaipamba kabisa kuwa ni kutumia busara ikitokea pande ya pili ni udikteta, kweli wa Tz ni wa Tz tu.

..hapana.

..Magufuli akifanya maamuzi kinyume na katiba ya ccm hutanisikia nikimpinga.

..kwangu mimi katiba ya NCHI ina uzito kuliko katiba za vyama vya siasa.

..lakini hata katiba za vyama zinapokiukwa ni lazima nijiridhishe na sababu za kufanya hivyo.

..kwa suala la Ole Sosopi naamini angepitishwa tuhuma za cdm kupendelea wenyeji wa kaskazini zingepamba moto. Kazi ya kukijenga chama kanda ya ziwa Nyasa ingekuwa ngumu zaidi.

Cc runyaga
 
..YES.

..kama hali halisi inalazimisha hivyo ili kukiwezesha chama kuongeza ushawishi ktk kanda ya Nyasa.
Basi namna tena moral authority ya kuikosoa ccm au Magufuli kwamba wanasigina demokrasia...unafiki siyo mzuri kabisa
 
Ukianza kusigina katiba ya chama chako kwa maslahi binafsi kitu gani kitakuzuia kusigina katiba ya nchi kwa maslahi binafsi? Acheni unafiki nyie wazee
 
sosopi na mwenyekiti wako wa BAVICHA mmepoa sana tofauti na kipnd cha ndg HECHE,vjana hamzunguki kuwaelimisha vjana kwa kuwapa elimu ya uraia sijui kwa nn? na niny mmesha anza kuiga matamko ya wazee wa chadema na kuwa kimya kama mhako vile'
 
Basi namna tena moral authority ya kuikosoa ccm au Magufuli kwamba wanasigina demokrasia...unafiki siyo mzuri kabisa

..na kwanini cdm wahangaike kuikosoa ccm ktk masuala yao ya ndani ya chama chao?

..Katiba ya NCHI ina uzito kuliko katiba za vyama.

..tusijaribu hata kidogo kuziweka katiba hizo ktk mizani moja.
 
..Ole Sosopi angechaguliwa mashambulizi kwamba cdm inapendelea watu wa "kaskazini" yangepamba moto.

..sikubaliani na siasa za kikabila , lakini ni ukweli usiopingika kwa siasa hizo zipo hapa Tz, na ni mtaji mkubwa kwa CCM.

Cc Gamba la Nyoka
Kwani Sosopi anatoka Kanda ya kaskazini? Ninyi ndo walewale
 
..na kwanini cdm wahangaike kuikosoa ccm ktk masuala yao ya ndani ya chama chao?

..Katiba ya NCHI ina uzito kuliko katiba za vyama.

..tusijaribu hata kidogo kuziweka katiba hizo ktk mizani moja.
Kama MTU hawezi kuheshimu cha kwake ataheshimu vipi cha wrote/wengine?
 
Wabakaji wa demokrasia ninyi.

Tuna kila sababu ya kumuunga mkono JPM awashikie chini maana chama kinaendeshwa kufamilia, kienyeji na hovyo hovyo tu.

Sisi ni wanachama tena viongozi wa CDM lkn haturidhishwi na mwenendo wa Mwenyekiti Mbowe anavyokiendesha chama hiki atakavyo.

Unanyonga demokrasia ndani ya chama chako alafu Unataka demokrasia hiyohiyo nje ya chama,,,,,nani atakusikikiza? Mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu mchungu....

Hii haikubaliki hata kidogo na ni Bora tuache kuhubiri demokrasia maana ni unafki mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…