CHADEMA imekuwa dampo la CCM

Nianze kwa kuwasalim wakuu
Kwanza kabisa sina kadi ya chama chochote bali ni mtanzania ninayefuatilia siasa za nchi yangu kwa undani.

Katika kila taifa kuna aina mbili za kuimarisha upinzani
Njia ya kwanza ni kwa upinzani kuombea kumeguka kwa chama tawala hasa ukizingatia kuwa nchi yetu ilikuwa na chama kimoja

Mifano ya njia hii iko mingi lakini wa karibu kabisa ni nchini Kenya

Njia ya pili ni kwa wale waliozaliwa katika mfumo wa vyama vingi na wakaelewa kwa nn wapo upande pinzani na chama tawala
Njia zote zinategemeana na lengo ni moja tuu katika kuuimarisha upinzani kwani upinza imara utoa nafasi ya chama tawala kujikosoa

Napendelea tanzania tuwe na upinzani imara lakini si upinzani huu unaofanywa na chama kikuu cha upinzani CHADEMA
Ni ukweli usiopingika kuwa kila mtu ana haki ya kuwa mwanachama wa chama chochote pasi kuvunja sheria na katiba ya nchi, lakini sasa CHADEMA wamekuwa watumwa wa makandokando ya CCM

Hii inaonesha kuwa chama kikubwa cha Upinzani hakina uwezo wa kutengeneza watu wake mpaka itegemee makando ya chama tawala

Hii halitatupa upinzani mzuri hivyi pia chama tawala kitakuwa legelege kwani hakitaweza kujitathimini

Upinzani imara ndio msingi wa nchi imara na si upinzani wa kutegemea makandokando

Kwani hayo makandokando hayataweza kamwe kujitofautisha na kule watokapo
Asanteni
 
mwanzo kabla ya 1992 hao wapinzani walikuwa vyama gani? kama walitoka ccm basi kila mmoja ana uhuru kuendelea kuchagua chama akipendacho
 
Hakuna tulicholithi kwa wazungu hapo, yaani nachukia sana.
 
Betony unategemea utawapata wapi wanachama wasio na chama??
Si kwamba napinga chama kutegemea wanachama toka chama kingine hapana
Ni kwamba chama kikuu cha Upinzani kwa zaidi ya miaka hii ishirini ya vyama vingi kiatakiwa kiwe na uwezo wa kuweza kutengeneza wanachama wake na si kutegemea makandokando ya vyama vingine
 
mwanzo kabla ya 1992 hao wapinzani walikuwa vyama gani? kama walitoka ccm basi kila mmoja ana uhuru kuendelea kuchagua chama akipendacho
Ni zaidi ya miaka ishirini sasa
Kutegemea makandokando hakukutofautishi na pal yalipotoka
 
Siasa ni kama mpira huwezi kuniambia Ronaldo kwenda Real Madrid eti Madrid ni dambo la Manchester United.Je Lowassa akirudi CCM Kwa hiyo CCM in dambo la chadema?
 
Siasa ni kama mpira huwezi kuniambia Ronaldo kwenda Real Madrid eti Madrid ni dambo la Manchester United.Je Lowassa akirudi CCM Kwa hiyo CCM in dambo la chadema?
Wema asingekamatwa na bangi, angehamia chadema?

Lowasa asingekuwa fisadi na kukatwa angehamia chadema??
 
Naomba kueleweshwa tu kama chadema ni chama cha wahalifu au la.

Kila anayetuhumiwa ndani ya ccm kwa uhalifu uwe ni ufisadi au dawa za kulevya utamsikia anakimbilia chadema.

Ni vema Chadema mkajitafakari kabla ya Watanzania kufanya uamuzi juu yenu mwaka 2020 na kujikuta hampati hata 5% ya wapiga kura wote.

Si kila ndege huliwa la hasha wengine wana sumu kali.
 
Kuhama chama hakuna mwanachama anayekatazwa yaan vyama ni kama timu za mpira....kumbuka machali moses kaamia ccm mbn hamjasema matapishi
 
Juzi juzi ccm IMEVUNA wana CHADEMA zaidi ya elfu 1. Ccm ni dampo la CHADEMA
 
Kuhama chama hakuna mwanachama anayekatazwa yaan vyama ni kama timu za mpira....kumbuka machali moses kaamia ccm mbn hamjasema matapishi
Chama kina katiba, pia kina miiko ya viongozi.

Je leo hii chadema watakuwa na ubavu wa kutoka mbele na kukemea ufisadi?

Leo hii chadema wana ubavu wa kukemea wauza madawa ya kulevya??
 
Mfamaji.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…