Tunaambiwa siasa zinabadilika (Political dynamics).
Mabadiliko ya siasa za Tanzania yanafanya watu wenye fikra pana wajiulize kuhusu hatima ya taifa na misingi ya vyama vya siasa.
Kwa kifupi, kile ambacho CHADEMA walikitetea, kwa sasa wanakipinga na kile ambacho CCM walikipinga kwa sasa wanakitetea!
Uchaguzi Mkuu uliopita, CCM walikuwa wanatetea sana ufisadi na mafisadi, kwa sasa kazi hiyo wameichukua CHADEMA.
Uchaguzi Mkuu uliopita, CCM ilikuwa inapinga sana midahalo ya wagombea Urais, kwa sasa kazi hiyo wameichukua CHADEMA.
Uchaguzi Mkuu uliopita, CCM walikuwa wanajitetea sana kuhusu uwezo wa mgombea Urais akiwa jukwaani, kwa sasa kazi hiyo wameichukua CHADEMA.
Uchaguzi Mkuu uliopita, CCM walidaiwa kuwa na wataalam wa kuiba kura, kwa sasa tunaambiwa CHADEMA pia wamesajiri watu wenye utaalamu wa kuiba kura.
Uchaguzi Mkuu uliopita, Mgombea Urais wa CCM alidaiwa ni mgonjwa baada ya kuanguka katika mkutano wa hadhara, kwa sasa CHADEMA wanadaiwa kuwa na mgombea Urais mgonjwa kutokana na afya yake kudhoofu ukilinganisha na miaka minane iliyopita.
Haya ndiyo mabadiliko ya siasa za Tanzania ambayo kwa sasa yanapigiwa upatu na vyama vya CCM na CHADEMA.
Kweli siasa ni mabadiliko!