CHADEMA imekuwa CCM, CCM imekuwa CHADEMA!

CHADEMA imekuwa CCM, CCM imekuwa CHADEMA!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Tunaambiwa siasa zinabadilika (Political dynamics).

Mabadiliko ya siasa za Tanzania yanafanya watu wenye fikra pana wajiulize kuhusu hatima ya taifa na misingi ya vyama vya siasa.

Kwa kifupi, kile ambacho CHADEMA walikitetea, kwa sasa wanakipinga na kile ambacho CCM walikipinga kwa sasa wanakitetea!

Uchaguzi Mkuu uliopita, CCM walikuwa wanatetea sana ufisadi na mafisadi, kwa sasa kazi hiyo wameichukua CHADEMA.

Uchaguzi Mkuu uliopita, CCM ilikuwa inapinga sana midahalo ya wagombea Urais, kwa sasa kazi hiyo wameichukua CHADEMA.

Uchaguzi Mkuu uliopita, CCM walikuwa wanajitetea sana kuhusu uwezo wa mgombea Urais akiwa jukwaani, kwa sasa kazi hiyo wameichukua CHADEMA.

Uchaguzi Mkuu uliopita, CCM walidaiwa kuwa na wataalam wa kuiba kura, kwa sasa tunaambiwa CHADEMA pia wamesajiri watu wenye utaalamu wa kuiba kura.

Uchaguzi Mkuu uliopita, Mgombea Urais wa CCM alidaiwa ni mgonjwa baada ya kuanguka katika mkutano wa hadhara, kwa sasa CHADEMA wanadaiwa kuwa na mgombea Urais mgonjwa kutokana na afya yake kudhoofu ukilinganisha na miaka minane iliyopita.

Haya ndiyo mabadiliko ya siasa za Tanzania ambayo kwa sasa yanapigiwa upatu na vyama vya CCM na CHADEMA.

Kweli siasa ni mabadiliko!
 
CCM ndio imekuwa mtetezi wa wanyonge dhidi ya makabaila.
 
Kweli. Ndo maana Makomeo hakumnadi Chenga! Na Timbanyuka wala hakupitishwa kugombea ubunge! CCMscrow ni waterezi wa wanyonge hasa.
 
CDM wanatetea ufisadi? Una wazimu sana wewe. CDM ndio inapinga ufisadi. Shida yenu ni maisha ya kukariri, Lowassa kawashika pabaya. Ufisadi haukemewi kwa mdomo.
 
Kama wewe fisadi ukitaka uwe salama nenda Chadema, watakukodia na TV kukusafisha.!
 
Kama wewe fisadi ukitaka uwe salama nenda Chadema, watakukodia na TV kukusafisha.!

wtcoj.jpg


CDM-TV
Copyright 2010
 
CDM wanatetea ufisadi? Una wazimu sana wewe. CDM ndio inapinga ufisadi. Shida yenu ni maisha ya kukariri, Lowassa kawashika pabaya. Ufisadi haukemewi kwa mdomo.

Chadema ya leo inapinga ufisadi? Chadema ya leo inasema ufisadi haukemewi kwa mdomo? Kwakwakwakwakwa
 
Zitto bana mbona wewe unanadiwa na Kikwete?
 
Last edited by a moderator:
Siasa haina adui wa kudumu wala haina rafiki wa kudumu.
Stukaaaaaa!!
Hizi ni hoja zinazotumiwa na wanasiasa ili waendeleze ulaghai wao kwa wananchi.

Siasa ina misingi ambayo ukiiacha inaondoa uhalali wako kama mwanasiasa kwa kile unachokisimamia.
 
Back
Top Bottom