Wewe ni muongo sana dahHuh? Mimi ni nani??? Ahahahaaaaa yaani nyie watu bana!!!
Magufuli made it so hard for Trojan horses like you.Jukumu la kudai demokrasia katika Tanzania sio la CHADEMA pekee bali ni la kila Mtanzania. Tunapoteza muda mwingi kuangalia CHADEMA imefanya nini au imefanywa nini badala ya kuiangalia Tanzania.
Sera nyingi zinazofanywa na Magufuli zitarudisha taifa nyumba sana. Magufuli ameua vitu vyote vinavyoweza kufanya vyama kujijenga: kuanzia mikutano ya siasa; kununua wabunge; kuwaminya Bungeni; kuwapiga na wakati mwingine kuwaumiza n.k. Vitu hivi vimeviweka vyama vya upinzani kwenye wakati mgumu sana.
Nyani Ngabu, kwa nyongeza uongozi wa juu wa CHADEMA uliridhika na kupata wabunge wengi kupitia umaarufu wa Lowassa. Lakini badala ya kuendelea kumtumia kikamilifu kukijenga chama, tunashuhudia ni kama hana nafasi ndani ya chama. Matokeo yake wamejitokeza makamanda (uchwara) ambao wamekuwa wasemaji wakuu wa chama, tena kwa lugha isiyo staha, ambayo haijawahi kutumika kwenye medani ya kisiasi nchini.Hiki chama kikuu cha upinzani baada ya uchaguzi wa 2015, badala ya kuendelea kukua, sasa ni dhahiri kabisa kuwa hakifanyi hivyo bali kimedumaa, kinazidi kudumaa, na kimedhoofu sana.
Wengi wetu tiliona jinsi chama hicho kilivyoendelea kustawi baada ya uchaguzi wa 2010. Kati ya 2010 hadi 2015 chama kilikua, kilistawi, hadi kikawa tishio la kweli dhidi ya CCM na kukifanya chama hicho tawala kulazimika kufanya mabadiliko na kimsingi kukiri kwamba ufisadi ni tatizo kubwa.
Sasa toka 2015 mpaka hivi sasa hiki chama ni kama kimechanganyikiwa kabisa. Hakijui hata kifanye nini. Kutwa kucha kinapoteza wanachama wake wanaohamia CCM. Kinapoteza wabunge, madiwani, na kadhalika.
Wenye chama, kwa mujibu wa kauli na matendo yao, wanaona eti hakuna tatizo. Mbunge akikihama na kwenda CCM, wenye chama wanakuja na majibu yaliyo 'formulaic'. Oh...kanunuliwa huyo...oh wamenunuliwa hao.
Kwa mtindo huu, hadi kufikia 2020, kama hicho chama hakitajitafakari na kufanya mabadiliko, basi kitaingia katika huo uchaguzi mkuu kikiwa dhoofu kushinda wakati mwingine wowote ule.
Kuhusu CUF, ACT, TLP, UDP, na wengineo, who really gives a damn about them? Vimefubaa.
Naisubiri kwa hamu Oktoba nione nani mwingine atayeitosa CHADEMA na kuhamia CCM.
Yours very truly,
Big Bad Wolf.
Mkuu ni kweli kabisa kuwaza tofauti na Bandiko la Nyani ni kutokuwa Mtanzania?? Hatutakiwi kuwaza Tofauti??Nyani ngabu wakati mwingine unapotea sana kulikon mkuu.
Ulicho andika ni ukwel sana atakaibisha labda awe si mtanzania
Nyani huwa namwelewaga sana kwa nondo. Mzee wa lugha ya malkia.
Nyani Ngabu, kwa nyongeza uongozi wa juu wa CHADEMA uliridhika na kupata wabunge wengi kupitia umaarufu wa Lowassa. Lakini badala ya kuendelea kumtumia kikamilifu kukijenga chama, tunashuhudia ni kama hana nafasi ndani ya chama. Matokeo yake wamejitokeza makamanda (uchwara) ambao wamekuwa wasemaji wakuu wa chama, tena kwa lugha isiyo staha, ambayo haijawahi kutumika kwenye medani ya kisiasi nchini.
CHADEMA watavuna walichopanda
sabha kwenda utanyangaNshenji gete ubhebhe.