Kzi kweli kweli, sikijua kumbe hata rangi za bendera nazo huwa zinaweza kuleta mvuto hata wananchi wakuunge mkono, hili kwangu nalo jipya! so kumbe hata Africa kusini nao wametuiga sisi Watanzania rangi za bendera yetu so maana wao wameendelea kuliko sisi, jamani, hivi wazo la katiba mpya, hapa wakulaumiwa nilidhani ni ccm, kwenye irani yao ya uchaguzi hili suala halikuwepo, mawaziri wao walikataa kabisa issue ya katiba mpya, mwanasheria mkuu wa serikali naye pia alikataa kuwa na katiba mpya, then Kikwete akasoma upepo akaanzisha mchakato wa hili, hivi hapa wa kulaumia ni CDM kweli? Hapa bwana Ibrahim asipotoshe historia, mwanzoni kabisa mwa mageuzi, enzi hizo sultani alikuwa mshauri wa uchumi wa bwana Mwinyi, akina Mabere Marando (NCCR mageuzi), Abdul Fundikila (UMD), James Mapalala (CUF, mwanzilishi) Mzee Mtei (CDM) walikutana Diamond Jubilee, miongoni mwa mambo waliyazungumza, katiba mya ilikuwepo, hili suala hata Prof Issa Shivji aliliandika sana enzi hizo kwenye magazeti ya Kingereza, narudia, ni enzi hizo, mwaka 1992, Lipumba wakati huo alikuwa mshauri wa uchumi.
Suala la serikali 3, hili nalo, naomba tuweke record vizuri hapa, hii kitu, CUF wasidandie umaarufu, hata CDM sio waasisi wa hiki kitu, nenda kwenye report ya Marehem Jaji Jalali, alipotumwa kukusanya maoni ya mfumo wa vyama vingi, maoni ya Watanzania wengi, pamoja na kile walicho ki sema juu ya chama kimoja au viwili, lakini issue ya muungano iliingia hapo, wengi walitaka mfumo wa serikali 3, Bungeni, i think wengi tunakumbuka ile kitu ilikuwa ikiitwa G 55 ikiongozwa na akina Tumtemeke Sanga (Makete) na wengineo, hawa walikuwa wabunge wa ccm, walitaka serikali ya Tanganyika irudi so, maanake walitaka serikali 3, kama sio mkwara wa Nyerere, leo hii tungekuwa na Zanzibar, Tanganyika na serikali ya muungano, hapa CUF inaingiaje? Mi nafikiri, CUF na CDM wamechukua kile wenye nchi wanataka then wakakiweka kwenye mikakati yao.
Suala la mwisho hapa ni hili, nashangaa sana kwa chama cha CUF kuipinga CDM while indirect unaunga mkono ccm, hivi bado unastahili kuitwa chama cha upinzani? Sasa ndo nimeelewa, ni kwanini Freeman Mbowe alikataa kuunganisha nguvu bungeni na hawa, i now understand why.