Gerald .M Magembe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 2,495
- 1,802
Kama ni hivyo kwa nini wali kuwa wakipinga chochote alichofanya Magufuli?Wewe siyo mtu MAKINI. Kama ungefuatilia aliyotenda Magufuli 2016-20 alikuwa anatembea kwenye Ilani ya CDM. Walichotofautiana CDM na Magufuli ni kukandamiza DEMOKRASIA, Utawala bora, kukanyaga Katiba, kukandamiza uhuru wa kujieleza na UDIKTETA. Lete kingine au funga mdomo
Bado sana, usijiaminishe hivyo kirahisi rahisi. Kaa Chadema halafu ujihusishe na siasa za CCM kwa muda, utakuja kutuelezea tofauti ya hivi vyama na nguvu zake kwa wananchi. Tumepita huko kwa miaka zaidi ya Ishirini.CCM wanatumia dola kubaki madarakani. CHADEMA wana nguvu ya wananchi yakuwaweka madarakani. Muda utaongea.
ccm au polisi ?CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu sana.
Umeeleza vizuri sana kuhusu kupeleka chama mpaka ngazi ya chini kabisa, lakini kipimo changu huwa jimbo lá Hai ambapo mzazi wangu mmoja ni mkazi.Mkuu nimependa hoja yako lakini hili suala lilifanyiwa kazi tokea 2012 ilipoanzishwa CHADEMA ni msingi na ndio iliopelekea hata kuimarishwa kwa kanda ili chama kishuke kwenye grassroots.
Kwahyo utekelezaji ulianza changamoto iwe ni ufuatiliaji tu lakini tukiwa wakweli CHADEMA imefanikiwa sana kushuka chini tofauti na miaka 10 iliyopita. Leo hii kanda zina ofisi zao na zinaendesha oparesheni bila kusubiri makao makuu so kuna hatua zimechukuliwa ila changamoto ni pesa tu maana wengi hapo wanajitolea tu zao mfukoni.
Nakushauri jitahidi kutembelea vijijini na hasa sehemu Chadema haina wafuasi sugu halafu utakuja kuandika ulichokiona.Mkuu CHADEMA ilijijenga kupitia Agenda ya kupigania haki za wananchi hasa kiuchumi pale walipopambana na ufisadi, pingana na mikataba ya kinyonyaji na sheria kandamizi bungeni na majukwaani.
However toka awamu ya 5 inaingia utoaji taarifa umebanwa sana na uhuru wa kufanya siasa bungeni na majukwaani ulipokwa hata vikao vya ndani tu ikawa shida. Hii ilipelekea panic hasa upinzani hadi ikabidi wengine wahamie CCM ili kunusuru political career zao.
Maadam ameingia kiongozi mpya ambaye naamini ni lenient kidogo kuliko aliyetoka. Hivyo naona upinzani ukipata motisha mpya na kurudi kwa nguvu zaidi kusimamia agenda zao ambazo wengi waliziacha kwa hofu ya kumiminiwa risasi au kuswekwa ndani kwa makosa ya Uchochezi!!
But all in all CHADEMA haikuwahi acha kusimamia agenda zake hii ni kma ulikua unafuatilia michango yao bungeni na vitabu vya sera toleo la 2018. Otherwise waliendeleza struggle kupitia CHADEMA ni msingi na ofisi za kanda na kma uchaguzi ungekua huru trust me wange retain majimbo mengi tu na kata mpya nyingi na hapo tungefanya evaluation nzuri zaidi.
Soma tena sentensi yangu ya pili kuna jibu pale ulipo ni quoteKama ni hivyo kwa nini wali kuwa wakipinga chochote alichofanya Magufuli?
Kama CHADEMA wangepinga kila alichofanya Magufuli, na Magufuli akawa hafanyi aliyoyaeleza huyo uliyemjibu , Stuxnet hapa, CHADEMA inawezekana wakati huu ingekuwa haipo kabisa!Kama ni hivyo kwa nini wali kuwa wakipinga chochote alichofanya Magufuli?
Nimetembea sana vijijini mkuu..... Wakati wa kampeni za uchaguzi nilikua mikoa ya magharibi yaani Tabora,Kigoma, na Mpanda. Aiseee CHADEMA ina hard core followers wengi tu tena maeneo ambayo sikutarajia kabisa hasa vijana ambao ndio wengi nchini na wamezaliwa enzi za vyama vingi so to them CCM means nothing.Nakushauri jitahidi kutembelea vijijini na hasa sehemu Chadema haina wafuasi sugu halafu utakuja kuandika ulichokiona.
Wakati Chadema inatawala mkoa wa Kilimanjaro CCM walikuwepo japo wsmepungua lakini wakiwa na Mapenzi ya chama chao ya kufa mtu.
CCM ina wapenzi wa kweli Kilimanjaro nadhani kuliko maeneo mengi. Iwe Upareni, Uchagani na hata maeneo mengine. Na wanajitoa kuliko vyama vingine.
CHADEMA wanaweza kuwa wamejiridhisha kuwa wamekwishafanya kazi kubwa ya kukipeleka chama kwa wananchi, hadi huko mitaani; na kama hivyo ndivyo ilivyo kweli inabidi wajitafakari sana kwa sababu bado kuna alama zinazoonyesha kwamba juhudi zao hizo bado hazijawa na mafanikio ya kutosha.Nakushauri jitahidi kutembelea vijijini na hasa sehemu Chadema haina wafuasi sugu halafu utakuja kuandika ulichokiona.
Wakati Chadema inatawala mkoa wa Kilimanjaro CCM walikuwepo japo wsmepungua lakini wakiwa na Mapenzi ya chama chao ya kufa mtu.
CCM ina wapenzi wa kweli Kilimanjaro nadhani kuliko maeneo mengi. Iwe Upareni, Uchagani na hata maeneo mengine. Na wanajitoa kuliko vyama vingine.
Hai ni sample ndogo sana embu fika mkoa wa songwe au kigoma na Mara.... Huko kuna followers wengi sana shida ni kwamba hakuna tu mikutano ya siasa na uhuru wa kufanya siasa za ushindani kama enzi za kikwete but trust me chama kipo hai kabisa na nadhani uliona mapokezi ya Lissu yalivyokua kanda ya ziwa na magharibi!!Umeeleza vizuri sana kuhusu kupeleka chama mpaka ngazi ya chini kabisa, lakini kipimo changu huwa jimbo lá Hai ambapo mzazi wangu mmoja ni mkazi.
Kunatakiwa kuimarishwe sana, labda kwa kuwa Wilaya ya Hai uongozi wote kuanzia nyumba kumi, wajumbe na Madiwani pamoja ofisi za Chadema kutumikia kama vijiwe vya CCM tunashindwa kukaa na kupima matokea ya Chadema Msingi.
Naomba ni object hiliCHADEMA wanaweza kuwa wamejiridhisha kuwa wamekwishafanya kazi kubwa ya kukipeleka chama kwa wananchi, hadi huko mitaani; na kama hivyo ndivyo ilivyo kweli inabidi wajitafakari sana kwa sababu bado kuna alama zinazoonyesha kwamba juhudi zao hizo bado hazijawa na mafanikio ya kutosha.
Inaeleweka, mazingira magumu sana yaliyokuwa yakiwakabili kufanya kazi zao maeneo yote nchini, lakini ni lazima wawe na muda wa ku'evaluate' matokeo ya juhudi hizo, hasa wakati huu tunapoingia kwenye hali iliyo tofauti kidogo na iliyokuwepo miaka mitano iliyopita.
Ni lazima watafute njia za kujua CHAMA chao kina hali gani huko mashinani, na kurekebisha panapohitaji kurekebishwa. Wakati ndio huu, na hawahitaji kabisa kumtangazia yeyote kuwa kazi hiyo inafanyika.
Hawawezi kuwa wanajiaminisha tu kuwa wamekwishafanya kazi za kukieneza chama bila kuwa na matokeo/majibu ya uhakika wa kazi hiyo.
Wao wanapenda sana hizi siasa za kwenye majukwaa, kazi muhimu za mtu kwa mtu huko mitaani inawawia ngumu sana kuifanya.
Mkuu, nikupongeze kwa hali hiyo hapo ulipo.Naomba ni object hili
Kata nayoishi huwa kila jumatatu wanakutana kufanya evaluation ya hali ya kisiasa kuanzia level ya kata,mtaa hadi kitongoji na uongozi upo kabisa ukiwa na kamati tendaji/sekretarieti functional kabisa.
Kwenye hivyo vikao hupeana milestones za kueneza chama, kukaribisha wanachama wapya, kujijenga mashinani kupitia PR nzuri, kufanya shughuli za kijamii n.k
Sasa kama haya yanafanyika wala 50% ya kata zote Tanzania then trust me CHADEMA ipo imara na kabla ya uchaguzi wowote tayari wana kura million 2 za kuanzia irrespective mgombea ni nani!!
Nimetoa experience yangu kwa ngazi ya kata yangu so naweza conclude kuwa hatutegemei siasa za majukwaani otherwise tusingeweza toa challenge kwa CCM despite mazingira magumu ya 2020
Hakuna shaka yeyote, na sidhani kwamba kuna mtu anayeweza kuhoji uwepo wa CHADEMA kama chama cha kisiasa kilicho na ushindani mkubwa hapa nchini licha ya misukosuko mingi iliyoelekezwa kwao ili kuwamaliza kabisa katika miaka mitano na zaidi sasa iliyopita.
Ni sawa kabisa kusema kwamba CHADEMA wamepitia kwenye tanuru la moto mkali, na wamepikika sawasawa kuweza kuendelea na pilkapilka zao za kisiasa na kutafuta njia ya kuliongoza taifa hili.
Sioni mbele yao, kupata hujuma tena, kama walizozipata miaka hii ya karibuni chini ya utawala wa Marehemu Magufuli. Tanzania itakuwa na bahati mbaya sana, kama patatokea hivi karibuni misukosuko iliyolitingisha taifa kama ilivyotokea wakati wa serikali ya Magufuli.
Watu wanaweza kuhoji kwamba kuendelea kuwepo kwa CCM madarakani hiyo ndiyo hatari kubwa kwa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani.
Mimi hilo silioni hivyo kwa sasa, na hata katika CCM ya enzi za Kikwete. Hatari iliongezeka zaidi alipoingia madarakani Magufuli na kutangaza waziwazi kutopenda uwepo wa vyama vya upinzani.
CCM wenyewe kama chama, hila zao zilikuwa ni za kawaida, mradi tu wanapata ushindi, hawakuwa na lengo maalum la kuua upinzani.
CHADEMA wafanye nini (samahani kwa kuwasema CHADEMA, badala ya vyama vya upinzani, kwa sababu vingine ndio hivyo tena vimetekwa).
Huu ni wakati wa CHADEMA kuwa wazi kabisa na sera zao. Wananchi waelewe chama kinasimamia nini.
Kati ya sifa chache, lakini muhimu alizojijengea Magufuli (sio CCM) ni kuonekana kuwa mtetezi wa mali na utajiri wa nchi hii na maendeleo ya wananchi wake.
Amejitambulisha bila shaka yoyote, kwamba yeye alikuwa ni mtetezi mkubwa wa maslahi ya Tanzania na wananchi wake. Amejenga hata ukuta, kulinda Tanzanite yetu iliyokuwa inatoroshwa kwenda nchi za nje na kuwanufaisha hao zaidi ya sisi tulivyokuwa tunanufaika kwayo.
Swala la madini aliliwekea mkazo sana; hata kama ilionekana kama kulikuwa na makosa katika juhudi hizo, lakini wananchi walielewa madhumuni yake. Kuna mifano mingi kuhusu msimamo wake juu ya mali za Tanzania.
Hatujui kuhusu mikataba mbalimbali nchi yetu iliyoiingia na nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa, lakini bado inaelekea wananchi waliamini kwamba mikataba hiyo ilikuwa ni kwa maslahi yao.
Jambo ambalo inawezekana hakulifanya vizuri ni kuhusu mashirikiano yetu na nchi mbalimbali duniani kwa vile alikazia zaidi "ubeberu" na mambo mengine kama masimango yao.
Nimeyaandika haya, ili CHADEMA watambue kwamba kama sera zao hazieleweki kwa wananchi, kazi yao itaendelea kuwa ngumu zaidi kuwashawishi wananchi hao kuwapa madaraka. Ni lazima wajieleze waziwazi kwa wananchi, wao ni nini hasa wanakisimamia kama chama cha siasa, na nchi yetu itafaidika vipi na misimamo yao hiyo kama watapewa ridhaa ya kuongoza serikali.
Kwa hiyo, nadhani ni halali sasa kusema kwamba adui mkubwa aliye mbele ya CHADEMA ni CHADEMA yenyewe. CCM wataendelea na hadaa zao kwa wananchi, hadaa za "Hawa ni Wenzetu" kama ilivyowahi kuwa huko nyuma, na wananchi kama hawaoni mbadala wa kuwapa madaraka, watarudi huko huko kwenye chama kilichooza ndani kwa ndani.
Niseme hapa, sijui kama Samia atakuwa na nguvu za kukibadilisha hiki chama kiwe chama cha wananchi wenyewe kwelikweli. Sijui.
Hatujui
Inawezekana sana kuna kitu ulichosoma kwenye hayo maandishi yangu kilichokuumiza sana hisia zako.kwa sasahv nawashauri mjikite kumsafisha lowasa aje kugombea tena 😂
Inawezekana sana kuna kitu ulichosoma kwenye hayo maandishi yangu kilichokuumiza sana hisia zako.
Unakijua mwenyewe.
Wewe siku zote najua ni mpuuzi.mm sio mgeni apa, na wewe sio mgeni tunajuana vizuri, kwenye mada wa kumsafisha mbowe na ofisi yake mpo vizuri, nlisoma tu title nkajua ni takataka maana icho chama nlishakihama mda mrefu na hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza fanya siasa kwenye hio ofisini yenu ya leo 1+1=2 kesho 1+1=3, miaka nenda rudi lowasa fisadi kipindi cha uchaguzi lowasa msafi, wafunge akile hao wengine mliobaki
Wewe siku zote najua ni mpuuzi.
Kwa hiyo sina muda na kupoteza wewe.