CHADEMA ime-savaivu, sasa nini?

CCM wakitaka watawale kwa raha,wasitulaze njaa tu kwa miradi yao aliyoiacha JPM,maana mh,tumepigika😂😂😂jamaa ametunyoosha

Wanawake,wanaume wote tunanyoa vipala kwa kwenda mbele🤓🤓
 
Ila Chadema ni chuma cha pua.Jiwe pamoja na figisu zote ameshindwa kuifuta chadema.Ameondoka ameiacha chadema!
 
Inasemwa, mara kwa mara; kwamba wanaofanikisha mipango mingi ya uchafuzi wa chaguzi, hasa huko mitaani ni hawa watu wa CCM walioko huko, kila sehemu.

Kuwepo kwa CHADEMA kwenye maeneo hayo, na wakawa tayari kabisa kuwakabili wenzao hao huko huko mitaani, nadhani hii itakuwa ni sehemu muhimu sana kwa CHADEMA kulinda haki yao.

Kumbuka, hawa wenye mabunduki wanaotumiwa na CCM, hawana mabunduki na mabomu ya machozi kila mtaa na kila kitongoji.
Wananchi watapata ujasiri sana wa kusimamia kura zao wakiona kwamba kuna uongozi mbele zao. Hawatakaa kimya kuona kura zao zikiharibiwa.

Kwa hiyo, kuwepo kwa CHADEMA hadi huko chini, sio faida ya kueneza sera zao pekee, bali pia wanawapa wananchi ujasiri wa kukataa uhujumu wa kura zao.

Ninakubaliana nawe juu ya hatua wanazo/walizochukua CHADEMA kwenda huko mitaani; nimeisikia sana habari hiyo. Nisichojua ni kiasi gani wamefanikiwa kuleta matokeo chanya kwa chama chao.
Lakini najua msemo wa wahenga kuhusu mji wa Roma.

Kama wamefika huko mitaani, basi kazi sasa ni kukaza kamba zaidi, pamoja na kuwa na hali ngumu ya ukata. Hao wanaojitolea kwa ajili ya chama wakati hali ikiwa ngumu, huenda ndio viongozi imara wa chama.
 
Ndiyo maana haya tunayaandika sasa mkuu NewOrder, kuwakumbusha/kuwahimiza CHADEMA. Zama zile zimepita, wasiendelee kubweteka.
Tunawapongeza kwa "ku'savaivu' hayo yote, wakabaki wamesimama; sasa ni mwendo wa kwenda mbele.

Tunayasema yote haya sasa kwa kuamini kwamba utawala wa kikatili kama aliouonyesha hayati Magufuli umeondoka naye.
Itakuwa ni bahati mbaya sana kwa taifa letu hili, aibuke mara moja hii wa kumfikia Magufuli katika eneo hili.

Kwa hiyo ni wakati mzuri kwa CHADEMA kufanya "SIASA za chama KOMAVU," wasije wakajisahau na kuendeleza siasa za kukandamizwa.
 
Mungu amejibu maombi ya wana Chadema na watanzania kwa ujumla.Dhulumaji Namba Wahedi wa kura,Kaelekea Jongomeo!
 
Ngoja nikwambie jambo mkuu wangu 'guwe_la_manga', CHADEMA wanastahiri kupewa pongezi sanaaana kwa waliyoyafanya katika miaka mitano ya hayati Magufuli.

Kazi hiyo kubwa waliyofanya ni kuepusha uhai wa waTanzania usipotee. Dalili zilikuwa wazi sana, kuwa jamaa alikuwa tayari sana kuiona damu ya waTanzania ikimwagika; na kwa ufundi mkubwa sana CHADEMA wakaiepusha.

Nikupe mfano mmoja uliotokea mapema kabisa - 'UKUTA' wa CHADEMA. Lile tukio lingekuwa ndio mwanzo wa damu kutiririka Tanzania.

Wapo waliosema CHADEMA wameogopa; sawa, na kama ni woga ndio uliosababisha UKUTA kutomwaga damu za waTanzania, woga ule ulikuwa ni woga mzuri. Hakuna kubwa sana walilopoteza CHADEMA kwa kutofanya maandamano yale; na kama yangefanyika wengi wao wangepoteza maisha na pengine wakati huu tusingekuwa tunaandika haya juu ya CHADEMA Ku'savaivu.

Kwa hiyo, CHADEMA walifanya vizuri kuwa wastahimilivu wa misukosuko mingi waliyopelekewa. Bila shaka wamejifunza mengi pia kutokana na uzoefu wa hiyo mikikimikiki iliyowapata.

Mwishoni tulianza kuona hisia za wananchi juu yao. Walipoitisha michango, wananchi waliitikia, kwa vile hapakuwepo na mabunduki ya kuwazuia wasiwachangie.
 
CCM WAJIFUNZE KUISHI NA CHADEMA AMA WAHAME NCHI VINGINEVYO CHADEMA WAPO MIAKA 1000
 
Well said.. Ngoja tuone
 
Kumbuka huyu unaemwita Nyoko ndio huyo aliye kufanya ukatambua nn maana ya uongozi wa umma kwa maslahi mapana ya Taifa
 
Mungu akulinde sana
 
Mungu akulinde sana
Mkuu 'Erythro', huyo jamaa kajibu kwa kujiamini sana, bila shaka ni mmoja kati ya viongozi wenu waandamizi.

Pamoja na hayo, tunaelewa sasa kwamba mmekwisha jpanga, lakini kazi inasubiri kufanywa.

Huo alioleza hapa ni muundo tu, mlioueneza hadi huko chini. Sasa fanyeni kazi huko huko mitaani.

Msisubiri wakati wa uchaguzi ndipo kazi ifanyike. Uhai wa chama chenu huko unategemea ufanisi wa kazi itakayofanyika huko, sio kuwepo kwenu huko.

Sasa huenda ukashindwa kuelewa ninachowahimiza hapa.

Wakati huu wa kimya kingi kisiasa nchini, ndiyo nafasi yenu ya kujijenga barabara nyumba kwa nyumba, kimya kimya huko huko vijijini/mitaani.

Hakuna sababu ya kupiga makelele mengi na kuwastua wabaya wenu.

Mkuu 'Zitto junior' kaeleza matatizo yenu ya kupungukiwa nyenzo za kufanyia kazi, lakini hilo pia linaweza kuwa ni motisha nzuri ya kujenga viongozi imara zaidi wasiotegemea kujazwa matumbo yao na kumbe vichwa vyao vikiwa kwingine. Kazi yenu kubwa hapa ni kuwatia mori hawa viongozi wenu huko matawina na wao kujua kwamba kazi zao zinatambulika kwenye chama.

Mwisho, kama kawaida yangu ya siku zote katika kuwashauri nyinyi- sera zenu ndiyo kila kitu katika kuwavuta waTanzania upande wenu.
Kubali au ukatae, hapa ndipo penye shida kubwa sana kwenu. Baadhi ya sera zenu ni ngumu sana kuziuza kwa Tanzania ya leo.

Kuzing'ang'ania hivyo hivyo, mradi mjionyeshe kuwa mpo tofauti sana na maisha wanayoyaishi waTanzania wa kawaida itaendelea kuwapa shida kubwa sana kuwashawishi waTanzania wawakubali, hata kama CCM wenyewe wameoza 'beyond recognition'.

Ninakuacha na haya machache.
 
Kumbuka huyu unaemwita Nyoko ndio huyo aliye kufanya ukatambua nn maana ya uongozi wa umma kwa maslahi mapana ya Taifa
Hamna kitu, linganisha na kiwango cha uharibifu alioufanya, halafu tafakari aina na namna ya kifo chake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…