CHADEMA ime-savaivu, sasa nini?

ajira ngapi zimeletwa ?
 
Bi Samia hawezi kukubali chama kifie mikononi mwake kwa hiyo suala la katiba mpya na tume huru hawezi hata kuvigusia. Sahau mkuu
 
Chadema inaongea Ccm inatenda, hapo ndipo tofauti inapokuja.
Chadema walileta habari za elimu bure ccm ikazifanyia kazi, hapo ndipo wanapowawini raia
 
Nyoko wenu hayupo kapewa kibano na Mungu kupitia korona anafukiwa futi 6 chini ya ardhi. Sasa uwanja wa mapambano umebadilika. Uaminifu kwenu umebakia kwa wadhaifu wachache ambao nao muda wao unayoyoma. TUTAELEWANA TU NA KUONGEA LUGHA MOJA. Sisi wenye chama cha CHADEMA hatutachoka kuwasitiri viongozi wetu kwa hali na mali na kuwakabidhi kwa Mungu.
 
Chadema inaongea Ccm inatenda, hapo ndipo tofauti inapokuja.
Chadema walileta habari za elimu bure ccm ikazifanyia kazi, hapo ndipo wanapowawini raia
Kama una watoto wanaosoma ungejua kama kuna elimu bure au kuna utopolo
 
Mama Samia akifungulia tu ajira na kupandisha mishahara Chadema mjue hamna chenu na hakuna atakae wasikiliza tena.
 
Kwa kutumia mtutu wa bunduki labda si kupitia uchaguzi huru na wa haki.
Uzuri wataalamu wa kuiba kura Mungu kawapangia majukumu mengine, ikiwemo kuongoza malaika.Ccm hawana jipya
 
Reactions: BAK
Sawa
 
Hakuna ccm imara bila upinzani imara,ccm ni tindo bila nyundo haiendi.Upinzani ndio chuo pekee cha Siasa kilichobakia.
 
Umesema sawa kabisa. Tatizo, inaelekea CHADEMA wenyewe wanachoamini ni kwamba wanafeli kwa sababu tu ya kuibiwa kura na hujuma zingine zinazofanywa na CCM. Sidhani kama wanaweka mkazo kwenye kuhakikisha wana sera mbadala zinazoeleweka kwa wananchi.

Sidhani ni swala la sera ndio linakiangusha CCM. Upinzani una maono sawasawa na CCM tofauti iliyopo ni kuwa siasa chafu ni sehemu kubwa sana ya siasa za nchi!! Upinzani hauna namna ya kuendesha siasa kwa maono yao. Hivi ni kweli umeshindwa kukumbuka misemo ya “Sera zinazotekelezwa ni za CCM?” - kwenye halmashauri upinzani ulishinda?? Ni halmashauri gani zilizokuwa zikiendeshwa na CCM madiwani walijiuzulu - utapata jibu kwanini mkazo wa kujiuzulu ulikuwa kwa halmashauri za upinzani!! Siaza zetu ni za kuzuiana, hata kama maana yake ni kuzuia jambo zuri kufanyika!! Chama kushika hatamu!!

Tunasahau mapema sana!!
 
Mkuu nimependa hoja yako lakini hili suala lilifanyiwa kazi tokea 2012 ilipoanzishwa CHADEMA ni msingi na ndio iliopelekea hata kuimarishwa kwa kanda ili chama kishuke kwenye grassroots.

Kwahyo utekelezaji ulianza changamoto iwe ni ufuatiliaji tu lakini tukiwa wakweli CHADEMA imefanikiwa sana kushuka chini tofauti na miaka 10 iliyopita. Leo hii kanda zina ofisi zao na zinaendesha oparesheni bila kusubiri makao makuu so kuna hatua zimechukuliwa ila changamoto ni pesa tu maana wengi hapo wanajitolea tu zao mfukoni.
 

Umesahau!! Nia halisi ya CCM ilikuwa ni kuzuia siasa na kuzifanya ni za uchaguzi tu! Kuwa “uchaguzi umekwisha sasa tujenge nchi”!! Kuwa anayeruhusiwa kufanya siasa ni mshindi wa eneo husika tu! Hii ikawafanya viongozi wa kitaifa wa Chadema kushindwa hata kufanya siasa za ndani. Ni mikutano mingapi ya ndani ilizuiwa kwa kuwa ilikuwa ikihusisha viongozi wa kitaifa?? Na wakati huo huo Polepole, Bashiru na marehemu wakizunguka nchi nzima wakifanya mikutano na kupokea wanachama na viongozi walioasi upinzani??!!

CCM imetumia dola kufanya siasa! Madhaifu ya Chadema yameletwa kimkakati, unachoona kama ni kushindwa kwa Chadema ni matokeo ya mikakati ya CCM na serikali. Kama vile unacheza mechi dhidi ya mpinzani wako ambaye ana refa, VAR na FA upande wake!!!
 
Mkuu CHADEMA ilijijenga kupitia Agenda ya kupigania haki za wananchi hasa kiuchumi pale walipopambana na ufisadi, pingana na mikataba ya kinyonyaji na sheria kandamizi bungeni na majukwaani.

However toka awamu ya 5 inaingia utoaji taarifa umebanwa sana na uhuru wa kufanya siasa bungeni na majukwaani ulipokwa hata vikao vya ndani tu ikawa shida. Hii ilipelekea panic hasa upinzani hadi ikabidi wengine wahamie CCM ili kunusuru political career zao.

Maadam ameingia kiongozi mpya ambaye naamini ni lenient kidogo kuliko aliyetoka. Hivyo naona upinzani ukipata motisha mpya na kurudi kwa nguvu zaidi kusimamia agenda zao ambazo wengi waliziacha kwa hofu ya kumiminiwa risasi au kuswekwa ndani kwa makosa ya Uchochezi!!

But all in all CHADEMA haikuwahi acha kusimamia agenda zake hii ni kma ulikua unafuatilia michango yao bungeni na vitabu vya sera toleo la 2018. Otherwise waliendeleza struggle kupitia CHADEMA ni msingi na ofisi za kanda na kma uchaguzi ungekua huru trust me wange retain majimbo mengi tu na kata mpya nyingi na hapo tungefanya evaluation nzuri zaidi.
 
Dr slaa? Mbona jimboni kwake waliipa CHADEMA kuanzia ubunge hadi halmashauri? Sidhani kma hyo ni sababu....... Otherwise Lissu asingepata mapokezi ya kishujaa vile Karatu.

Nachofahamu upinzani ni ideology sio mtu.... Ndio maana kina Slaa Zitto Mashinji wameondoka ila bado ni chama kikuu cha upinzani
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…