Chadema ilifanya makosa uteuzi wa Wabunge Viti Maalumu 2015

kuna baadhi ya wabunge walipelekwa baadhi ya mikoa sijui walipotokea. mfano mtu analetwa Shinyanga hata wenyeji tunajiuliza katokea wapi huyu?atakuwa na impact gani hata kukipromot chama. niliwahi kumtumia sms Mbowe,huu ni ujinga matokea yake mbunge hayupo jimboni miaka yote
Afadhali yako umekiri mnafanya ujinga
 
Hawa viti maalum ndio watafanya wengine ambao walikuwa wawe wazuri waonekane sio na wakose kupewa viti maalum, kwa sasa wapambanani haswa ndio wanaweza kupewa ila hawa wakuokota tu hapana wanachosha sana
Moja ya kasoro kubwa tulinayo watanzania tuliowengi ni kwamba hatupendi kukosolewa, zaidi sana hatupendi watu wenye mawazo tofauti na sisi.

Tabia hii tusipoiacha itatutesa sana. Tunapigana na kuumizana kwa sababu hatupendi kukosolewa.

Miongoni mwa wabunge wa viti maalumu walioteuliwa na Chadema mwaka 2015 , walikuwa na uwezo mdogo sana. Kiasi kwamba mtu ungeweza kushangaa iweje Chama chenye watu wenye akili kama Chadema kilifanya makosa makubwa kiasi hicho.

Nadhani kwa kuwa chama hiki kina watu makini basi naamini watakuwa wamejifunza jambo fulani hivi. Makosa haya hayatajirudia tena.
 
Kweli kati ya Vitu ambavyo sikuvipenda ni namna ubunge wa viti maalumu ulivyotolewa ndani ya Chama. Mfano wapigania Chama akina Nusrate Hanje walinyimwa kwa Hila na kuwapa watu ambao hata hawakijui Chama zaidi ya kupeperushwa na Wimbi la Lowasa. That has to be a teaching
 
Yes.
Kweli kati ya Vitu ambavyo sikuvipenda ni namna ubunge wa viti maalumu ulivyotolewa ndani ya Chama. Mfano wapigania Chama akina Nusrate Hanje walinyimwa kwa Hila na kuwapa watu ambao hata hawakijui Chama zaidi ya kupeperushwa na Wimbi la Lowasa. That has to be a teaching
 
Moja ya kasoro kubwa tulinayo watanzania tuliowengi ni kwamba hatupendi kukosolewa, zaidi sana hatupendi watu wenye mawazo tofauti na sisi.

Tabia hii tusipoiacha itatutesa sana. Tunapigana na kuumizana kwa sababu hatupendi kukosolewa.

Miongoni mwa Wabunge wa Viti Maalumu walioteuliwa na Chadema mwaka 2015, walikuwa na uwezo mdogo sana, kiasi kwamba mtu ungeweza kushangaa iweje Chama chenye watu wenye akili kama Chadema kilifanya makosa makubwa kiasi hicho.

Nadhani kwa kuwa chama hiki kina watu makini basi naamini watakuwa wamejifunza jambo fulani hivi. Makosa haya hayatajirudia tena.
Nadhani kosa kubwa kuliko yote walilolifanya ni kushindwa kuwagroom kuwa national figures kupitia mijadala bungeni.

Mkakati wa CHADEMA wa 2005- 2010 ulijenga wanasiasa wazuri sana kina Zito, Mdee, Owenya, Pauline Gekul, Lymo na wengineo walikuwa na uwezo mkubwa sana nadhani walikuwa wanafaidika sana na experience ya Dk Slaa na wabunge wa CUF chini ya Rashid Mohamed.

2010 - 2015 walipoibuka kina Mnyika, Lema, Msigwa, Silinde,Wenje, Tundu Lissu , Sugu na wale wa viti maalumu kulikuwa na ukomavu moubwa sana wa kihoja.

2015 -2020 pamoja na wingi wao lakini kulikuwa na ombwe la kihoja kwa kiwango kikubwa nadhani mazingira ya siasa ya awamu ya tano yalikiathiri sana chama tukashindwa hata kujenga personalities za wanachama wake waliokuwa bungeni ikiwemo kuchange their party agenda into national agenda kuwaconvert wabunge wake from mere political members into national figures.

Kwa wingi wao sasa hivi wangekuwa na ushawishi mkubwa sana nchini na kwa wananchi. Kuibuka law kina Catherine Ruge, Suzan Masele, Upendo Peneza, Nagenjwa kaboyoka, Kunti ,Saguti, prof Jay, John Heche, Jesca Kishoa na wengineo walipaswa mpaka tunaingia uchaguzi mkuu wawe national figures wa chama ambao wanaweza kuibua na kusukuma agenda za chama kuwa agenda za kitaifa.

Haya ndiyo mapungufu ambayo niliyaona mimi Mkuu wa kitengo cha Bunge kashindwa kutekeleza majukumu yake sawa sawa pale Chadema lakini pia wazee wa chama kuna mahali imepwaya.

Chama inakundi kubwa la wanasiasa wachanga ni kundi linalohitaji sana kujifunza kupitia kwa wanasiasa wakongwe wa mageuzi na kupata seminar za mara kwa mara za chama na vyama rafiki wa CHADEMA nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom